Luka 2:21-40 NEN

Luka 2:21-40

2:21 Lk 1:31, 59Hata zilipotimia siku nane, ulikuwa ndio wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Yesu, jina alilokuwa amepewa na malaika kabla hajatungwa mimba.

Yesu Apelekwa Hekaluni

2:22 Law 12:2-8Ulipotimia wakati wa utakaso wake Maria kwa mujibu wa Sheria ya Mose, basi Yosefu na Maria walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Bwana 2:23 Kut 2:12-15; Hes 3:13(kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana”), 2:24 Law 12:8na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa.”

2:25 Lk 16:6; 23:51; Isa 52:9Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 2:26 Za 89:48; Ebr 11:5Roho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Kristo wa Bwana. 2:27 Mwa 46:30; Flp 1:23; Lk 2:22Simeoni, akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria, ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema:

2:29 Mdo 2:24“Bwana Mwenyezi, kama ulivyoahidi,

sasa wamruhusu mtumishi wako

aende zake kwa amani.

2:30 Isa 40:5; Lk 3:6; Isa 52:10Kwa maana macho yangu yameuona wokovu wako,

ulioweka tayari machoni pa watu wote,

2:32 Isa 49:6; Mdo 26:23nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa

na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.”

Naye Yosefu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. 2:34 Mt 12:46; Isa 8:14; Gal 5:11Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, 2:35 Za 42:10; Yn 19:25ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.”

2:36 Mdo 21:9Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa. 2:37 1Tim 5:9; Mdo 14:23Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba. 2:38 Isa 52:9; Lk 24:21Wakati huo huo, Ana alikuja akaanza kusifu, akimshukuru Mungu na kusema habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu.

2:39 Mt 2:23Yosefu na Maria walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Sheria ya Bwana, walirudi mjini kwao Nazareti huko Galilaya. 2:40 Lk 2:52; 1:80Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akiwa amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Read More of Luka 2