Luka 9:10-27 NEN

Luka 9:10-27

Yesu Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14)

9:10 Mk 6:30; Mt 11:21Mitume wake waliporudi, wakamweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji uitwao Bethsaida. 9:11 Lk 9:2Lakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.

9:12 Mt 14:15; Mk 6:35; Yn 6:1, 5Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Yesu na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.” Walikuwako wanaume wapatao 5,000.

Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.” Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. 9:16 Mt 14:19Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29)

9:18 Lk 3:21Wakati mmoja, Yesu alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

9:19 Mt 14:2; Lk 9:7; 8Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

9:20 Yn 1:49; 11:27Kisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo9:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. wa Mungu.”

9:21 Mt 16:20; Mk 8:30Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo. 9:22 Mt 8:20; 16:21; 27:1-2; Mdo 2:23; 3:13Yesu akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”

9:23 Mt 10:38; Lk 14:27Kisha akawaambia wote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate. 9:24 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. 9:25 Mt 16:26; Mk 8:36Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au kuangamiza nafsi yake? 9:26 2Tim 2:12; Mt 16; 27; 10:33Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba, pamoja na malaika watakatifu. 9:27 Mt 16:28; Mk 9:1Amin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu.”

Read More of Luka 9