Walawi 21:1-24, Walawi 22:1-33 NEN

Walawi 21:1-24

Sheria Kwa Ajili Ya Makuhani

21:1 Kut 28:1; Law 5:3; 13:3; Hes 5:2; 6:6; 19:11; 31:19; Eze 44:25Bwana akamwambia Mose, “Sema na makuhani, wana wa Aroni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa utaratibu wa kiibada kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa, isipokuwa jamaa wake wa karibu, kama vile mama yake au baba yake, mwanawe au binti yake, ndugu yake, 21:3 Hes 6:6; 21:5; Law 13:40; 19:28; Yer 7:29; 16:6; Eze 5:1; 44:20au dada yake asiyeolewa ambaye anamtegemea kwa kuwa hana mume, kwa ajili ya hao aweza kujitia unajisi. Kamwe asijitie unajisi mwenyewe kutokana na wale watu ambao anahusiana nao kwa kuoana, na hivyo kujitia unajisi.

“ ‘Kamwe makuhani wasinyoe nywele za vichwa vyao wala wasinyoe pembeni mwa ndevu zao, au kuweka chale kwenye miili yao. 21:6 Ezr 8:28; Law 18:21; 3:11; 22:25; 10:3; Kut 19:22; Law 20:7; Za 15:4; Mt 5:33-37; Yak 5:12Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao, na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Bwana, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu.

21:7 Eze 44:22; 21:8; Law 3:11; Kut 31:13; 21:9; Mwa 38:24; Law 19:29; Kut 29:29; Hes 35:25; Kut 28:2“ ‘Kamwe wasioe wanawake waliojinajisi kwa ukahaba, au waliopewa talaka na waume wao, kwa sababu makuhani ni watakatifu kwa Mungu wao. Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu Mimi Bwana ni mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi kuwa watakatifu.

“ ‘Ikiwa binti wa kuhani anajitia unajisi kwa kufanya ukahaba, anamwaibisha baba yake; lazima achomwe kwa moto.

21:10 Kut 29:7; Law 8:7-13; 16:4; 10:6“ ‘Kuhani mkuu, yule miongoni mwa ndugu zake ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake, na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa, wala asirarue nguo zake. 21:11 Hes 5:2; 6:6; 9:6; 19:11-14; 31:19; Law 19:28Kamwe asiingie mahali palipo maiti ndani. Kamwe asijitie unajisi, hata kwa ajili ya baba yake au mama yake, 21:12 Kut 25:8; 28:41; Law 10:7wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimi Bwana.

21:13 Eze 44:22“ ‘Mwanamke kuhani atakayemwoa lazima awe bikira. Kamwe asimwoe mjane, au mwanamke aliyepewa talaka, wala mwanamke aliyejinajisi kwa ukahaba, bali atamwoa tu bikira kutoka miongoni mwa watu wake, 21:15 Rum 12:1; 1Kor 3:16; Efe 5:17; 1The 4:1-8na hivyo hatawatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. Mimi ndimi Bwana, nimfanyaye mtakatifu.’ ”

Bwana akamwambia Mose, 21:17 Hes 16:5; Za 64:4“Mwambie Aroni: ‘Kwa vizazi vijavyo, hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake. 21:18 Law 22:19-25; 19:14; 2Sam 4:4; 9:3; 19:26Hakuna mtu mwenye dosari yoyote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili, hakuna mtu mwenye mguu au mkono uliolemaa, 21:20 Law 22:24; Kum 23:1; Isa 56:3au mwenye kibiongo au aliyedumaa, au aliye na tatizo la macho, au aliye na uvimbe wenye usaha au majipu, au aliyehasiwa. 21:21 Law 3:11; 22:19Hakuna mzao wa kuhani Aroni mwenye kilema chochote atakayekaribia kutoa sadaka kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake. 21:22 1Kor 9:13Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu. 21:23 Kut 25:8; Law 20:8; Hes 18:19Lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie karibu na pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye watakatifu.’ ”

Basi Mose akamwambia Aroni jambo hili na wanawe, pamoja na Waisraeli wote.

Read More of Walawi 21

Walawi 22:1-33

Matumizi Ya Sadaka Takatifu

Bwana akamwambia Mose, 22:2 Law 19:8; Kut 20:7; Mt 5:33; Eze 44:8; Hes 15:15, 31; Kut 28:38; Kum 15:19“Mwambie Aroni na wanawe kushughulikia kwa uangalifu sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwangu, ili wasilinajisi Jina langu takatifu. Mimi ndimi Bwana.

22:3 Ezr 8:28; Law 7:20-21; Hes 19:13“Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa yeyote wa wazao wako ni najisi kwa taratibu za kiibada, naye akakaribia sadaka takatifu zile Waisraeli wanazoweka wakfu kwa Bwana, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimi Bwana.

22:4 Law 14:1-32; 15:2-15; 11:24-28, 39; Hes 19:11“ ‘Ikiwa mzao wa Aroni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Pia atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu chochote kilicho najisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa, 22:5 Law 11:24-28, 43; 15:7au ikiwa atagusa kitu chochote kitambaacho kimfanyacho mtu najisi, au mtu yeyote awezaye kumtia unajisi, hata unajisi uwe gani. 22:6 Hag 2:13; Law 11:24; 14:8; Ebr 10:22Mtu anayegusa kitu chochote cha aina hiyo atakuwa najisi mpaka jioni. Kamwe hatakula sadaka yoyote takatifu mpaka yeye mwenyewe awe ameoga kwa maji. 22:7 Hes 18:11Wakati jua linapotua, atakuwa safi, na baadaye anaweza kula sadaka takatifu, kwa kuwa ni vyakula vyake. 22:8 Law 11:39-44; 17:15; Kut 22:31Kamwe asile nyama ya mzoga wala iliyoraruliwa na wanyama pori, naye akatiwa unajisi kwa hilo. Mimi ndimi Bwana.

