Marko 15:33-47 NEN

Marko 15:33-47

Kifo Cha Yesu Msalabani

(Mathayo 27:45-56; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30)

15:33 Amo 8:9Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 15:34 Za 21:1; Mt 27:46Mnamo saa tisa, Yesu akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”)

Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Eliya.”

15:36 Mk 15:23; Za 69:21Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”

15:37 Yn 19:30Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.

15:38 Ebr 10:19-20Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini. 15:39 Mt 4:3; Mk 9:7Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

15:40 Za 38:11; Lk 24:10; Yn 19:25Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. 15:41 Mt 27:55-56; Lk 8:2-3Hawa walifuatana na Yesu na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwepo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye Yerusalemu.

Maziko Ya Yesu

(Mathayo 27:57-61; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)

15:42 Mt 27:62; Yn 19:31Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizi, yaani siku moja kabla ya Sabato, 15:43 Mt 5:22; 3:2; Lk 2:25, 38Yosefu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Yesu. Pilato alikuwa akijiuliza kama Yesu alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Yesu alikuwa amekwisha kufa. 15:45 Mk 15:39Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yosefu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. 15:46 Mk 16:3Hivyo Yosefu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi. Maria Magdalene na Maria mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa.

Read More of Marko 15