Marko 8:14-38, Marko 9:1 NEN

Marko 8:14-38

Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode

(Mathayo 16:5-12)

8:14 Mt 16:5Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 8:15 1Kor 5:6-8; Lk 12:1; Mt 14:1; Mk 12:13Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”

8:16 Mt 16:7Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.”

8:17 Isa 6:9-10; Mk 6:52Yesu, akifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamtambui wala hamwelewi? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 8:18 Yer 5:21; Eze 12:2Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? 8:19 Lk 9:17; Yn 6:13Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?”

Wakamjibu, “Kumi na viwili.”

8:20 Mk 8:6-9; Mt 15:37“Je, nilipoimega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?”

Wakamjibu, “Saba.”

8:21 Mk 6:52Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?”

Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida

8:22 Mt 11:21; Mk 10:46; Yn 9:1Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Yesu amguse. 8:23 Mk 7:33; 5:23Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, “Unaona chochote?”

Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.”

Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 8:26 Mt 8:14; Mk 5:43Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.”

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-20; Luka 9:18-21)

8:27 Mt 16:13; Lk 9:18Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

8:28 Mt 3:1; Mal 4:5Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”

8:29 Yn 6:69; 11:27Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.”8:29 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

8:30 Mt 17:9; Lk 9:21Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.

Yesu Atabiri Kifo Chake

(Mathayo 16:21-28; Luka 9:22-27)

8:31 Mt 8:20; 16:21; 27:1-2; Mdo 2:23Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuke. 8:32 Yn 18:20Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea.

8:33 Mt 4:10Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

8:34 Mt 10:38; Lk 14:27Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 8:35 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 8:38 Mt 8:20; 10:33; Lk 12:9; 1The 2:19Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”

Read More of Marko 8

Marko 9:1

9:1 Mk 13:30; Lk 22:18; Mt 24:30; 25:30Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”

Read More of Marko 9