Mathayo 2:1-18 NEN

Mathayo 2:1-18

Wataalamu Wa Nyota Wafika Kumwona Mtoto Yesu

2:1 Lk 2:4, 6; Mwa 10:30; 25:6; 1Fal 4:30Baada ya Yesu kuzaliwa katika mji wa Bethlehemu huko Uyahudi, wakati wa utawala wa Mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu 2:2 Yer 23:5; Yn 1:49; Hes 24:17wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.”

Mfalme Herode aliposikia jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu. 2:4 2Nya 36:14; 34:13; Mal 2:7Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, akawauliza ni mahali gani ambapo Kristo2:4 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. angezaliwa. 2:5 Yn 7:42; Mik 5:2Nao wakamwambia, “Katika Bethlehemu ya Uyahudi, kwa maana hivyo ndivyo ilivyoandikwa na nabii:

2:6 Mik 5:2; 2Sam 5:2; Yn 7:42; Ufu 2:27“ ‘Nawe, Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,

wewe si mdogo miongoni

mwa watawala wa Yuda;

kwa maana kutoka kwako atakuja mtawala

atakayekuwa mchungaji

wa watu wangu Israeli.’ ”

Ndipo Herode akawaita wale wataalamu wa nyota kwa siri na kutaka kujua kutoka kwao uhakika kamili wa wakati ile nyota ilionekana. Kisha akawatuma waende Bethlehemu akiwaambia, “Nendeni mkamtafute kwa bidii huyo mtoto. Nanyi mara mtakapomwona, mniletee habari ili na mimi niweze kwenda kumwabudu.”

Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama mahali pale alipokuwa mtoto. Walipoiona ile nyota wakajawa na furaha kubwa mno. 2:11 Isa 60:3; Za 72:10Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Maria mama yake, wakamsujudu na kumwabudu yule mtoto Yesu. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane. 2:12 Ebr 11:7; Mt 2:13; 2:19; 2:22; 27:19Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasirudi kwa Herode, wakarudi kwenda katika nchi yao kwa njia nyingine.

Yosefu, Maria Na Mtoto Yesu Wakimbilia Misri

2:13 Mdo 5:19; Mt 27:19Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto akamwambia, “Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.”

Kisha Yosefu akaondoka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake wakati wa usiku, nao wakaenda Misri 2:15 Hes 11:1; Kut 4:22-23ambako walikaa mpaka Herode alipofariki. Hili lilifanyika ili litimie lile lililonenwa na Bwana kwa kinywa cha nabii kusema: “Nilimwita mwanangu kutoka Misri.”

Herode alipongʼamua kwamba wale wataalamu wa nyota wamemshinda kwa akili, alikasirika sana, naye akatoa amri ya kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kurudi chini katika mji wa Bethlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda alioambiwa na wale wataalamu wa nyota. 2:17 Yer 31:15; Mt 2:17, 23; 1:2Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia.

2:18 Mwa 35:19“Sauti ilisikika huko Rama,

maombolezo na kilio kikubwa,

Raheli akilia kwa ajili ya wanawe,

akikataa kufarijiwa,

kwa sababu hawako tena.”

Read More of Mathayo 2