Walawi 19:1-37, Walawi 20:1-27 NEN

Walawi 19:1-37

Sheria Mbalimbali

Bwana akamwambia Mose, “Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wenu, ni mtakatifu.

19:3 Kut 20:8, 12; Law 11:44; Neh 9:14; 13:15-21; Isa 58:13; Mk 2:27“ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

19:4 Kut 20:4; Amu 17:3; Za 96:5; 115:4-7; 135:15; 1Kor 10:14“ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

“ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Bwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu. 19:6 Law 7:16-18Sadaka hiyo italiwa siku iyo hiyo mnayoitoa, au kesho yake; chochote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto. Kama sehemu yoyote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi, nayo haitakubaliwa. 19:8 Law 22:2, 15-16; Hes 18:32; Mwa 17:14Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa Bwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.

19:9 Rut 2:2-7; Law 23:10, 22; Kum 24:19-22; Ay 24:10; Kut 23:11; Kum 15:1-18“ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako. 19:10 Kum 24:19-22; Za 140:12; Mit 14:31; Isa 3:12-15; Mhu 5:8Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

19:11 Kut 20:15-16; 23:4; Lk 3:14; Efe 4:25; Law 6:2; 1Fal 13:18; Yer 9:3-5; Mdo 5:3-4“ ‘Usiibe.

“ ‘Usiseme uongo.

“ ‘Msidanganyane.

19:12 Yer 5:2; 7:9; 34:16; 44:16, 26; Mal 3:5; Kut 3:13; 20:7; Kum 18:19; Mit 18:10; Isa 42:8; Mt 5:33“ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

19:13 Law 25:14, 17; Kut 20:15; 22:15, 25-27; Ay 7:2; 24:12; 31:39; Isa 16:14; Mal 3:5; Kum 24:15; Yer 22:13; Mt 20:8; 1Tim 5:18; Yak 5:4“ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako.

“ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

19:14 Kut 4:11; Law 21:18; 25:17, 36; Kum 27:18; Rum 14:13; 1Pet 2:17“ ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

19:15 Kut 13:2; 23:8; Kum 24:17; Ay 13:8, 10; 32:21; 34:19; Mit 24:23; 28:21; Mal 2:9; Yak 2:1-4“ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

19:16 Za 15:3, 5; 31:13; 41:6; 101:5; Yer 6:28; 9:4; Eze 22:9, 12; Kut 23:7; Kum 10:17; 27:25“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako.

“ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana.

19:17 1Yn 2:9; Mt 18:15; Lk 17:3; Mwa 27:41“ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

19:18 Mwa 4:23; Rum 12:19; 13:9; Ebr 10:30; Za 103:9; Kut 20:16; Mt 5:43; 19:16; 22:39; Mk 12:31; Lk 10:27; Yn 13:34; Gal 5:14; Yak 2:8“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.

19:19 Mwa 26:5; Kum 22:9, 11“ ‘Mtazishika amri zangu.

“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.

“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.

“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.

19:20 Kum 22:23-27“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru. 19:21 Law 5:15Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana. Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

“ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa. 19:24 Kut 22:29; Mit 3:9; Kum 12:17-18Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Bwana. Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

19:26 Mwa 9:4; 30:27; Isa 44:25; Eze 22:18; 2Fal 17:17“ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake.

“ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.

19:27 Law 21:5; 2Sam 10:4-5; Yer 41:5; 48:37; Eze 5:1-5; Yer 9:26“ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu.

19:28 Law 21:5; 1Fal 18:28; Yer 16:6; 41:5; 47:5“ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Bwana.

19:29 Law 21:9; Kum 23:18; Mwa 34:7“ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.

19:30 Kut 20:8; Law 26:2“ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Bwana.

19:31 Kut 22:18; 1Sam 28:7-20; 1Nya 10:13; Law 20:6; 2Fal 21:6; 23:24; Isa 8:19; 19:3; 29:4; 47:12; 65:4“ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

19:32 1Fal 12:8; Ay 29:8; 32:4; Mit 23:22; Mao 5:12; 1Tim 5:1; Law 11:44“ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase. 19:34 Kut 12:48; 22:21; 23:9; Kum 10:19; 23:7; Za 146:9Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

19:35 Kum 25:13-16“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 19:36 Ay 31:6; Mit 11:1; 20:10; Hes 12:7; Mik 6:11; Amu 6:19; Rut 2:17; 1Sam 1:24; 17:17; Eze 45:10-11; Kum 25:13-15; Kut 12:17Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa19:36 Efa kilikuwa kipimo cha vitu vikavu. halali, na hini19:36 Hini kilikuwa kipimo cha vitu vimiminika. halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

