Walawi 9:1-24, Walawi 10:1-20 NEN

Walawi 9:1-24

Makuhani Waanza Huduma Yao

9:1 Eze 43:27; Law 4:15Katika siku ya nane, Mose akawaita Aroni na wanawe, na wazee wa Israeli. 9:2 Law 4:3; 8:14-18Akamwambia Aroni, “Chukua ndama dume kwa ajili ya sadaka yako ya dhambi, na kondoo dume kwa sadaka yako ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, nao uwalete mbele za Bwana. 9:3 Law 4:3, 32; 10:16; Ezr 6:17; Isa 53:10; Rum 8:3; 1Pet 2:24Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, 9:4 Law 4:10; Kut 32:6; 29:43; 9:6; 16:7; 24:16; 40:34-35; 1Fal 8:10-12na pia maksai na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya amani, ili kutoa dhabihu mbele za Bwana, pamoja na sadaka ya nafaka iliyochanganywa na mafuta. Kwa kuwa leo Bwana atawatokea.’ ”

Wakavileta vile vitu Mose alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, nalo kusanyiko lote likakaribia na kusimama mbele za Bwana. Ndipo Mose akasema, “Hili ndilo Bwana alilowaagiza mlifanye, ili utukufu wa Bwana upate kuonekana kwenu.”

9:7 Law 16:6; Kut 30:10; Ebr 4:1-4; 7:27; 1Sam 3:14Mose akamwambia Aroni, “Njoo madhabahuni ili utoe dhabihu yako ya sadaka ya dhambi na sadaka yako ya kuteketezwa, ufanye upatanisho kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya watu. Kisha utoe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya watu, kama vile Bwana alivyoagiza.”

9:8 Law 4:1-12; 10:19; 9:9; Kut 29:12; Eze 43:20; Law 4:7; 8:15Hivyo Aroni akaja madhabahuni na kumchinja yule ndama kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe. Wanawe wakamletea damu, naye akachovya kidole chake katika hiyo damu, akaitia kwenye pembe za madhabahu, nayo damu iliyobaki akaimwaga chini ya madhabahu. Juu ya madhabahu akateketeza mafuta, figo na mafuta yanayofunika ini kutoka kwenye hiyo sadaka ya dhambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 9:11 Law 4:11-12Akateketeza nyama na ngozi nje ya kambi.

9:12 Law 10:19Kisha Aroni akachinja sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu. 9:13 Law 1:8-9Wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu. 9:14 Isa 53:10; 1Kor 15:3; 2Kor 5:21; Gal 1:4; Ebr 2:17; 1Pet 2:24; 3:18Akasafisha sehemu za ndani na miguu, akaviteketeza juu ya sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.

9:15 Law 4:27-31Kisha Aroni akaleta sadaka ile iliyokuwa kwa ajili ya watu. Akachukua yule mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, akamchinja na kumtoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kama alivyofanya kwa ile ya kwanza.

9:16 Law 1:1-13Aroni akaleta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama ilivyoelekezwa. 9:17 Law 2:1-2; 3:5; Kut 29:38; 9:18; Law 3:1-11Pia akaleta sadaka ya nafaka, akachukua konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.

Akachinja maksai na kondoo dume kama sadaka ya amani kwa ajili ya watu. Wanawe Aroni wakampa ile damu, naye akainyunyiza kwenye madhabahu pande zote. Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, mafuta yaliyofunika tumbo, ya figo na yaliyofunika ini, hivi vyote wakaviweka juu ya vidari, kisha Aroni akayateketeza hayo mafuta ya wanyama juu ya madhabahu. 9:21 Kut 29:24-26; Law 7:30-34Aroni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za Bwana ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Mose alivyoagiza.

9:22 Mwa 48:20; Kut 39:43; Lk 24:50Kisha Aroni akainua mikono yake kuwaelekea watu na kuwabariki. Naye baada ya kutoa dhabihu ya sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani, akashuka chini.

9:23 Kut 40:2; 24:16; 2Sam 6:18; 2Nya 16:2; Hes 16:19Kisha Mose na Aroni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje, wakawabariki watu. Nao utukufu wa Bwana ukawatokea watu wote. 9:24 Kut 19:18; Amu 6:21; 13:20; 1Fal 18:39; Mwa 15:17; 2Nya 7:1; Ezr 3:1Moto ukaja kutoka uwepo wa Bwana, ukairamba ile sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sehemu ya mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipoona jambo hili, wakapiga kelele kwa furaha na kusujudu.

