Luka 11:33-54 NEN

Luka 11:33-54

Taa Ya Mwili

(Mathayo 5:15; 6:22-23)

11:33 Mt 5:15; Mk 4:21“Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru. 11:34 Mt 6:22; 2711:34 Mt 6:22; 23Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza. Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyoko ndani yako isiwe giza. Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.”

Yesu Awashutumu Mafarisayo Na Wanasheria

(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)

11:37 Lk 7:36; 14:1Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani. 11:38 Mk 7:3-4Yule Farisayo akashangaa kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula.

11:39 Lk 7:13; Mt 23:25-26; Mk 7:20-23Ndipo Bwana akamwambia, “Sasa, enyi Mafarisayo, mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na uovu. 11:40 Lk 12:20; 1Kor 15:36Enyi wapumbavu! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza nje ndiye alitengeneza na ndani pia? 11:41 Lk 12:33; Mdo 10:15Basi toeni sadaka ya vile mlivyo navyo, na tazama, vitu vyote vitakuwa safi kwenu.

11:42 Lk 18:12; Kum 6:5; Mik 6:8; Mt 23:23“Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kufanya haya ya pili bila kupuuza hayo ya kwanza.

11:43 Mt 23:6-7; Mk 12:38-39“Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kukalia viti vya mbele katika masinagogi, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.

11:44 Mt 23:27-35“Ole wenu, kwa sababu ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

11:45 Mt 22:35Mtaalamu mmoja wa sheria akamjibu, akasema, “Mwalimu, unaposema mambo haya, unatutukana na sisi pia.”

11:46 Mt 23:4Yesu akamjibu, “Nanyi wataalamu wa sheria, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.

11:47 Mt 23:29“Ole wenu, kwa sababu ninyi mnajenga makaburi ya manabii waliouawa na baba zenu. 11:48 Mt 23:29-32; Mdo 7:51-53Hivyo ninyi mwashuhudia na mnathibitisha kile baba zenu walichofanya. Wao waliwaua manabii, nanyi mnawajengea makaburi. 11:49 1Kor 1:24; Kol 2:3Kwa sababu ya jambo hili, Mungu katika hekima yake alisema, ‘Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na wengine watawatesa.’ Kwa hiyo kizazi hiki kitawajibika kwa ajili ya damu ya manabii iliyomwagwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, 11:51 Mwa 4:8; 2Nya 24:20-21; Mt 23:35-36tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zekaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, nawaambia, kizazi hiki kitawajibika kwa haya yote.

11:52 Mt 23:13“Ole wenu ninyi wataalamu wa sheria, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”

Yesu alipoondoka huko, walimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kumpinga vikali na kumsonga kwa maswali, 11:54 Mt 12:10; Mk 12:13wakivizia kumkamata kwa kitu atakachosema ili wamshtaki.

Read More of Luka 11