Luka 4:14-37 NEN

Luka 4:14-37

Mwanzo Wa Huduma Ya Galilaya

(Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15)

4:14 Mt 4:12; 9:26Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. 4:15 Mt 4:23Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.

Yesu Akataliwa Nazareti

(Mathayo 13:53-58; Marko 6:1-6)

4:16 Mt 2:23; 13:54Yesu akaenda Nazareti, alipolelewa, na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, 4:17 Isa 61:1, 2; 58:6naye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa:

4:18 Yn 3:34“Roho wa Bwana yu juu yangu,

kwa sababu amenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao,

na vipofu kupata kuona tena,

kuwaweka huru wanaoonewa,

na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”

4:20 Mt 26:55Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 4:21 Mt 1:22Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.”

4:22 Yn 6:42; 7:15Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

4:23 Mt 2:23; Mk 1:21-28; 2:1-12Yesu akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”

4:24 Mt 13:57; Yn 4:44Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. 4:25 1Fal 18:1; Ufu 11:6Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima. 4:26 1Fal 17:8-16; Mt 11:21Hata hivyo Eliya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 4:27 2Fal 5:1-14Pia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu.”4:27 Shamu hapa inamaanisha Syria.

Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. 4:29 Hes 15:35; Ebr 13:12Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali. 4:30 Yn 8:59; 10:39Lakini yeye akapita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.

Yesu Atoa Pepo Mchafu

(Marko 1:21-28)

4:31 Mt 4:13Kisha Yesu akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilaya, na katika siku ya Sabato akawa anafundisha. 4:32 Mt 7:28-29Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.

4:33 Mk 1:23Ndani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Naye akapiga kelele kwa nguvu akisema, 4:34 Mt 8:28-29; Mk 1:24; Yak 2:19“Tuache! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

4:35 Mt 8:26; Lk 8:24Basi Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akisema, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” Yule pepo mchafu akamwangusha yule mtu chini mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru. 4:36 Mt 7:28-29; 10:1Watu wote wakashangaa, wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!” 4:37 Mt 9:26Habari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile.

Read More of Luka 4