Luka 17:11-37 NEN

Luka 17:11-37

Yesu Atakasa Wakoma Kumi

17:11 Lk 9:51-52; Yn 4:3-4Yesu alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. 17:12 Mt 8:2; Law 13:45-46Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, 17:13 Lk 5:5wakapaza sauti, wakasema, “Yesu, Bwana, tuhurumie!”

17:14 Law 14:2; Mt 8:4Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.

17:15 Mt 9:8Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 17:16 Mt 10:5Akajitupa miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

Yesu akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” 17:19 Mt 9:22Yesu akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.”

Kuja Kwa Ufalme Wa Mungu

(Mathayo 24:23-28, 37-41)

17:20 Yn 18:36; 3:3Yesu alipoulizwa na Mafarisayo Ufalme wa Mungu utakuja lini, yeye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza kwa bidii, 17:21 Mt 24:23; Yn 1:26; 12:35wala watu hawatasema, ‘Huu hapa,’ au ‘Ule kule,’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

17:22 Mt 8:20; 9:15; Lk 5:35Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 17:23 Mt 24:23; Mk 13:21Watu watawaambia, ‘Yule kule!’ Au, ‘Huyu hapa!’ Msiwakimbilie. 17:24 Mt 24:27Kwa maana kama vile umeme wa radi umulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. 17:25 Mt 16:21; Lk 9:22; Mk 13:30; Lk 18:32Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.

17:26 Mwa 6:5-8; 7:6-24“Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. 17:27 Mwa 7:7-23Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Noa alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote.

17:28 Mwa 19:1-28“Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Loti: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. 17:29 Mwa 19:1-28Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote.

17:30 2Pet 3:4; Ufu 1:7“Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. 17:31 Mt 24:17-18; Mk 13:15-16Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote. 17:32 Mwa 19:26Mkumbukeni mke wa Loti! 17:33 Yn 12:25Mtu yeyote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa. 17:34 Mt 24:40, 41; 1The 4:17Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. 17:35 Mt 24:41Wanawake wawili watakuwa wanasaga nafaka pamoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. [ Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.]”

17:37 Mt 24:28Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana?”

Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.”

Read More of Luka 17