Maombolezo 3:40-66, Maombolezo 4:1-22, Maombolezo 5:1-22 NEN

Maombolezo 3:40-66

3:40 2Kor 13:5; Za 119:59; 139:23-24Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu,

na tumrudie Bwana Mungu.

3:41 Dan 9:5; Yer 14:20; 2Fal 24:4; Yer 5:7-9; Za 86:4Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu

kwa Mungu mbinguni, na tuseme:

3:42 Dan 9:5“Tumetenda dhambi na kuasi

nawe hujasamehe.

3:43 Mao 2:2, 17, 21; Za 35:6“Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia;

umetuchinja bila huruma.

3:44 Mao 2:1; Zek 7:13; Za 97:2; Isa 58:4Unajifunika mwenyewe kwa wingu,

ili pasiwe na ombi

litakaloweza kupenya.

3:45 1Kor 4:13Umetufanya takataka na uchafu

miongoni mwa mataifa.

3:46 Za 22:13; Mao 2:16“Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao

wazi dhidi yetu.

3:47 Yer 48:43; Isa 24:17-18; 51:19Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula,

uharibifu na maangamizi.”

3:48 Yer 9:1; Mao 2:18Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu,

kwa sababu watu wangu wameangamizwa.

Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,

bila kupata nafuu,

3:50 Za 14:2; 80:14; Isa 63:15hadi Bwana atazame chini

kutoka mbinguni na kuona.

Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini

kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.

3:52 Za 35:7; 69:4Wale waliokuwa adui zangu bila sababu

wameniwinda kama ndege.

3:53 Yer 38:6; 37:16; Dan 6:17Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo

na kunitupia mawe;

3:54 Za 69:2; Yon 2:3-5; Eze 37:11; Za 88:5maji yalifunika juu ya kichwa changu,

nami nikafikiri nilikuwa karibu

kukatiliwa mbali.

3:55 Za 130:1; 2Nya 33:12; Yon 2:2; Za 18:5, 6Nililiitia jina lako, Ee Bwana,

kutoka vina vya shimo.

3:56 Rum 8:26; Za 116:1-2; 6:8Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako

kilio changu nikuombapo msaada.”

3:57 Isa 41:10; Yak 4:8; Za 46:1; 69:18; Isa 58:9Ulikuja karibu nilipokuita,

nawe ukasema, “Usiogope.”

3:58 Yer 51:36; Za 34:22; Yer 50:34; 1Sam 25:39Ee Bwana, ulichukua shauri langu,

ukaukomboa uhai wangu.

3:59 Yer 18:19; Za 35:23Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa.

Tetea shauri langu!

3:60 Yer 11:20; 18:18Umeona kina cha kisasi chao,

mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.

Ee Bwana, umesikia matukano yao,

mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:

3:62 Eze 36:3kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia

dhidi yangu mchana kutwa.

3:63 Ay 30:9; Za 139:2Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama,

wananidhihaki katika nyimbo zao.

3:64 Za 28:4; Yer 51:6; 2Tim 4:14; Yer 11:20; Ufu 6:10Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana,

kwa yale ambayo mikono yao imetenda.

3:65 Kut 14:8; Kum 2:30; Isa 6:10; Za 8:3Weka pazia juu ya mioyo yao,

laana yako na iwe juu yao!

Wafuatilie katika hasira na uwaangamize

kutoka chini ya mbingu za Bwana.

Read More of Maombolezo 3

Maombolezo 4:1-22

4 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 4:1 Eze 7:19Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake,

dhahabu iliyo safi haingʼai!

Vito vya thamani vimetawanywa

kwenye mwanzo wa kila barabara.

4:2 Isa 51:18; 2Kor 4:7Wana wa Sayuni wenye thamani,

ambao mwanzo uzito wa thamani yao

ulikuwa wa dhahabu,

sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo,

kazi ya mikono ya mfinyanzi!

4:3 Ay 39:14-16Hata mbweha hutoa matiti yao

kunyonyesha watoto wao,

lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma

kama mbuni jangwani.

4:4 Mao 2:11-12; Za 22:15; 2Fal 18:31; Kum 28:48Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga

umegandamana na kaakaa la kinywa chake,

watoto huomba mkate,

lakini hakuna yeyote awapaye.

4:5 Yer 6:2; Isa 3:26; Amo 6:3-7; Ay 24:8; Lk 15:16Wale waliokula vyakula vya kifahari

ni maskini barabarani.

Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau

sasa wanalalia majivu.

4:6 Mwa 19:25Adhabu ya watu wangu

ni kubwa kuliko ile ya Sodoma,

ambayo ilipinduliwa ghafula

bila kuwepo mkono wa msaada.

Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji

na weupe kuliko maziwa,

miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani,

kuonekana kwao kama yakuti samawi.

4:8 Ay 30:28; Za 102:3-5; Mao 3:4Lakini sasa ni weusi kuliko masizi;

hawatambulikani barabarani.

Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao,

imekuwa mikavu kama fimbo.

4:9 Yer 15:2; 16:4; 2Fal 25:3; Mao 5:10Wale waliouawa kwa upanga ni bora

kuliko wale wanaokufa njaa;

wanateseka kwa njaa, wanatokomea

kwa kukosa chakula kutoka shambani.

4:10 Mao 2:20; Law 26:29; Kum 28:53-57; Eze 5:10; Yer 19:9Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma

wanapika watoto wao wenyewe,

waliokuwa chakula chao

watu wangu walipoangamizwa.

