Mathayo 21:33-46, Mathayo 22:1-14 NEN

Mathayo 21:33-46

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Marko 12:1-12; Luka 20:9-19)

21:33 Za 80:8; Isa 5:1-7; Mt 25:14-25“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine. 21:34 Mt 22:3Wakati wa mavuno ulipokaribia, akawatuma watumishi wake kwa hao wapangaji ili kukusanya matunda yake.

21:35 2Nya 24:1; Ebr 11:36-37“Wale wapangaji wakawakamata wale watumishi, wakampiga mmoja, wakamuua mwingine, na yule wa tatu wakampiga mawe. 21:36 Mt 22:4Kisha akawatuma kwao watumishi wengine, wengi kuliko wale wa kwanza, nao wale wapangaji wakawatendea vilevile. Mwisho wa yote, akamtuma mwanawe kwao, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’

21:38 Ebr 1:2; Mt 12:14; Za 2:8“Lakini wale wapangaji walipomwona mwanawe, wakasemezana wao kwa wao, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, ili tuchukue urithi wake.’ 21:39 Mt 26:50; Mk 14:46; Lk 22:54; Yn 18:12; Mdo 2:32Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.

“Kwa hiyo, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?”

21:41 Mt 8:11-12; Mdo 18:6; 28:28Wakamjibu, “Kwa huzuni kuu atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.”

21:42 Za 118:22-23; 1Pet 2:7Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba:

“ ‘Jiwe walilolikataa waashi

limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Bwana ndiye alitenda jambo hili,

nalo ni la ajabu machoni petu’?

21:43 Mt 8:12“Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake. 21:44 Lk 2:34Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”

Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano ya Yesu, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 21:46 Mt 21:11, 26Wakatafuta njia ya kumkamata, lakini wakaogopa umati wa watu, kwa kuwa watu walimwona Yesu kuwa ni nabii.

Read More of Mathayo 21

Mathayo 22:1-14

Mfano Wa Karamu Ya Arusi

(Luka 14:15-24)

22:1 Lk 14:16; Ufu 19:7-9Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, 22:2 Mt 13:24; Yn 3:29“Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. 22:3 Mt 21:34Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.

22:4 Mt 21:36“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’

“Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua. 22:7 Lk 19:27Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.

22:8 Mt 10:11-13“Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. 22:9 Eze 21:21; Mt 13:47; 21:43Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ 22:10 Mt 13:47-48Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.

22:11 2Kor 5:3; Efe 4:24; Kol 3:10, 12; Ufu 3:4; 16:15; 19:8“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. 22:12 Mt 20:12; 26:50Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema.

22:13 Mt 8:12“Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

22:14 Ufu 17:14; Mt 20:16“Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.”

Read More of Mathayo 22