Read More of Walawi 9

Walawi 10:1-20

Kifo Cha Nadabu Na Abihu

10:1 Kut 6:23; 24:1; 28:1; 30:9; Hes 3:2-4; 16:46; 26:61; 16:7, 18; 1Nya 6:3; 1Fal 7:50; Yer 52:19; 2Fal 25:15; 2Nya 4:22; Eze 8:11; Law 16:12; Isa 6:6Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea Bwana moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu. 10:2 Za 2:12; 50:3; 106:18; Hes 11:1; 16:35; Isa 29:6; Mwa 19:24; 38:7; 1Nya 24:2; Ay 1:16Hivyo moto ukaja kutoka kwa uwepo wa Bwana na kuwaramba, nao wakafa mbele za Bwana. 10:3 Kut 14:4; 19:22; 30:29; Law 21:6; 22:32; Hes 16:5; 20:13; Isa 5:16; 44:23; 49:3; 55:5; 60:21; Eze 28:22; 38:16Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonena Bwana wakati aliposema:

“ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia

nitajionyesha kuwa mtakatifu;

machoni pa watu wote

nitaheshimiwa.’ ”

Aroni akanyamaza.

10:4 Kut 6:18-22; 25:8; Mdo 5:6-10Mose akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Aroni, akawaambia, “Njooni hapa. Ondoeni miili ya binamu zenu mbele ya mahali patakatifu, mkaipeleke nje ya kambi.” 10:5 Law 8:13; 10:6; Kut 6:23; Law 13:45; 21:10; Hes 1:53; 5:18; 16:22; 20:29; Yer 41:5; Mk 14:63; Yos 7:1; 22:18; Mwa 50:3, 10; 1Sam 25:1Hivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa bado wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Mose alivyoamuru.

Ndipo Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa na Bwana ataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, wanaweza kuwaombolezea wale ambao Bwana amewaangamiza kwa moto. 10:7 Kut 25:8; 28:41; Law 21:12Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya Bwana ya upako yako juu yenu.” Hivyo wakafanya kama vile Mose alivyosema.

Kisha Bwana akamwambia Aroni, 10:9 Mwa 9:21; Kut 12:14; 29:40; Law 23:13; Hes 6:3; 15:5; 28:7; Kum 14:26; 28:39; 29:6; Isa 5:22; 22:13; 28:1, 7; Yer 35:6; Hos 4:11; Hab 2:15-16; Amu 13:4; Mit 21:1; 23:29-35; 31:4-7; Eze 44:21; Mik 2:11; Lk 1:15; Efe 5:18; 1Tim 3:3; Tit 1:7“Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 10:10 Mwa 7:2; Law 6:27; 14:57; 20:25; Eze 22:26; 10:11; 2Nya 15:3; 17:7; Ezr 7:25; Neh 8:7; Mal 2:7; Kum 17:10-11; 24:8; 25:1; 33:10; Mit 4:27; Hag 2:11Ni lazima mtenganishe kilicho kitakatifu na kile kilicho cha kawaida, kati ya yaliyo najisi na yaliyo safi, na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazo Bwana aliwapa kupitia Mose.”

10:12 Kut 29:41; Law 6:14-18; 10:13; 6:16; Eze 42:13Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe waliosalia, Eleazari na Ithamari, “Chukueni sadaka ya nafaka iliyobaki kutoka sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, muile hapo kando ya madhabahu ikiwa imeandaliwa bila chachu, kwa sababu ni takatifu sana. Mtaila katika mahali patakatifu kwa sababu ni fungu lenu na fungu la wana wenu la sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, kwa maana hivyo ndivyo nilivyoamriwa. 10:14 Hes 5:9; Kut 29:31; Law 4:12Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli. 10:15 Law 7:34; Kut 29:28Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za Bwana kama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kama Bwana alivyoagiza.”

10:16 Law 9:3Mose alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliobaki, akawauliza, 10:17 Law 6:24-30; Eze 42:13; Kut 28:38“Kwa nini hamkula sadaka ya dhambi katika eneo la mahali patakatifu? Ni takatifu sana. Mlipewa ninyi ili kuondoa hatia ya jumuiya kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho mbele za Bwana. 10:18 Law 4:18; 6:17, 26, 30Kwa kuwa damu yake haikuletwa ndani ya Mahali Patakatifu, mngemla mbuzi huyo katika sehemu ya mahali patakatifu kama nilivyoagiza.”

10:19 Law 9:12; Yer 6:20; 14:12; Hos 9:4; Mal 1:10Aroni akamjibu Mose, “Leo wanangu wametoa sadaka zao za dhambi na sadaka zao za kuteketezwa mbele za Bwana, lakini mambo kama haya yamenitokea mimi. Je, Bwana angependezwa kama ningekuwa nimekula sadaka ya dhambi leo?” Mose aliposikia haya, akaridhika.

Read More of Walawi 10