Mathayo 20:20-34 NEN

Mathayo 20:20-34

Ombi La Mama Yake Yakobo Na Yohana

(Marko 10:35-45)

20:20 Mt 4:21; 8:2Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Yesu pamoja na wanawe, naye akapiga magoti mbele yake, akamwomba Yesu amfanyie jambo fulani.

20:21 Mt 19:28Yesu akamuuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”

20:22 Yer 49:12; Yn 18:11Yesu akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?”

Wakajibu, “Tunaweza.”

20:23 Mdo 12:2; Ufu 1:9Yesu akawaambia, “Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba yangu.”

20:24 Lk 22:24-25Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, waliwakasirikia hao ndugu wawili. Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 20:26 Mt 22:11; Mk 9:35Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 20:27 Mt 18:4; Mk 9:35naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: 20:28 Mt 8:20; Isa 42:1; Flp 2:8; Kut 30:2; Ebr 9:28kama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

Yesu Awaponya Vipofu Wawili

(Marko 10:46-52; Luka 18:35-43)

20:29 Mk 10:46; Lk 18:35Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu ulimfuata. 20:30 Mt 9:27; 15:22Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”

Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”

Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”

Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.

Read More of Mathayo 20