22:9 Law 8:35; 20:8; Kut 28:38-43; Hes 18:22“ ‘Makuhani lazima washike maagizo yangu ili wasiwe na hatia, wakafa kwa kuyadharau. Mimi ndimi Bwana ninayewafanya watakatifu.

22:10 Kut 12:45; 29:33; Hes 3:10; 1Sam 21:6“ ‘Hakuna mtu yeyote asiye wa jamaa ya kuhani anayeruhusiwa kula sadaka takatifu, hata mgeni wa kuhani au mfanyakazi wake haruhusiwi kuila. 22:11 Mwa 17:13; Kut 12:44Lakini ikiwa kuhani amenunua mtumwa kwa fedha, au mtumwa amezaliwa katika nyumba ya kuhani huyo, mtumwa huyo aweza kula chakula cha huyo kuhani. Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula chochote cha matoleo matakatifu. Lakini ikiwa binti wa kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, na akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula chochote katika chakula hiki.

22:14 Law 4:2; 5:15“ ‘Ikiwa mtu yeyote amekula sadaka takatifu kwa makosa, lazima atoe malipo ya sadaka hiyo kwa kuhani na kuongeza sehemu ya tano ya thamani ya sadaka hiyo. 22:15 Law 19:8; Hes 18:32Kamwe makuhani wasiinajisi sadaka takatifu ambayo Waisraeli wameitoa kwa Bwana 22:16 Hes 18:11; Kut 28:38; Law 20:8kwa kuwaruhusu kuzila sadaka hizo takatifu, na hivyo kuwaletea hatia ya kudaiwa malipo. Mimi ndimi Bwana niwafanyaye watakatifu.’ ”

Dhabihu Zisizokubalika

Bwana akamwambia Mose, 22:18 Hes 15:8, 16; 19:10; Yos 8:33; Mwa 28:20; Za 22:25; 76:11; 116:8; Law 7:16“Sema na Aroni na wanawe, na Waisraeli wote uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Bwana, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari, 22:19 Law 1:2; 21:18-21; Hes 28:11; Kum 15:21lazima mtoe mnyama dume asiye na dosari, akiwa ngʼombe, mbuzi au kondoo, ili aweze kukubalika kwa niaba yako. 22:20 Kum 15:21; 17:1; Eze 43:23; 45:18; 46:6; Mal 1:8; Ebr 9:14; 1Pet 1:19; Kut 28:38Kamwe usitoe kitu chochote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako. 22:21 Kut 12:5; 32:6; Law 3:6; 7:16; Mal 1:14; Amo 4:5; Hes 15:38Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa Bwana kutoka kundi la ngʼombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike. Kamwe usimtolee Bwana mnyama aliye kipofu, aliyejeruhiwa wala aliye kilema, au chochote kilicho na uvimbe, au chenye upele au vidonda vinavyotoka usaha. Kamwe chochote cha aina hii kisiwekwe juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana ya kuteketezwa kwa moto. 22:23 Law 21:18Lakini waweza ukatoa ngʼombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa kama sadaka ya hiari, lakini hii haitakubalika kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri. 22:24 Law 21:20Kamwe usimtolee Bwana mnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au kuhasiwa, au kuraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye hivi katika nchi yako mwenyewe, 22:25 Law 21:6; 1:3; 3:1; Hes 19:2; 15:15na kamwe usikubali wanyama wa aina hii kutoka mkono wa mgeni ili kuwatoa wanyama hao kuwa chakula kwa Mungu wako. Wanyama hao hawatakubaliwa kwa niaba yako, kwa sababu wana vilema, nao wana dosari.’ ”

Bwana akamwambia Mose, 22:27 Law 1:3; Kut 22:30; 28:38“Wakati ndama, mwana-kondoo au mwana-mbuzi azaliwapo, atabaki na mama yake kwa siku saba. Kuanzia siku ya nane na kuendelea anaweza kukubaliwa kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto. 22:28 Kum 22:6-7Usimchinje ngʼombe na ndama wake, au kondoo na kitoto chake siku moja.

22:29 Law 7:12; Za 107:22“Unapomtolea Bwana dhabihu ya shukrani, itoe kwa namna ambayo itakubalika kwa niaba yako. 22:30 Law 7:15; 11:44; Za 116:17Ni lazima iliwe siku iyo hiyo, pasipo kubakiza chochote mpaka asubuhi. Mimi ndimi Bwana.

22:31 Kum 4:2; Za 105:45; Kut 22:31; Law 19:37; Hes 15:40“Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimi Bwana. 22:32 Law 18:21; 10:3; 20:8Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimi Bwana ninayewafanya watakatifu, 22:33 Kut 6:6; Mwa 17:7; Law 11:45na niliyewatoa katika nchi ya Misri niwe Mungu wenu. Mimi ndimi Bwana.”

Read More of Walawi 22