Mathayo 13:18-35 NEN

Mathayo 13:18-35

Maelezo Ya Mfano Wa Mbegu

(Marko 4:13-20; Luka 8:11-15)

13:18 Mk 4:14; Lk 8:11“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: 13:19 Mt 4:23; 5:37Mtu yeyote anaposikia neno la Ufalme naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. Hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. 13:20 Isa 58:2; Eze 33:31, 32; Yn 5:35Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha. 13:21 Mt 11:6; 26:31Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, yeye mara huchukizwa. 13:22 Mt 19:23; 1Tim 6:9-10, 17Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. 13:23 Mt 13:8Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”

Mfano Wa Magugu

13:24 Mt 25:1; Mk 4:26-39Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.

“Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’

“Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’

“Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayangʼoe?’

“Lakini akasema, ‘Hapana, msiyangʼoe, kwa maana wakati mkingʼoa magugu mnaweza mkangʼoa na ngano pamoja nayo. 13:30 Mt 3:12Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

Mfano Wa Mbegu Ya Haradali

(Marko 4:30-32; Luka 13:18-19)

13:31 Mt 17:20; Lk 17:6Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake. 13:32 Za 104:12; Dan 4:12Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

(Luka 13:20-21)

13:33 Mt 13:24; Mwa 18:6; Gal 5:9Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

Sababu Ya Yesu Kutumia Mifano

(Marko 4:33-34)

13:34 Mk 4:33-34Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano. 13:35 Za 78:2; 1Kor 2:7Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema:

“Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano;

nitahubiri mambo yaliyofichika

tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

Read More of Mathayo 13