Luka 13:1-30 NEN

Luka 13:1-30

Tubu, La Sivyo Utaangamia

13:1 Mt 27:2Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Yesu habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. 13:2 Yn 9:2-3Yesu akawauliza, “Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo cha namna hiyo walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 13:3 Za 7:12La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo. 13:4 Yn 9:7-11Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? 13:5 Mt 3:2; Mdo 2:38Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.”

Mfano Wa Mti Usiozaa Matunda

13:6 Isa 5:2; Mt 21:19Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja. 13:7 Mt 3:10Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’

13:8 2Pet 3:9, 15“Yule mtunza shamba akamjibu, ‘Bwana, uache tena kwa mwaka mmoja zaidi, nami nitaupalilia na kuuwekea mbolea. Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vyema, la sivyo uukate.’ ”

Yesu Amponya Mwanamke Kilema Siku Ya Sabato

13:10 Mt 4:23Basi Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo siku ya Sabato. 13:11 Lk 13:16Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 13:13 Mt 5:23Yesu alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu.

13:14 Mt 12:2; Lk 14:3; Kut 20:9; Mk 5:22Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia ule umati wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.”

13:15 Lk 14:5Lakini Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ngʼombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato? 13:16 Lk 3:8; 19:9; Mt 4:10Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka kifungo hicho siku ya Sabato?”

13:17 Isa 66:5Aliposema haya, wapinzani wake wakaaibika, lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya.

Mfano Wa Punje Ya Haradali

(Mathayo 13:31-32; Marko 4:30-32)

13:18 Mt 3:2; 13:24Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaufananisha na nini? 13:19 Lk 17:6; Mt 13:32Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

(Mathayo 13:33)

Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini? 13:21 1Kor 5:6Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

Mlango Mwembamba

(Mathayo 7:13-14, 21-23)

13:22 Lk 9:51Yesu akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu. Mtu mmoja akamuuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?”

13:24 Mt 7:13Yesu akawaambia, “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza. 13:25 Mt 7:23; 25:10-12Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’

“Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’

13:26 Mt 7:22, 23“Ndipo mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, tena ulifundisha katika mitaa yetu.’

13:27 Mt 25:41“Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’

13:28 Mt 8:11-12“Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapowaona Abrahamu, Isaki, Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje. 13:29 Mal 1:11; Isa 49:12; 59:19; Za 107:3; Lk 14:15Watu watatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika Ufalme wa Mungu. 13:30 Mt 19:30Tazama, kunao walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, nao wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.”

Read More of Luka 13