Luka 5:33-39, Luka 6:1-11 NEN

Luka 5:33-39

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22)

5:33 Lk 7:18; Yn 1:35; 3:25-26; Mt 14:17; Mk 2:18-22Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”

5:34 Yn 3:29; Mt 14:17; Mk 2:18-22Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao? 5:35 Lk 9:22; 7:22; Mt 14:17; Mk 2:18-22Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.”

5:36 Mt 14:17; Mk 2:18-22; Mt 9:16, 17; Mk 2:21, 22Yesu akawapa mfano huu, akawaambia: “Hakuna mtu achanaye kiraka kutoka kwenye nguo mpya na kukishonea kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, atakuwa amechana nguo mpya, na kile kiraka hakitalingana na ile nguo iliyochakaa. 5:37 Mt 14:17; Mk 2:18-22Hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo yote itamwagika. 5:38 Mt 14:17; Mk 2:18-22Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 5:39 Mt 14:17; Mk 2:18-22Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ”

Read More of Luka 5

Luka 6:1-11

Bwana Wa Sabato

(Mathayo 12:1-8; Marko 2:23-28)

6:1 Kum 23:25Ikawa siku moja ya Sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake. 6:2 Mt 12:2Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya mambo yasiyo halali kufanywa siku ya Sabato?”

6:3 1Sam 21:6Yesu akawajibu, “Je, ninyi hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa? 6:4 Law 24:5-9Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.” 6:5 Mt 8:20Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

Mtu Aliyepooza Mkono Aponywa

(Mathayo 12:9-14; Marko 3:1-6)

6:6 Lk 6:1; Mt 12:9; Mk 3:1; Lk 13:14; 14:3; Yn 9:16Ikawa siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. 6:7 Mt 9:4Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. 6:8 Mt 9:4Lakini Yesu alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.

Ndipo Yesu akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?”

6:10 Mt 13:47Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukaponywa kabisa. 6:11 Yn 5:18Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Yesu.

Read More of Luka 6