Luka 18:1-30 NEN

Luka 18:1-30

Mfano Wa Mjane Asiyekata Tamaa

18:1 Rum 1:10; Kol 4:2Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa. Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwepo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 18:3 Isa 1:17Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’

“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Ijapokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 18:5 Lk 11:8lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ”

18:6 Lk 7:13Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 18:7 Za 88:1; Ufu 6:10Je, Mungu hatawatendea haki wateule wake wanaomlilia usiku na mchana? Je, atakawia kuwasaidia? 18:8 Mt 8:20; 16:27Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?”

Mfano Wa Farisayo Na Mtoza Ushuru

18:9 Lk 16:15; Isa 65:5Yesu akatoa mfano huu kwa wale waliojiamini kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine: 18:10 Mdo 3:1“Watu wawili walikwenda Hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 18:11 Za 135:2; Isa 1; 15; 58:2; Ufu 3:17Yule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyangʼanyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 18:12 Isa 58:3; Mt 9:14; Mal 3:8; Lk 11:42Mimi nafunga mara mbili kwa juma, na natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’

18:13 Isa 66:2; Lk 23:48; 5:32; 1Tim 1:15“Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

18:14 Mt 23:12; Lk 14:11“Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa, na yeyote ajishushaye atakwezwa.”

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

(Mathayo 19:13-15; Marko 10:13-16)

18:15 Mt 19:13; Lk 10:13Pia, watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wachanga ili awaguse. Wanafunzi wake walipoona hivyo, wakawakemea. 18:16 1Kor 14:20; 1Pet 2:2Lakini Yesu akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 18:17 Mt 11:25; 18:3Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”

Mtawala Tajiri

(Mathayo 19:16-30; Marko 10:17-31)

18:18 Mt 19:16-29; Mk 10:17-3018:18 Lk 10:25Mtawala mmoja akamuuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. 18:20 Kut 20:12-16; Rum 13:9Unazijua amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

Akajibu, “Amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”

18:22 Mdo 2:45; Mt 6:20Yesu aliposikia haya, akamwambia, “Bado kuna jambo moja ulilopungukiwa. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Aliposikia jambo hili, alisikitika sana kwa maana alikuwa mtu mwenye mali nyingi. 18:24 Mit 11:28Yesu akamtazama, akasema, “Tazama jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! Hakika ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

Wale waliosikia haya wakauliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

18:27 Mt 19:26Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.”

18:28 Mt 4:19Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!”

18:29 Kum 33:9Yesu akajibu, “Amin, nawaambia, hakuna hata mtu aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu 18:30 Mt 12:32; 25:46ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya, na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.”

Read More of Luka 18