Luka 22:1-38 NEN

Luka 22:1-38

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

(Mathayo 26:14-16; Marko 14:10-11)

22:1 Yn 11:55Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia. 22:2 Mt 12:14Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wanatafuta njia ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu. 22:3 Mt 4:10; Mk 14:10, 1122:3 Mt 4:10; Yn 13:2; Mt 10:4Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili. 22:4 Mdo 4:1; 5:24Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 22:5 Zek 11:12Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu kwao, wakati ambapo hakuna umati wa watu.

Maandalizi Ya Pasaka

(Mathayo 26:17-25; Marko 14:12-21; Yohana 13:21-30)

22:7 Kum 16:5-8; Mk 4:12Basi ikawadia siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa. 22:8 Mdo 3:1, 11; 4:13-19Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohana, akisema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuweze kuila.”

Wakamuuliza, “Unataka tukuandalie wapi?”

Yesu akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia. Nanyi mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kikiwa kimepambwa vizuri. Andaeni humo.”

22:13 Lk 19:32Wakaenda, nao wakakuta kila kitu kama Yesu alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Yohana 13:36-38)

22:14 Mk 6:30; Mt 26:20; Mk 14:17-18Wakati ulipowadia, Yesu akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. 22:15 Mt 16:21Kisha akawaambia, “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 22:16 Lk 14:15; Ufu 19:9Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka mpaka itakapotimizwa katika Ufalme wa Mungu.”

Akiisha kukichukua kikombe, akashukuru, akasema, “Chukueni hiki mnywe wote. 22:18 Mt 26:29; Mk 14:29Kwa maana nawaambia tangu sasa sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

22:19 Mt 14:19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”

22:20 Zek 9:11; 2Kor 3:6Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu. 22:21 Za 41:9Lakini mkono wake huyo atakayenisaliti uko hapa mezani pamoja nami. 22:22 Mt 8:20; Mdo 2:23; 4:29Mwana wa Adamu anaenda zake kama ilivyokusudiwa. Lakini ole wake mtu huyo amsalitiye.” 22:23 Mt 26:22; Yn 13:22, 25Wakaanza kuulizana wenyewe ni nani miongoni mwao angeweza kufanya jambo hilo.

Mabishano Kuhusu Ukuu

22:24 Mk 9:34; Lk 9:46Pia yakazuka mabishano katikati ya wanafunzi kwamba ni nani aliyeonekana kuwa mkuu kuliko wote miongoni mwao. Yesu akawaambia, “Wafalme na watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu. Nao wenye mamlaka juu yao hujiita ‘Wafadhili.’ 22:26 1Pet 5:5; Mk 9:35; Lk 12:37Lakini ninyi msifanane nao. Bali yeye aliye mkuu kuliko wote miongoni mwenu, inampasa kuwa kama yeye aliye mdogo wa wote, naye atawalaye na awe kama yeye ahudumuye. 22:27 Mt 20:28; Lk 12:37Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule aketiye mezani au ni yule ahudumuye? Si ni yule aliyekaa mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule ahudumuye. 22:28 Ebr 4:15Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu. 22:29 Mt 25:34; 2Tim 2:12Nami kama Baba yangu alivyonipa ufalme, kadhalika mimi nami ninawapa ninyi, ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu, na kukaa katika viti vya enzi, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.”

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

22:31 Ay 16:12; Amo 9:9Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. 22:32 Yn 17:9-15; Rum 8:34; Yn 21:15-17Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”

22:33 Yn 11:16Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.”

22:34 Mt 26:34; Mk 14:30; Yn 13:38Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba hunijui mimi.”

Mfuko, Mkoba Na Upanga

22:35 Mt 10:9-10; Lk 9:3Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?”

Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu chochote.”

Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko na auchukue, na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga, auze joho lake anunue mmoja. 22:37 Isa 53:12Kwa sababu, nawaambia, andiko hili lazima litimizwe juu yangu, kwamba, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji’; kwa kweli yaliyoandikwa kunihusu mimi hayana budi kutimizwa.”

Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna panga mbili.”

Akawajibu, “Inatosha.”

Read More of Luka 22