Mathayo 10:32-42, Mathayo 11:1-15 NEN

Mathayo 10:32-42

10:32 Rum 10:9“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 10:33 Mk 8:38; 2Tim 2:12Lakini yeyote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

Sikuleta Amani, Bali Upanga

(Luka 12:51-53; 14:26-27)

10:34 Lk 12:51-53“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. 10:35 Mik 7:6Kwa maana nimekuja kumfitini

“ ‘mtu na babaye,

binti na mamaye,

mkwe na mama mkwe wake;

10:36 Mik 6:7nao adui za mtu watakuwa

ni wale watu wa nyumbani kwake.’

10:37 Lk 14:26“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. 10:38 Mt 16:24-25; Lk 14:27Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 10:39 Lk 17:33; Yn 12:44Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.

Watakaopokea Thawabu

(Marko 9:41)

10:40 Kut 16:8; Gal 4:14; Lk 10:16; Yn 12:44“Mtu yeyote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi, na yeyote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma. 10:41 1Fal 17:10; 18:4; 2Fal 4:8Mtu yeyote anayempokea nabii kwa kuwa ni nabii atapokea thawabu ya nabii, naye mtu anayempokea mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki atapokea thawabu ya mwenye haki. 10:42 Mt 25:40; Mdo 10:4; Mit 14:30; Mk 9:41Kama yeyote akimpa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, nawaambia, hataikosa thawabu yake.”

Read More of Mathayo 10

Mathayo 11:1-15

Yesu Na Yohana Mbatizaji

(Luka 7:18-35)

11:1 Mt 7:28; 26:1Baada ya Yesu kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

11:2 Mt 14:3Yohana aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Kristo11:2 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake 11:3 Za 118:26; Ebr 10:37ili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mnayosikia na kuyaona: 11:5 Lk 4:18-19; Isa 61:1-2Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 11:6 Mt 13:21; 26:31Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

11:7 Mt 3:1-5Wale wanafunzi wa Yohana walipokuwa wanaondoka, Yesu akaanza kusema na makutano kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme. 11:9 Lk 1:76; 7:26Basi mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 11:10 Mal 3:1; Lk 7:27Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:

“ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,

atakayetengeneza njia mbele yako.’

11:11 Mt 13:17Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yohana. 11:12 Lk 16:16; 13:24Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. 11:13 Lk 16:16Kwa maana manabii wote na Sheria walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 11:14 Mal 4:5; Yn 1:21Ikiwa mko tayari kukubali hilo, yeye ndiye yule Eliya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. 11:15 Lk 14:35; Ufu 2:7Yeye aliye na masikio, na asikie.

Read More of Mathayo 11