Luka 6:12-36 NEN

Luka 6:12-36

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Marko 3:13-19)

6:12 Lk 3:21Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 6:13 Mk 6:30Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume: 6:14 Yn 1:42Simoni aliyemwita Petro, Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, 6:15 Mt 9:9Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote, Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote ambaye alikuwa msaliti.

Yesu Aponya Wengi

(Mathayo 4:23-25)

6:17 Mt 11:21; Mk 3:7-8; Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 6:18 Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. 6:19 Mt 9:20; 14:36; Mk 5:30; Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Watu wote walikuwa wanajitahidi kumgusa kwa sababu nguvu zilikuwa zikimtoka na kuwaponya wote.

Baraka Na Ole

(Mathayo 5:1-12)

6:20 Mt 25:34Akawatazama wanafunzi wake, akasema:

“Mmebarikiwa ninyi mlio maskini,

kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

6:21 Isa 55:1; 61:2-3; Ufu 7:17Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa,

kwa sababu mtashibishwa.

Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa,

kwa sababu mtacheka.

6:22 Yn 9:22; 16:2; 15:21; Isa 51:7; Yn 15:19; 16:2Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia,

watakapowatenga na kuwatukana

na kulikataa jina lenu kama neno ovu,

kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

6:23 Mt 5:21; 5:12; Mdo 5:41; Kol 1:24; Yak 1:2; Mdo 7:51“Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.

6:24 Yak 5:1; Lk 16:25; Amo 6:1; Yak 5:1; Lk 12:21; Mt 6:2, 5, 16; Lk 16:25“Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri,

kwa sababu mmekwisha kupokea faraja yenu.

6:25 Isa 65:13; Mit 14:13; Isa 65:13; Mit 14; 13Ole wenu ninyi mlioshiba sasa,

maana mtaona njaa.

Ole wenu ninyi mnaocheka sasa,

maana mtaomboleza na kulia.

6:26 Mt 7:15; Yn 15:19; 1Yn 4:5Ole wenu watu watakapowasifu,

kwani ndivyo baba zao walivyowasifu

manabii wa uongo.

Wapendeni Adui Zenu

(Mathayo 5:38-48)

6:27 Mt 5:44; Rum 12:20; Kut 23:4; Mt 5:44; Lk 6:35; Rum 12:20“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 6:28 Lk 23:34; Mdo 7:60Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. 6:29 Mt 5:39; 1Kor 6:7Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. 6:30 Kum 15:7-10; Mt 21:36Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. 6:31 Mt 7:12Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.

6:32 Mt 5:42-46“Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwapenda wale wawapendao. Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ hufanya vivyo hivyo. 6:34 Mt 5:42Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwakopesha ‘wenye dhambi’ wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote. 6:35 Rum 8:14; Mk 5:7Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu. 6:36 Yak 2:13; 1Pet 1:17; 1Yn 3:1Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Read More of Luka 6