Walawi 17:1-16, Walawi 18:1-30 NEN

Walawi 17:1-16

Kunywa Damu Kumekatazwa

Bwana akamwambia Mose, 17:2 Law 10:6, 12“Sema na Aroni na wanawe, pamoja na Waisraeli wote, uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana aliloagiza: 17:3 Law 3:7; 7:23Mwisraeli yeyote atakayetoa dhabihu ya maksai, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake, 17:4 1Fal 8:4; 2Nya 1:3; Kum 12:5-21; Mwa 17:14badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Bwana mbele ya Maskani ya Bwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. 17:5 Law 3:1; Eze 43:27; Mwa 21:33; 22:2; 1Fal 14:22-23Hii ni ili Waisraeli wamletee Bwana dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Bwana, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kama sadaka za amani. Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Bwana katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 17:7 Kut 12:14; 22:20; 34:15; 34:15; Yer 3:6-9; Eze 23:3; 1Kor 10:20; Mwa 9:12; Kum 32:17; 2Nya 11:15; Za 106:37Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’

“Waambie: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu 17:9 Law 1:3; 3:7bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa Bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

17:10 Mwa 9:4; Kum 12:16, 23; 1Sam 14:33; Law 26:17; Yer 44:11; Eze 15:7“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakunywa damu yoyote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake. 17:11 Mwa 9:4; Ebr 9:22Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu. Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kunywa damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kunywa damu.”

17:13 Law 7:26; Eze 24:7; 33:25; Mdo 15:20; Kum 12:16“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo, 17:14 Mwa 9:4; Law 7:24; 14:8; 11:40; Kol 1:14; Kum 14:21; Kut 22:31; Mk 14:24; Rum 5:9kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; yeyote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”

17:15 Kut 22:31; Kum 14:2; Eze 4:14“ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi. 17:16 Law 5:1; Hes 19:20; Ebr 9:28Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ”

Read More of Walawi 17

Walawi 18:1-30

Uhusiano Wa Kukutana Kimwili Kinyume Cha Sheria

Bwana akamwambia Mose, 18:2 Mwa 17:7; Eze 20:5; Kut 6:7“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 18:3 Kut 23:24; Kum 18:9; 2Fal 16:3; 17:8; 1Nya 5:25; Eze 23:8Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao. 18:4 Mwa 26:5; Kum 4:1; 1Fal 11:11; Yer 44:10, 23; Eze 11:12Ni lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 18:5 Mwa 26:5; Neh 9:20; Isa 55:2; Eze 18:9; 20:11; Amo 5:4-6; Mt 19:17; Rum 10:5; Gal 3:12Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Hakuna mtu awaye yote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Bwana.

18:7 Law 20:11; Kum 27:20; Eze 22:10-11“ ‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

18:8 1Kor 5:11; Mwa 35:22; Law 20:11; Kum 22:30; 27:20“ ‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.

18:9 Law 20:17; Kum 27:22; 2Sam 13:13; Eze 22:11“ ‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti wa baba yako, au binti wa mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.

“ ‘Usikutane kimwili na binti wa mwanao ama binti wa binti yako; utajivunjia heshima.

“ ‘Usikutane kimwili na binti wa mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.

18:12 Law 20:19“ ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.

18:13 Law 20:20“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.

“ ‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.

18:15 Mwa 11:31; 38:16; Eze 22:11; Law 20:12“ ‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.

18:16 Law 20:21; Mt 14:4; Mk 6:18“ ‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.

18:17 Law 20:14; Kum 27:23“ ‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti wa mwanawe au binti wa binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.

18:18 Mwa 30:1; Mal 2:15“ ‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.

18:19 Law 15:24-30; 20:18; Eze 18:6“ ‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.

18:20 Kut 20:14; Mt 5:27-28; 1Kor 6:9; Ebr 13:4; Mit 6:29“ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.

18:21 Kum 9:4; 12:31; 18:10; 2Fal 16:3; 17:17; 21:6; 23:10; 2Nya 28:1-4; 33:6; Za 106:37-38; Isa 48:11; 57:5; Yer 7:30-31; 19:5; 32:35; Eze 16:20; 22:26; 36:20; Mik 6:7; Law 19:12; 20:2-5; 21:6; Amo 2:7; 1Fal 11:5, 7, 33; Sef 1:5; Mal 1:12; Kut 6:2“ ‘Usimtoe mtoto wako yeyote awe kafara kwa mungu Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

18:22 Law 20:13; Kum 23:18; Rum 1:27; 1Kor 6:9; Mwa 19:5“ ‘Usikutane kimwili na mwanaume kama mtu akutanaye na mwanamke; hilo ni chukizo.

18:23 Kut 22:19; Law 20:15; Kum 27:21“ ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.

18:24 Law 20:23; Kum 9:4; 18:12; Mt 15:18; 1Kor 3:17“ ‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi. 18:25 Hes 35:34; Kum 9:5; 12:31; 18:12; 21:23; Law 20:23; Ay 20:15; Yer 51:34Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake. 18:26 Mwa 26:5; 18:28; Law 20:22; Ezr 9:11; Mao 1:17Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi. Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.

“ ‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao. 18:30 Law 8:35; Kum 11:1; 19:2; Hes 14:5; Za 68:26; Kut 20:2; 15:11; 1Pet 1:16; Law 11:44; 20:26Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.’ ”

Read More of Walawi 18