Mathayo 12:46-50, Mathayo 13:1-17 NEN

Mathayo 12:46-50

Mama Na Ndugu Zake Yesu

(Marko 3:31-35; Luka 8:19-21)

12:46 Lk 11:24; Ay 1:7; 1Pet 5:8Wakati alikuwa angali anazungumza na makutano, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. Ndipo mtu mmoja akamwambia, “Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe.”

12:48 Lk 2:49Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, “Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?” Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 12:50 Mt 6:10; Yn 15:14Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”

Read More of Mathayo 12

Mathayo 13:1-17

Mfano Wa Mpanzi

(Marko 4:1-9; Luka 8:4-8)

13:1 Mt 13:36; 9:28Siku iyo hiyo Yesu akatoka nje ya nyumba, akaketi kando ya bahari. 13:2 Lk 5:3Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari. 13:3 Lk 8:5Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema: “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea. 13:8 Mwa 26:12Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini, na nyingine mara thelathini. 13:9 Mt 11:15Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

Sababu Ya Kufundisha Kwa Mifano

(Marko 4:10-12; Luka 8:9-10)

Wanafunzi wake wakamwendea, wakamuuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?”

13:11 Kol 1:27; 1Yn 2:20, 27Akawajibu, “Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao hawajapewa. 13:12 Mt 25:29; Lk 19:26Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa. 13:13 Yer 5:21; Eze 12:2Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano:

“Ingawa wanatazama, hawaoni;

wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi.

13:14 Mt 1:22; 13:35; Eze 12:2; Isa 6:9; Mdo 28:26-28Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:

“ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

na pia mtatazama lakini hamtaona.

13:15 Isa 6:9-10; Rum 11:8Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

hawasikii kwa masikio yao,

na wamefumba macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

na kugeuka nami nikawaponya.’

13:16 Mt 16:17; Lk 10:23-24Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. 13:17 Ebr 11:13; 1Pet 1:10-12Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia.

Read More of Mathayo 13