Malaki 1:1-14, Malaki 2:1-16 NEN

Malaki 1:1-14

1:1 Nah 1:1; Mdo 7:38; Rum 3:1-2; 1Pet 4:11Ujumbe: Neno la Bwana kwa Israeli kupitia kwa Malaki.

Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa

1:2 Kum 4:37; Mal 2:14-17; 3:7-13; Yer 46:27; Rum 9:13; Mwa 25:23; 28:13Bwana asema, “Nimewapenda ninyi.”

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ”

Bwana asema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo, 1:3 Lk 14:26; Eze 35:3; Isa 34:10; 13:22lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.”

1:4 Isa 11:14; 34:11; 9:10; 34:5; Mao 4:22; Eze 25:12-14; 26; 14Edomu anaweza kusema, “Ingawa tumepondapondwa, tutajenga upya magofu.”

Lakini hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Wanaweza kujenga, lakini nitabomoa. Wataitwa Nchi Ovu, watu ambao siku zote wapo chini ya ghadhabu ya Bwana. 1:5 Za 35:17; 48:1; Mik 5:4; Isa 45:22; 52:10; Amo 1:11-12; Za 83:18Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Bwana ni mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Dhabihu Zilizo Na Mawaa

1:6 Law 20:9; Mt 15:14; 23:9; Lk 6:46; Ay 5:17; Kum 31; 12; 20:12; 5:16; Efe 6:2; Lk 18:20“Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Ni ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.

“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’

1:7 Law 21:6; Eze 23; 41; 41:22“Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu.

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’

“Kwa kusema kuwa meza ya Bwana ni ya kudharauliwa. 1:8 Law 1:3; Kum 15:21; Mwa 32:20; Isa 43:23; Ay 42:8Wakati mletapo dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

1:9 Law 23:33-44; Za 51:17; Mik 6:6-8; Rum 12; 1; Ebr 13:16; Yer 6:20; Hos 13:9“Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

1:10 2Nya 28:24; Hos 5:6; Mal 2:12; Law 22; 20; Isa 1:11-14; Yer 14:12; 1Kor 9:13; Flp 3:18-19“Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu. 1:11 Isa 24:15; 56:6; 6:3; 12:4; 60:6-7; 19:21; Za 113:3; Mt 8:11; Ufu 5:8; Ebr 13:15; Isa 59:19; 66:19; Yn 4:21; 1Tim 2:8Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia mawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

1:12 Eze 41:22“Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’ 1:13 Isa 43:22-24; Hes 14:11; Kum 15:21; Law 22:20; Isa 1:12Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asema Bwana. 1:14 Kut 12:5; Za 95:3; 72:6-11; Oba 1:21; Law 22:18-21; Mdo 5:1“Amelaaniwa yeye adanganyaye, aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwa Bwana. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Read More of Malaki 1

Malaki 2:1-16

Onyo Kwa Makuhani

“Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, enyi makuhani. 2:2 Kum 28:15Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” Asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu. Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 2:5 Hes 25:12; Kum 33:8“Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu. 2:6 Dan 12:3; Lk 1:16-17; Yak 5:20Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.

2:7 Kum 17:9; Isa 42:19; Hag 1:13; Gal 4:14“Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe wa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 2:8 1Sam 2:17Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.”

Yuda Si Mwaminifu

2:10 Isa 51:2; Mt 3:9; 1Kor 8:6; Ebr 12:9; Za 100:3Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake?

2:11 Neh 13:23Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapo Bwana, kwa kuoa binti wa mungu mgeni. Kwa maana kwa mtu yeyote atendaye jambo hili, Bwana na amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamletea Bwana Mwenye Nguvu Zote sadaka.

2:13 Yer 11:11; 14:12; Za 39:12; 66:18; Isa 58:2Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. 2:14 Mwa 21:30; 24:22; Mit 5:18; Ebr 13:4Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu Bwana ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.

2:15 Mwa 2:24; Mt 19:4-6; Kum 14:2; 4:15; 1Kor 7:14; 7:10; Isa 54:6; Ebr 13:4Je, Bwana hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.

2:16 Kum 24:1; Mt 5:31-32; 19:4-9; Isa 58:4; Mk 10:4-5; Mwa 6:11; 34:25; Mit 4:17; Za 51:10“Ninachukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Read More of Malaki 2