Mathayo 14:1-21 NEN

Mathayo 14:1-21

Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa

(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9)

14:1 Lk 13:31; 9:7-9; Mdo 12:1Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Yesu, 14:2 Mt 3:1akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

14:3 Mt 4:12; 11:2; Lk 3:19-20Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 14:4 Law 18:16; 20:21kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 14:5 Mt 11:19; 21:26; Lk 20:26Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 14:10 Mt 17:12Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. 14:12 Mt 8:2Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.

Yesu Alisha Wanaume 5,000

(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)

14:13 Mk 6:31-44; Mt 10:23; Mk 6:32; Lk 9:19; Yn 6:13Yesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 14:14 Mt 9:36; 4:23Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

14:15 Mk 6:35; Lk 9:12; Yn 6:5Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”

14:17 Mt 16:9; 1Sam 9:13; 1Kor 10:16Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 14:19 Mt 15:36; 1Sam 9:13; Mt 26:26; Mk 8:6; Lk 9:16; 24:30; Mdo 2:42; 20:7Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 14:20 2Fal 4:44Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Read More of Mathayo 14