Luka 22:63-71, Luka 23:1-25 NEN

Luka 22:63-71

Walinzi Wamdhihaki Yesu Na Kumpiga

(Mathayo 26:67-68; Marko 14:65)

22:63 Mt 26:67, 68; Mk 14:6522:63 Mt 26:67, 68; Mk 14:65Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” 22:65 Mt 16:21Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi.

Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza

(Mathayo 26:59-66; Marko 14:55-64; Yohana 18:28-38)

22:66 Mt 5:22; 27:1; Mk 15:1; Mdo 4:26; 22:5Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu,22:66 Baraza la wazee hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 22:67 Mt 26:63; Mk 14:61Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo,22:67 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. tuambie.”

Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini. 22:68 Lk 20:3-8Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. 22:69 Mk 16:19Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”

22:70 Mt 26:65; 27:11; Lk 23:3Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?”

Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”

22:71 Mt 26:65; Mk 14:62Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”

Read More of Luka 22

Luka 23:1-25

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-14; Marko 15:1-5; Yohana 18:28-38)

23:1 Mk 15:1; Yn 18:28Kisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 23:2 Lk 20:22; Yn 18:28Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo,23:2 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. mfalme.”

23:3 Mt 27:11; 1Tim 6:13Basi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Wewe wasema.”

23:4 1Tim 6:13; 2Kor 5:21Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”

23:5 Mk 1:14Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”

Yesu Apelekwa Kwa Herode

23:6 Lk 22:59Pilato aliposikia hayo akauliza, “Huyu mtu ni Mgalilaya?” 23:7 Mk 14:1; Lk 3:1Alipofahamu kwamba Yesu alikuwa chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa pia Yerusalemu.

23:8 Lk 9:9Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu yeye. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha. 23:9 Mk 14:61Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Yesu hakumjibu lolote. Wakati huo viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 23:11 Mk 15:17-19; Yn 19:2-3Herode na askari wake wakamdhihaki Yesu na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato. 23:12 Mdo 4:27Siku hiyo, Herode na Pilato wakawa marafiki; kabla ya jambo hili walikuwa na uadui kati yao.

Yesu Ahukumiwa Kifo

(Mathayo 27:15-26; Marko 15:6-15; Yohana 18:39–19:16)

23:13 Mt 27:23; Mk 15:14; Yn 18:38Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu, 23:14 Lk 23:1, 2, 4akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami nimeona hakuna msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake. Wala Herode hakumwona na kosa lolote, ndiyo sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lolote linalostahili kifo. 23:16 Mdo 16:37; 2Kor 11:23-24Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachia.” [ 23:17 Mt 27:15; Mk 15:6; Yn 18:39Kwa kuwa ilikuwa lazima kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa Sikukuu.]

23:18 Mdo 3:13-14Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyo! Tufungulie Baraba!” (Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji.)

Pilato, akitaka kumwachia Yesu, akasema nao tena. Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!”

23:22 Lk 23:18Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”

Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu zaidi, wakidai kwamba Yesu asulubiwe. Hivyo, kelele zao zikashinda. 23:24 Mt 27:26; Mk 15:15; Yn 19:17Kwa hiyo Pilato akatoa hukumu kwamba madai yao yatimizwe. Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.

Read More of Luka 23