Mathayo 16:1-20 NEN

Mathayo 16:1-20

Mafarisayo Wadai Ishara

(Marko 8:11-13; Luka 12:54-56)

16:1 Mdo 4:1; Mt 12:38Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu na kumjaribu kwa kumwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

16:2 Lk 12:54-56Yesu akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’ 16:3 Lk 12:54-56Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati. 16:4 Mt 12:39Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.

Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo

(Marko 8:14-21)

16:5 Mk 8:14Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. 16:6 Lk 12:1Yesu akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”

Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.”

16:8 Mt 6:30Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? 16:9 Mt 14:17-21Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 16:10 Mt 15:34-38Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 16:12 Yn 6:27; Mdo 4:1Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ni Mwana Wa Mungu

(Marko 8:27-30; Luka 9:18-21)

16:13 Mk 8:27; Lk 9:18Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?”

16:14 Mt 3:1; 14:2; Mk 6:15; Yn 1:21; Mt 14:2; Lk 9:7, 8, 9Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.”

Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

16:16 Yer 10:10; Yn 11:27Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo,16:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu aliye hai.”

16:17 Gal 1:16; Efe 6:12Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona,16:17 Bar-Yona ni neno la Kiaramu, maana yake ni Mwana wa Yona. kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. 16:18 Yn 1:42; Efe 2:20Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. 16:19 Isa 22:22; Ufu 3:7; Mt 18:18; Yn 20:23Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.” 16:20 Mt 8:30 Kisha akawakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.

Read More of Mathayo 16