4:11 Yer 17:27; Kum 32:22; Yer 7:20; Ay 20:23; 2Nya 34:21; Eze 22:31Bwana ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake;

ameimwaga hasira yake kali.

Amewasha moto katika Sayuni

ambao umeteketeza misingi yake.

4:12 1Fal 9:9; Yer 21:13; Kum 29:24Wafalme wa dunia hawakuamini,

wala mtu yeyote wa duniani,

kwamba adui na watesi wangeweza kuingia

kwenye malango ya Yerusalemu.

4:13 Yer 5:31; Eze 22:28; Mik 3:11; 2Fal 21:16; Mt 23:31Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake,

na maovu ya makuhani wake,

waliomwaga ndani yake

damu ya wenye haki.

4:14 Isa 59:10; Yer 2:34; 19:4Sasa wanapapasa papasa barabarani

kama watu ambao ni vipofu.

Wamenajisiwa kabisa kwa damu,

hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao.

4:15 Yer 44:14; Law 13:46; Mik 2:10Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi!

Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!”

Wanapokimbia na kutangatanga huku na huko,

watu miongoni mwa mataifa wanasema,

“Hawawezi kukaa hapa zaidi.”

4:16 Isa 9:14-16; Mao 5:12Bwana mwenyewe amewatawanya;

hawaangalii tena.

Makuhani hawaonyeshwi heshima,

wazee hawakubaliki.

4:17 Mwa 15:18; Eze 29:16; Yer 37:7; Isa 20:5-6; 2Fal 24:7Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka,

kwa kutazamia bure msaada;

tuliangalia kutoka minara yetu

kwa taifa lisiloweza kutuokoa.

4:18 Eze 7:2-12; Amo 8:2; Yer 51:33; 2Fal 25:4; Yer 51:33Watu walituvizia katika kila hatua

hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu.

Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia,

kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika.

4:19 Kum 28:49; Law 26:36; Isa 5:26-28; Yer 52:7Waliotufuatia walikuwa wepesi

kuliko tai angani;

walitusaka juu milimani

na kutuvizia jangwani.

4:20 1Sam 26:9; 2Sam 19:21; Yer 39:5; Eze 19:4-8; 12:12-13; Mwa 2:7; Yer 52:9Mpakwa mafuta wa Bwana, pumzi ya uhai wetu hasa,

alinaswa katika mitego yao.

Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake

tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.

4:21 Za 16:5; Yer 25:15; Eze 35:15; Hab 2:16; Mwa 10:23; Isa 34:6-10; Amu 1:11Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu,

wewe unayeishi nchi ya Usi.

Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa,

Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.

4:22 Isa 40:2; Yer 33:8; Eze 25:12-14; Mal 1:4; Za 137:7Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha,

hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni.

Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako,

na atafunua uovu wako.

Read More of Maombolezo 4

Maombolezo 5:1-22

5:1 Za 44:13-16; 89:50Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata,

tazama, nawe uione aibu yetu.

5:2 Za 79:1; Sef 1:13; Yer 17:4Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni,

na nyumba zetu kwa wageni.

5:3 Kut 22:24; Yer 15:8; 18:21Tumekuwa yatima wasio na baba,

mama zetu wamekuwa kama wajane.

5:4 Isa 55:1; Eze 4:16-17; Isa 3:1Ni lazima tununue maji tunayokunywa,

kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.

5:5 Isa 47:6; Neh 9:37; Yos 1:13Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu,

tumechoka na hakuna pumziko.

5:6 Yer 2:36; Mwa 24:2; Hos 5:13; 7:11; Yer 50:15; Hos 12:1Tumejitolea kwa Misri na Ashuru

tupate chakula cha kutosha.

5:7 Yer 14:20; 16:12; Eze 8:2; Yer 31:29; Eze 18:2; Mt 23:32Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena,

na sisi tunachukua adhabu yao.

5:8 Neh 5:15; Zek 11:6Watumwa wanatutawala

na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.

Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu

kwa sababu ya upanga jangwani.

5:10 Ay 30:30; Mao 4:8-9Ngozi yetu ina joto kama tanuru,

kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.

5:11 Mwa 34:29; Zek 14:2; Isa 13:16Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni,

na mabikira katika miji ya Yuda.

Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao,

wazee hawapewi heshima.

5:13 Amu 13:16; 16:21Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia,

wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.

5:14 Isa 24:8; Yer 7:34; 2Fal 25:18Wazee wameondoka langoni la mji,

vijana wameacha kuimba nyimbo zao.

5:15 Amu 8:10; Yer 25:10Furaha imeondoka mioyoni mwetu,

kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.

5:16 Yer 13:18; 14:20; Za 89:39; Ay 19:9; Isa 3:11Taji imeanguka kutoka kichwani petu.

Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!

5:17 Ay 17:7; Za 6:7; 16:8; Yer 8:18Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia,

kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,

5:18 Isa 27:10; Mik 3:12; Za 74:2-4kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa,

nao mbweha wanatembea juu yake.

5:19 1Nya 16:31; Za 45:6; 102:22-27Wewe, Ee Bwana unatawala milele,

kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.

5:20 Za 13:1; 44:24; 71:11Kwa nini watusahau siku zote?

Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?

5:21 Isa 60:20-22; Za 80:3Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana,

ili tupate kurudi.

Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,

5:22 Isa 64:9; Yer 6:30; Za 53:5; 60:12isipokuwa uwe umetukataa kabisa

na umetukasirikia pasipo kipimo.

Read More of Maombolezo 5