Mathayo 21:1-17 NEN

Mathayo 21:1-17

Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

21:1 Yn 8:1; Mdo 1:12Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 21:3 Mt 26:18Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”

21:4 Mt 1:22Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:

21:5 Zek 9:9; Isa 62:11“Mwambieni Binti Sayuni,

‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,

juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”

21:6 Mk 11:4Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 21:7 1Fal 9:13Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 21:8 2Fal 9:3Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 21:9 Mt 9:27; Za 118:26; Mt 23:29; Lk 2:14Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,

“Hosana,21:9 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe. Mwana wa Daudi!”

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Hosana juu mbinguni!”

21:10 Mk 11:15; Lk 19:45; Yn 2:13, 15Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”

21:11 Kum 18:15; Yn 1:21Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

Yesu Atakasa Hekalu

(Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)

21:12 Kum 14:26; Kut 30:13; Law 1:14Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 21:13 Isa 56:7; Yer 7:11Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.”

21:14 Mt 4:23Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. 21:15 Mt 9:27; Lk 19:39Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.

21:16 Za 8:2Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?”

Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma,

“ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao

umeamuru sifa’?”

21:17 Lk 24:50; Yn 11:18Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

Read More of Mathayo 21