Luka 22:39-62 NEN

Luka 22:39-62

Yesu Aomba Kwenye Mlima Wa Mizeituni

(Mathayo 26:36-46; Marko 14:32-42)

22:39 Lk 21:37; Mt 21:1Yesu akatoka, akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. 22:40 Mt 6:13; 26:41; Mk 14:38Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” 22:41 Lk 18:11Akajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 22:42 Mt 20:22; 26:39akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 22:43 Mt 4:11; 1:13Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 22:44 Yn 12:27Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wakiwa wamechoka kutokana na huzuni. 22:46 Lk 22:40Naye akawauliza, “Mbona mmelala? Amkeni, mwombe ili msije mkaingia majaribuni.”

Yesu Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Yohana 18:3-11)

22:47 Mt 26:47-57; Mk 14:43-49; Yn 18:2-11Yesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu. Lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 22:50 Mt 26:51; Mk 14:47; Yn 18:10Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.

Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

22:52 Mt 26:55; Mk 14:14-48Kisha Yesu akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 22:53 Mt 26:55; Yn 12:27; Mt 8:12; Yn 3:20Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!”

Petro Amkana Yesu

(Mathayo 26:57-75; Marko 14:53-72; Yohana 18:12-27)

22:54 Mt 26:57; Mk 14:53; Mt 26:58; Yn 18:15Kisha wakamkamata Yesu, wakamchukua, wakaenda naye mpaka nyumbani kwa kuhani mkuu. Lakini Petro akafuata kwa mbali. 22:55 Mt 26:69; Mk 14:66Walipokwisha kuwasha moto katikati ya ua na kuketi pamoja, Petro naye akaketi pamoja nao. Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!”

Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!”

22:58 Mt 26:71; Mk 14:69; Yn 18:26Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!”

22:59 Lk 23:6Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.”

Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika. 22:61 Lk 7:13Naye Bwana akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Read More of Luka 22