Mathayo 12:1-21 NEN

Mathayo 12:1-21

Bwana Wa Sabato

(Marko 2:23-28; Luka 6:1-5)

12:1 Kum 23:25Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, nao wakaanza kuvunja masuke ya nafaka na kuyala. 12:2 Kut 20:10; Yn 9:6Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.”

12:3 1Sam 21:1-6Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? 12:4 Law 24:5-9Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao. 12:5 Hes 28:9-10; Yn 7:22-23Au hamjasoma katika Sheria kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja sheria ya Sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? 12:6 Mt 12:41-42Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. 12:7 Hos 6:6; Mt 9:13Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia, 12:8 Mt 8:20kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono

(Marko 3:1-6; Luka 6:6-11)

12:9 Mk 3:1; Lk 6:6Yesu akaondoka mahali hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao, 12:10 Lk 14:3; Yn 9:6na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, wakamuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?”

12:11 Lk 15:5Yesu akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa? 12:12 Mt 6:26; 10:31Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”

Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine. 12:14 Mwa 37:18; Yn 11:53Lakini Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri baya juu ya Yesu jinsi watakavyoweza kumuua.

Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu

12:15 Mt 4:23Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote, 12:16 Mt 8:4akiwakataza wasiseme yeye ni nani. 12:17 Isa 42:1-4; 41:9Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

12:18 Mt 3:7; Isa 42:1-4; 41:9“Tazama mtumishi wangu niliyemchagua,

mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Nitaweka Roho wangu juu yake,

naye atatangaza haki kwa mataifa.

Hatagombana wala hatapiga kelele,

wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

Mwanzi uliopondeka hatauvunja,

na utambi unaofuka moshi hatauzima,

mpaka atakapoifanya haki ishinde.

12:21 Isa 42:1-4Katika Jina lake mataifa

wataweka tumaini lao.”

Read More of Mathayo 12