Luka 3:1-22 NEN

Luka 3:1-22

Yohana Mbatizaji Aanza Kuhubiri

(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Yohana 1:19-28)

3:1 Mt 27:2Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, 3:2 Yn 18:13; Mdo 4:6; Mt 3:1nao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yohana, mwana wa Zekaria huko jangwani. 3:3 Mk 3:16; Mal 1:4Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 3:4 Isa 40:3-5; Mt 3:3; Mk 1:3; Yn 1:23Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Sauti ya mtu aliaye nyikani,

‘Itengenezeni njia ya Bwana,

yanyoosheni mapito yake.

Kila bonde litajazwa,

kila mlima na kilima vitashushwa.

Njia zilizopinda zitanyooshwa,

na zilizoparuza zitasawazishwa.

3:6 Za 98:2; Lk 2:30Nao watu wote watauona

wokovu wa Mungu.’ ”

3:7 Mt 12:34; 23:33; Rum 1:18Yohana akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 3:8 Isa 51:7; Gal 3:7Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka mawe haya. 3:9 Mt 3:10Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.”

3:10 Mdo 2:37; 16:30Ule umati wa watu ukamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?”

3:11 Isa 58:7; Eze 18:7Yohana akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.”

3:12 Lk 7:29Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Bwana na sisi inatupasa tufanyeje?”

3:13 Lk 19:8Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.”

3:14 Law 19:11Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?”

Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”

3:15 Mt 3:1; Yn 1:19-20; Mdo 13:25Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.3:15 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. 3:16 Mk 1:4; Yn 1:26, 33; Mdo 11:16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.3:16 Tafsiri nyingine zinasema ndani ya maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 3:17 Isa 30:24; Mt 13:30; 25:41Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

3:19 Mt 14:1Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, 3:20 Mt 14:3-4Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani.

Kubatizwa Kwa Bwana Yesu

(Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11)

3:21 Mt 14:23; Mk 1:35Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. 3:22 Isa 42:1; Yn 1:32-33; Mt 3:17Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Read More of Luka 3