Marko 10:13-31 NEN

Marko 10:13-31

Yesu Anawabariki Watoto Wadogo

(Mathayo 19:13-15; Luka 18:15-17)

10:13 Mt 19:13; Lk 18:15Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. 10:14 Mt 25:34Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 10:15 Mt 18:3Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 10:16 Mk 9:36Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Kijana Tajiri

(Mathayo 19:16-30; Luka 18:18-30)

10:17 Mk 1:40; Lk 10:25; Mdo 20:32Yesu alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. 10:19 Kut 20:12-16; Kum 5:16-20Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

Akamjibu, “Mwalimu, amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”

10:21 Mdo 2:45; Mt 6:20; Lk 12:33; Mt 4:19Yesu akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana. Akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

10:23 Za 62:10; 1Tim 6:9-17Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika Ufalme wa Mungu!”

10:24 Mt 7:13-14; Yn 3:5Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu. 10:25 Lk 12:16-20; 16:19-31Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri10:25 Tajiri ina maana wale wanaotumainia mali. kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

10:27 Mt 19:26Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”

10:28 Mt 4:18-19; Lk 18:28Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!”

Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, 10:30 Mt 6:33; 12:32; 25:46ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 10:31 Mt 19:30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

Read More of Marko 10