Mathayo 16:21-28, Mathayo 17:1-13 NEN

Mathayo 16:21-28

Yesu Anatabiri Juu Ya Kifo Chake

(Marko 8:31–9:1; Luka 9:22-27)

16:21 Za 22:6; Yn 19:3; Hos 6:2; 1Kor 15:3-4; Lk 18:31-33; 9:22Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.

Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea akisema, “Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!”

16:23 Mt 4:10Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

16:24 Mt 10:38-39; Lk 14:27Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 16:25 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. 16:26 Za 49; Mt 4:8Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 16:27 Mt 8:20; 1Kor 1:7; Ufu 22:7; 2Nya 6:23; 2Kor 5:10Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 16:28 Mk 9:1; Lk 9:27; Mt 10:23Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake.”

Read More of Mathayo 16

Mathayo 17:1-13

Yesu Abadilika Sura Mlimani

(Marko 9:2-13; Luka 9:28-36)

17:1 Mk 9:2; Lk 9:28; Mt 4:21Siku sita baada ya jambo hili, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapeleka juu ya mlima mrefu peke yao. 17:2 2Pet 1:16-18Wakiwa huko, Yesu alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukangʼaa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho. Ghafula wakawatokea mbele yao Mose na Eliya, wakizungumza na Yesu.

Ndipo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.”

17:5 Mt 3:17; 2Pet 1:17; Mdo 3:22-23Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”

17:6 2Pet 1:18Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. 17:7 Mt 14:27Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine yeyote isipokuwa Yesu.

17:9 Mk 8:30; Mt 8:20; 16:21; Mk 8:30; Mt 8:20; 16:21Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”

17:10 Mt 11:14; Mal 4:5Wale wanafunzi wakamuuliza, “Kwa nini basi walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?”

17:11 Mal 4:5-6; Lk 1:16-17Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. 17:12 Mt 11:14; 14:3, 10; 16:21Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao.” 17:13 Lk 1:17Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yohana Mbatizaji.

Read More of Mathayo 17