Marko 2:18-27, Marko 3:1-30 NEN

Marko 2:18-27

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Mathayo 9:14-17; Luka 5:33-39)

2:18 Mt 6:16-18; Mdo 1; Mt 9Basi wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Yesu na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?”

Yesu akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati angali pamoja nao? Wakati bwana arusi bado yuko pamoja nao, hawawezi kufunga. 2:20 Lk 17:22Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Siku hiyo ndipo watakapofunga.

“Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kitachanika kutoka ile nguo iliyochakaa, nayo itachanika zaidi. 2:22 Lk 5:33-38Wala hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo hiyo divai itamwagika na viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”

Bwana Wa Sabato

(Mathayo 12:1-8; Luka 6:1-5)

2:23 Kum 23:25; Mt 12:1; Lk 6:1Siku moja ya Sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke. 2:24 Mt 12:2Mafarisayo wakamwambia, “Tazama, mbona wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato?”

Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa, wakahitaji chakula? 2:26 1Nya 24:6; 2Sam 8:17; Law 24:5-9; 1Sam 21:1-6Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.”

2:27 Kut 23:12; Kum 5:14; Kol 2:16Kisha Yesu akawaambia, “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato.

Read More of Marko 2

Marko 3:1-30

Mtu Aliyepooza Mkono Aponywa

(Mathayo 12:9-14; Luka 6:6-11)

3:1 Mt 4:23; Mk 1:21Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi, na huko palikuwa na mtu aliyepooza mkono. 3:2 Mt 12:10; Lk 14:1Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”

Kisha Yesu akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza kimya.

3:5 Yn 11:33Yesu akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa! 3:6 Mt 22:16; Mk 12:13; Mt 12:14Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya shauri la kumuua Yesu wakiwa na Maherode.

Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

3:7 Mt 4:25Yesu pamoja na wanafunzi wake wakaondoka huko wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya ukamfuata. 3:8 Mt 11:21Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, na ngʼambo ya Yordani, pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni. Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga. 3:10 Mt 4:23; 9:20Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa. 3:11 Mt 4:3; Mk 1:23, 24Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.” 3:12 Mt 8:4; Mdo 16:17, 18Lakini aliwaonya wasimseme yeye ni nani.

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Luka 6:12-16)

3:13 Mt 5:11Yesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. 3:14 Mk 6:30Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri 3:15 Mt 10:1na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. 3:16 Yn 1:42Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); 3:17 Lk 2Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

Yesu Na Beelzebuli

(Mathayo 12:22-32; Luka 11:14-23; 12:10)

3:20 Mk 6:31Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. 3:21 Yn 10:20; Mdo 26:24Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

3:22 Mt 15:1; 12:24; Yn 10:20; Mt 9:34Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!3:22 Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu. Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”

3:23 Mk 4:2; Mt 4:10Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia. 3:27 Isa 49:24-25Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali zake. 3:28 Mt 12:31; Lk 12:10; 1Yn 5:16Amin, nawaambia, dhambi zote na makufuru yote ya wanadamu watasamehewa. 3:29 Mt 12:31-32; Lk 12:10Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.”

3:30 Mk 3:22Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”

Read More of Marko 3