Marko 14:17-42 NEN

Marko 14:17-42

14:17 Mt 26:20Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 14:18 Za 41:10Walipoketi mezani wakila, Yesu akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

14:20 Yn 13:18-27Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. 14:21 Mt 8:20Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.”

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

14:22 Mt 14:22Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

14:23 1Kor 10:16Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

14:24 Mt 26:28Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 14:25 Mt 3:2Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

14:26 Mt 21:1Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

14:27 Zek 13:7Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:

“ ‘Nitampiga mchungaji,

nao kondoo watatawanyika.’

14:28 Mk 16:7Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

14:29 Mt 26:33-34; Lk 22:33, 34; Yn 13:37, 38Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

14:30 Lk 22:34; Yn 13:38Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

14:31 Lk 22:33; Yn 13:37Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Yesu Aomba Katika Bustani Ya Gethsemane

(Mathayo 26:36-46; Luka 22:39-46)

14:32 Mt 26:36; Lk 22:29; Yn 13:37Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.” Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. 14:34 Yn 12:27Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.”

14:35 Mk 14:41; Mt 26:18Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. 14:36 Rum 8:15; Gal 4:6; Mt 20:22; 26:39Akasema, “Abba,14:36 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; ni mtoto wa kuzaa tu angeweza kulitumia kwa baba yake. Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.”

Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 14:38 Mt 6:13; Rum 7:22-23Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia.

14:41 Mt 26:18Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. 14:42 Mt 26:46; Yn 18:1, 2Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”

Read More of Marko 14