Walawi 7:11-38, Walawi 8:1-36 NEN

Walawi 7:11-38

Sadaka Ya Amani

“ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwa Bwana:

7:12 Law 2:1-4; 22:29; Za 50:14; 54:6; 107:22; 116:17; Yer 33:11; 44:19; Hes 6:19“ ‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonyesha shukrani, pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu iliyopakwa mafuta, maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta. 7:13 Kut 34:22; Law 23:17; Amo 4:5Pamoja na sadaka hii ya amani ya shukrani ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu. 7:14 Hes 18:8Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwa Bwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani. 7:15 Kut 12:10; Law 22:30; Ebr 3:13-15Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote mpaka asubuhi.

7:16 Mwa 28:20; Kum 12:6; 23:21-23; Kut 35:29; Law 19:5-9; 22:18-21; 23:38; Hes 15:3; 29:39; Za 54:6; Eze 46:12“ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake. 7:17 Kut 12:10; Law 19:6Nyama yoyote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto. 7:18 2Nya 33:16; Law 5:1; 19:7; Hes 18:27; Mwa 4:4-5; Mit 15:8; 21:27; Yer 6:20; Amo 5:22Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, Bwana hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia.

“ ‘Nyama ile inayogusa chochote ambacho ni najisi kwa kawaida ya ibada kamwe haitaliwa, ni lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu yeyote aliye safi kwa kawaida ya ibada anaweza kuila. 7:20 Law 5:3; 22:3-7; Mwa 17:14; Law 15:3Lakini kama mtu yeyote najisi akila nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, huyo mtu lazima akatiliwe mbali na watu wake. 7:21 Law 5:2; 11:24-28; 11:10-13; Kum 14:3; Eze 4:14Kama mtu yeyote akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu chochote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Kula Mafuta Na Kunywa Damu Kwakatazwa

Bwana akamwambia Mose, 7:23 Law 17:13; Kum 14:4; 1Sam 2:29“Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yoyote ya ngʼombe, kondoo wala mbuzi. 7:24 Kut 22:31Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale. Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa Bwana kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 7:26 Mwa 9:4; Law 3:17; 17:10-14; Kum 12:16; 1Sam 14:33; Eze 44:15; Mdo 15:20Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. 7:27 Mwa 9:4; Mdo 15:20-29Ikiwa mtu yeyote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Fungu La Makuhani

Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote aletaye sadaka ya amani kwa Bwana ataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwa Bwana. 7:30 Kut 29:24; Hes 6:20; Law 8:27; 9:21Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 7:31 Kut 29:27, 31Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe. 7:32 Kut 29:27; Law 10:14-15; Hes 5:9; 6:20; 18:18Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo. Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake. 7:34 Kut 29:22, 27; Law 10:15; Hes 6:20; 18:18-19; 1Sam 9:24Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’ ”

Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia Bwana katika kazi ya ukuhani. 7:36 Law 8:12, 30; Kut 40:13-15; Ebr 7:18-28; 8:1-13Siku ile walipotiwa mafuta, Bwana aliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la kawaida kwa vizazi vijavyo.

7:37 Law 6:9, 14; Kut 29:31; Law 6:20Basi haya ndiyo masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu, na sadaka ya amani, 7:38 Law 26:46; Hes 36:13; Kum 4:5; 29:1-3; Kut 19:11ambayo Bwana alimpa Mose juu ya Mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwa Bwana, katika Jangwa la Sinai.

Read More of Walawi 7

Walawi 8:1-36

Kuwekwa Wakfu Kwa Aroni Na Wanawe

(Kutoka 29:1-37)

Bwana akamwambia Mose, 8:2 Kut 28:1-4, 43; 30:10, 23-30; 39:27; 29:2-3; Law 1:5“Waletee Aroni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu. 8:3 Hes 8:9Kisha kusanya mkutano wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.” Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza, na mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

Mose akaliambia kusanyiko, “Hili ndilo Bwana ameagiza lifanyike.” 8:6 Kut 29:4; 30:19; Mdo 22:16; Za 26:6; 1Kor 6:11; Isa 52:11; Eze 36:25; Efe 5:26; Ebr 9:9-14Kisha Mose akamleta Aroni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. 8:7 Kut 28:4Akamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi. 8:8 Kut 25:7; 28:30; Hes 27:21; Kum 33:8; 1Sam 28:6; Neh 7:65Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu8:8 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. kwenye hicho kifuko. 8:9 Kut 39:28; 28:2, 36; Law 21:10; Kut 29:6; Zek 3:5; 6:11Kisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

