Marko 6:30-56 NEN

Marko 6:30-56

Yesu Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)

6:30 Lk 24:10; Mdo 1:2, 26; Lk 9:10Wale mitume wakakusanyika kwa Yesu na kumpa taarifa ya mambo yote waliyokuwa wamefanya na kufundisha. 6:31 Mk 3:20Basi kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakawa hawana nafasi ya kula, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.”

6:32 Mk 6:45; 4:36Hivyo wakaondoka kwa mashua peke yao, wakaenda mahali pasipo na watu. Lakini watu wengi waliowaona wakiondoka, wakawatambua, nao wakaenda haraka kwa miguu kutoka miji yote, nao wakatangulia kufika. 6:34 Mt 9:36Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.

6:35 Mk 8:1-9; Mt 14:15; Lk 9:11Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimekwenda sana. Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.”

6:37 2Fal 4:42-44Lakini Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari 2006:37 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja; hivyo dinari 200 ni sawa na mshahara wa siku 200. ili tuwape watu hawa wale?”

6:38 Mt 15:34; Mk 8:5Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.”

Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”

Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini. 6:41 Mt 14:19Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. Watu wote wakala, wakashiba. 6:43 Kum 28:5Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. Idadi ya wanaume waliokula walikuwa 5,000.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Yohana 6:15-21)

6:45 Mt 11:21Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 6:46 Lk 3:21Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.

6:47 Mt 14:23; Yn 6:16, 17Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 6:48 Lk 24:28Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 6:49 Lk 24:27lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 6:50 Lk 14:27kwa sababu wote walipomwona waliogopa.

Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” 6:51 Mk 6:32; 4:39Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, 6:52 Mk 8:17-21kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.

6:53 Yn 6:24-25Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Yesu. Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Yesu yupo. 6:56 Mt 9:20; Mk 5:27, 28; Mdo 19:12Kila mahali Yesu alipokwenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa.

Read More of Marko 6