Luka 3:23-38, Luka 4:1-13 NEN

Luka 3:23-38

Ukoo Wa Bwana Yesu

(Mathayo 1:1-17)

3:23 Mt 4:17; Lk 1:27Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu,

Yosefu alikuwa mwana wa Eli,

Eli alikuwa mwana wa Mathati,

Mathati alikuwa mwana wa Lawi,

Lawi alikuwa mwana wa Melki,

Melki alikuwa mwana wa Yanai,

Yanai alikuwa mwana wa Yosefu,

Yosefu alikuwa mwana wa Matathia,

Matathia alikuwa mwana wa Amosi,

Amosi alikuwa mwana wa Nahumu,

Nahumu alikuwa mwana wa Esli,

Esli alikuwa mwana wa Nagai,

Nagai alikuwa mwana wa Maathi,

Maathi alikuwa mwana wa Matathia,

Matathia alikuwa mwana wa Semeini,

Semeini alikuwa mwana wa Yoseki,

Yoseki alikuwa mwana wa Yoda,

3:27 Mt 1:12; 1Nya 3:17Yoda alikuwa mwana wa Yoanani,

Yoanani alikuwa mwana wa Resa,

Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli,

Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli,

Shealtieli alikuwa mwana wa Neri,

Neri alikuwa mwana wa Melki,

Melki alikuwa mwana wa Adi,

Adi alikuwa mwana wa Kosamu,

Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu,

Elmadamu alikuwa mwana wa Eri,

Eri alikuwa mwana wa Yoshua,

Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri,

Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu,

Yorimu alikuwa mwana wa Mathati,

Mathati alikuwa mwana wa Lawi,

Lawi alikuwa mwana wa Simeoni,

Simeoni alikuwa mwana wa Yuda,

Yuda alikuwa mwana wa Yosefu,

Yosefu alikuwa mwana wa Yonamu,

Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu,

Eliakimu alikuwa mwana wa Melea,

3:31 2Sam 5:14; 1Nya 3:5Melea alikuwa mwana wa Mena,

Mena alikuwa mwana wa Matatha,

Matatha alikuwa mwana wa Nathani,

Nathani alikuwa mwana wa Daudi,

3:32 Rut 4:22; 1Nya 2:10Daudi alikuwa mwana wa Yese,

Yese alikuwa mwana wa Obedi,

Obedi alikuwa mwana wa Boazi,

Boazi alikuwa mwana wa Salmoni,

Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni,

3:33 Rut 4:18-22; 1Nya 2:10Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu,

Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu,

Aramu alikuwa mwana wa Hesroni,

Hesroni alikuwa mwana wa Peresi,

Peresi alikuwa mwana wa Yuda,

3:34 Mwa 11:24-26Yuda alikuwa mwana wa Yakobo,

Yakobo alikuwa mwana wa Isaki,

Isaki alikuwa mwana wa Abrahamu,

Abrahamu alikuwa mwana wa Tera,

Tera alikuwa mwana wa Nahori,

Nahori alikuwa mwana wa Serugi,

Serugi alikuwa mwana wa Reu,

Reu alikuwa mwana wa Pelegi,

Pelegi alikuwa mwana wa Eberi,

Eberi alikuwa mwana wa Sala,

3:36 Mwa 5:28-32; 11:12Sala alikuwa mwana wa Kenani,

Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi,

Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu,

Shemu alikuwa mwana wa Noa,

Noa alikuwa mwana wa Lameki,

3:37 Mwa 5:12-25Lameki alikuwa mwana wa Methusela,

Methusela alikuwa mwana wa Enoki,

Enoki alikuwa mwana wa Yaredi,

Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli,

Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani,

3:38 Mwa 5:19Kenani alikuwa mwana wa Enoshi,

Enoshi alikuwa mwana wa Sethi,

Sethi alikuwa mwana wa Adamu,

Adamu alikuwa mwana wa Mungu.

Read More of Luka 3

Luka 4:1-13

Yesu Ajaribiwa Na Shetani

(Mathayo 4:1-11; Marko 1:12-13)

4:1 Lk 1:15-45; 3:3-21; Eze 37:1; Lk 2:27Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi nyikani, 4:2 Kut 34:28; 1Fal 19:8mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula chochote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.

4:3 Mt 4:3Ibilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”

4:4 Kum 8:3Yesu akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ”

4:5 Mt 24:14Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja. 4:6 Yn 14:30Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka. Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”

4:8 Kum 6:3Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”

4:9 Mt 4:5Kisha ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, 4:10 Za 91:11, 12kwa maana imeandikwa:

“ ‘Atakuagizia malaika zake

ili wakulinde;

4:11 Za 91:12nao watakuchukua mikononi mwao,

usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

4:12 Kum 6:12Yesu akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

4:13 Ebr 4:15; Yn 14:30Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Yesu mpaka wakati mwingine ufaao.

Read More of Luka 4