Marko 1:1-28 NEN

Marko 1:1-28

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28)

1:1 Mt 4:3Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

1:2 Mal 3:1; Lk 7:27Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,

atakayetengeneza njia mbele yako”:

1:3 Isa 40:3; Yn 1:23“sauti ya mtu aliaye nyikani.

‘Itengenezeni njia ya Bwana,

yanyoosheni mapito yake.’ ”

1:4 Yn 1:26, 33; Mt 3:1; Mdo 11:16; Lk 1:7Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 1:5 Mt 3:5Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 1:6 Law 11:22; Mt 3:4Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 1:7 Mdo 13:25; Yn 1:27; Mdo 13:25Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 1:8 Yoe 2:28; Yn 1:33Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”

Ubatizo Wa Yesu

(Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-22)

1:9 Mt 2:23; Lk 3:21Wakati huo Yesu akaja kutoka Nazareti ya Galilaya, naye akabatizwa na Yohana katika Mto Yordani. 1:10 Yn 1:32Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. 1:11 Mt 3:17; Mk 9:7; Za 2:7; Isa 42:1Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Majaribu Ya Yesu

(Mathayo 4:1-11; Luka 4:1-13)

1:12 Mt 4:1; Lk 4:1Wakati huo huo, Roho akamwongoza Yesu kwenda nyikani, 1:13 Mt 4:10; Ebr 4:15naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

1:14 Mt 4:12; 4:23; 4:12; 4:23; Lk 4:14, 15Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, 1:15 Rum 5:6; Gal 4:4; Mdo 20:21akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wanne

(Mathayo 4:12-22; Luka 4:14-15; 5:1-11)

1:16 Mt 4:18; Lk 5:4Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 1:17 Mt 13:47Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 1:18 Mt 19:27; Lk 5:11; Mt 4:19Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

1:19 Mt 4:21Alipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Yesu.

Yesu Amtoa Pepo Mchafu

(Luka 4:31-37)

1:21 Mk 1:39; Mt 4:23Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya Sabato, mara Yesu akaingia sinagogi, akaanza kufundisha. 1:22 Mt 7:28-29Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria. 1:23 Lk 4:33Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, 1:24 Mt 8:29; Yn 1:45-46; Mdo 4:10; Za 16:10; 1Yn 2:20naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

1:25 Mk 1:34Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 1:26 Mk 9:20Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.

1:27 Mk 10:24, 32Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” 1:28 Mk 9:26Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya.

Read More of Marko 1