Mathayo 20:1-19 NEN

Mathayo 20:1-19

Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu

20:1 Mt 13:24; 21:28, 33“Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu. Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari20:2 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu.

“Mnamo saa tatu akatoka tena, akawakuta wengine wamesimama sokoni bila kazi. Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda.

“Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’

“Wakamjibu, ‘Ni kwa sababu hakuna yeyote aliyetuajiri.’

“Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu.’

20:8 Law 19:13; Kum 24:15“Ilipofika jioni, yule mwenye shamba la mizabibu akamwambia msimamizi, ‘Waite hao vibarua na uwalipe ujira wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’

“Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akapokea dinari moja. Hivyo wale walioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipokea dinari moja. 20:11 Yn 4:1Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, 20:12 Yn 4:8; Yak 1:11wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’

20:13 Mt 22:12; 26:50“Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja? Chukua ujira wako na uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu aliyeajiriwa mwisho kama nilivyokupa wewe. 20:15 Kum 15:9; Mk 7:22Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’

20:16 Mt 19:30“Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Yesu Atabiri Tena Kuhusu Kifo Chake

(Marko 10:32-34; Luka 18:31-34)

20:17 Mk 10:32; Lk 18:31; Yn 12:12Basi Yesu alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili na kuwaambia, 20:18 Lk 9:51; Mt 8:20; 16:21; 27:1-2“Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa viongozi wa makuhani na walimu wa sheria. Nao watamhukumu kifo 20:19 Mdo 2:23; Mt 16:21na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa ili wamdhihaki na kumpiga mijeledi na kumsulubisha msalabani. Naye atafufuliwa siku ya tatu!”

Read More of Mathayo 20