8:10 Kut 30:26; 26:1Ndipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu. 8:11 Kut 30:29Akanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu. 8:12 Law 7:36; 21:10-12; Kut 30:30; 29:7; Za 133:2; Isa 61:2; 8:13; Kut 28:4; Law 21:10; Za 132:9; Isa 61:10Akamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Aroni, akamtia mafuta ili kumweka wakfu. Kisha akawaleta wana wa Aroni mbele, akawavika makoti, akawafunga mishipi na kuwavika vilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

8:14 Law 4:3, 15; Kut 30:10; 29:10; Za 51:19; Eze 43:19; Ebr 9:13-14Kisha akamtoa fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nao Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. 8:15 Law 4:7, 18; Ebr 9:22; Eze 43:20Mose akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kutakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. Kwa hiyo akayaweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu. 8:16 Kut 29:13; Law 4:8; 8:17; 4:11-12; Kut 29:14Pia Mose akachukua mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, akayateketeza juu ya madhabahu. Lakini fahali, ikiwa pamoja na ngozi yake na nyama yake na sehemu zake za ndani na matumbo, akaiteketeza nje ya kambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

8:18 Kut 29:15; 8:22; Law 4:15; Kut 29:19, 31; Law 7:37Kisha Mose akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. Ndipo Mose akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. Mose akamkata yule kondoo dume vipande vipande na kukiteketeza kichwa, vile vipande na yale mafuta. Kisha akamsafisha sehemu za ndani na miguu kwa maji, na kumteketeza yule kondoo dume mzima juu ya madhabahu kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Kisha akaleta kondoo dume mwingine, ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. 8:23 Law 14:14, 25; 8:23; Rum 12:1; 1Kor 6:20Mose akamchinja yule kondoo dume, akaichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Aroni, na juu ya kidole gumba cha mkono wake wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. 8:24 Ebr 9:18-22Pia Mose akawaleta hao wana wa Aroni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu. 8:25 Law 3:3-5; Kut 29:22Akachukua mafuta ya mnyama, mafuta ya mkia, mafuta yote yanayozunguka sehemu za ndani, mafuta yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, na paja la kulia. 8:26 Law 2:4Kisha kutoka kwenye kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichokuwa mbele za Bwana, akachukua andazi moja, na jingine lililotengenezwa kwa mafuta, na mkate mwembamba; akaviweka hivi vyote juu ya mafungu ya mafuta ya mnyama, na juu ya lile paja la kulia. 8:27 Hes 5:25Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe, na kuviinua mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 8:28 Kut 29:25; Mwa 8:21; Efe 5:2Kisha Mose akavichukua kutoka mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kuwa sadaka ya kuwekwa wakfu, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 8:29 Law 7:31-34Kisha akachukua kidari, kilicho fungu la Mose la kondoo dume kwa ajili ya kuwekwa wakfu, na kukiinua mbele za Bwana kama sadaka ya kuinuliwa, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

8:30 Kut 28:1-2; Law 7:36; Kut 30:30; Hes 3:3; 1Pet 1:2Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao.

8:31 Law 6:16; Kut 29:31; Eze 46:20Kisha Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Pika hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na uile hapo pamoja na mkate kutoka kwenye kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza, nikisema, ‘Aroni na wanawe wataila.’ Kisha teketeza nyama na mikate iliyobaki. 8:33 Law 14:8; 15:13, 28; Hes 19:11; Eze 43:25Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, mpaka siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba. 8:34 Ebr 7:16; Law 18:30; 22:9; Hes 3:7; 9:19; Kum 11:1; 1Fal 2:3; Eze 48:11; 3:7; 1Tim 5:21Lile lililofanyika leo liliagizwa na Bwana ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Lazima mkae kwenye ingilio la Hema la Kukutania usiku na mchana kwa siku saba, na kufanya lile Bwana analolitaka, ili kwamba msife; kwa kuwa hilo ndilo nililoamriwa.” Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya kila kitu Bwana alichoamuru kupitia kwa Mose.

Read More of Walawi 8