19:37 2Fal 17:37; 2Nya 7:17; Za 119:5; Eze 18:9; Mwa 26:5; Kum 6:25; Law 18:4-5“ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.’ ”

Read More of Walawi 19

Walawi 20:1-27

Adhabu Kwa Ajili Ya Dhambi

Bwana akamwambia Mose, 20:2 Mwa 26:11; Kut 19:21; Law 24:14; Hes 15:35-36; Kum 21:21; Yos 7:25; 2Fal 17:17; 23:10; 2Nya 33:6“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa yeyote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe. 20:3 Law 23:30; 15:31; 18:21; Za 74:7; 79:1; Yer 7:30; Eze 5:11; Hes 19:20Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu. 20:4 Kum 17:2-5Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumuua, 20:5 Kut 20:5; Law 17:7mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo pamoja na jamaa yake, nami nitawakatilia mbali yeye na watu wote waliofanya ukahaba na Moleki.

20:6 Law 19:31“ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayeenda kwa waaguzi na wenye pepo, na hivyo kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake.

20:7 Law 11:44, 45; Kut 29:1; 31:13; Efe 1:4; 1Pet 1:16; Kut 6:2; 20:2“ ‘Jitakaseni basi, nanyi kuweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 20:8 Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

20:9 Kut 20:12; 21:17; Yer 35:16; Mal 1:6; 2:10; Kum 21:21; 22:30; 27:16; Eze 18:13; 22:7; 33:4-5; Mt 15:4; Mk 7:10; Yos 2:19; 2Sam 1:16; 3:29; 1Fal 2:37“ ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani baba yake au mama yake, lazima auawe. Amemlaani baba yake au mama yake, nayo damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

20:10 Kut 20:14; 21:12; Kum 5:18; 22:22; Yn 8:5; Mwa 38:24“ ‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.

20:11 Law 18:7-8; Kum 27:23“ ‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

20:12 Mwa 11:31; 38:16; Law 18:15“ ‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

20:13 Law 18:22“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

20:14 Law 18:8, 17; 21:9; Hes 16:39; Amu 14:15; 15:6; Kum 27:23“ ‘Ikiwa mwanaume ataoa binti pamoja na mama yake, huo ni uovu. Wote watatu ni lazima wachomwe moto, ili kwamba pasiwepo na uovu katikati yenu.

20:15 Kut 20:10; 22:19; Law 18:23; 18:9; 5:1; Mwa 17:14; 20:12“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe.

“ ‘Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, muueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.

20:17 Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12; Mwa 26:5; Kut 31:13; Eze 20:12“ ‘Ikiwa mtu anamwoa dada yake, binti aliyezaliwa na baba yake au mama yake, nao wakakutana kimwili, ni aibu. Lazima wakatiliwe mbali machoni pa watu wao. Huyo mwanaume amemwaibisha dada yake, hivyo atawajibika kwa ajili ya uovu huo.

20:18 Law 15:24; Eze 18:6; 20:19; Law 18:2, 12“ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.

“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.

20:20 Law 18:13-14; Mwa 15:2“ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na shangazi yake, amemwaibisha mjomba wake. Nao watawajibika kwa ajili ya uovu huo; watakufa bila kuzaa mtoto.

20:21 Law 18:16; Mt 14:4; Mk 6:18“ ‘Ikiwa mwanaume ataoa mke wa ndugu yake, hili ni tendo chafu; amemwaibisha ndugu yake. Nao hawatazaa mtoto.

20:22 Mwa 26:5; Law 18:25-28“ ‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike. 20:23 Law 18:3, 24-25, 27-30Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao. 20:24 Kut 3:8; 13:5; 33:16; Hes 14:8; 16:14; 1Fal 8:53; Za 135Lakini niliwaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka mataifa.

20:25 Law 10:10; Kum 14:3-21; Mdo 10:14; Law 11:47“ ‘Kwa hiyo, ninyi lazima mweze kutofautisha kati ya wanyama walio safi na wasio safi, pia kati ya ndege wasio safi na walio safi. Msijitie unajisi kutokana na mnyama yeyote, au ndege, wala kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi, vile ambavyo nimevitenga kuwa najisi kwa ajili yenu. 20:26 Kum 14:2; Law 19:2; Yos 24:19; 2Fal 19:22Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi, Bwana, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka mataifa kuwa wangu mwenyewe.

20:27 Kut 22:18; Law 19:31; 24:14; Kum 18:10; 1Sam 28:7“ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ”

Read More of Walawi 20