Maombolezo 2:7-22, Maombolezo 3:1-39 NEN

Maombolezo 2:7-22

2:7 Eze 7:1-2; Isa 64:10-11; Yer 7:12-14; Law 26:31; Yer 33:4-5; 52:13; Za 78:59-61; Mik 3:12; Yer 7:12-14; Mt 24:2Bwana amekataa madhabahu yake

na kuacha mahali patakatifu pake.

Amemkabidhi adui kuta

za majumba yake ya kifalme;

wamepiga kelele katika nyumba ya Bwana

kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.

2:8 2Fal 21:13; Isa 34:11; 3:26; Yer 39:8; Za 48:13; Amu 7:7Bwana alikusudia kuangusha

ukuta uliomzunguka Binti Sayuni.

Ameinyoosha kamba ya kupimia

na hakuuzuia mkono wake usiangamize.

Alifanya maboma na kuta ziomboleze,

vyote vikaharibika pamoja.

2:9 Yer 16:13; Amo 8:11-12; Hos 3:4; 2Nya 15:3; Yer 14:14; Isa 45:2; 2Fal 24:15; Kum 28:36; 2Fal 25:7; Za 74:9; Mik 3:6, 7Malango yake yamezama ardhini,

makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu.

Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishoni

miongoni mwa mataifa,

sheria haipo tena,

na manabii wake hawapati tena

maono kutoka kwa Bwana.

2:10 Ay 2:12-13; Isa 3:24, 26; Eze 27:30-31; Isa 15:3; Mao 3:28; 4:5; Isa 47:1-5Wazee wa Binti Sayuni

wanaketi chini kimya,

wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao

na kuvaa nguo za gunia.

Wanawali wa Yerusalemu

wamesujudu hadi ardhini.

2:11 Isa 15:3; Ay 30:27; Za 22:14; Ay 16:13; Mao 3:48-51; Za 119:82; 6:7Macho yangu yamedhoofika kwa kulia,

nina maumivu makali ndani,

moyo wangu umemiminwa ardhini

kwa sababu watu wangu wameangamizwa,

kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimia

kwenye barabara za mji.

Wanawaambia mama zao,

“Wapi mkate na divai?”

wazimiapo kama watu waliojeruhiwa

katika barabara za mji,

maisha yao yadhoofikavyo

mikononi mwa mama zao.

2:13 Isa 37:22; Yer 14:17; 30:12-15; Dan 9:12; 2Fal 19:2; Ay 5:1Ninaweza kusema nini kwa ajili yako?

Nikulinganishe na nini,

ee Binti Yerusalemu?

Nitakufananisha na nini,

ili nipate kukufariji,

ee Bikira Binti Sayuni?

Jeraha lako lina kina kama bahari.

Ni nani awezaye kukuponya?

2:14 Isa 58:1; Yer 8:11; 20:6; Eze 13:3; Yer 28:3; 28:15; Eze 22:28Maono ya manabii wako

yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu,

hawakuifunua dhambi yako

ili kukuzuilia kwenda utumwani.

Maneno waliyokupa

yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.

2:15 Hes 24:20; Eze 25:6; Nah 3:19; Za 45:11; Eze 16:14; Za 48:2; Yer 19:8; 1Fal 9:8Wote wapitiao njia yako

wanakupigia makofi,

wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyao

kwa Binti Yerusalemu:

“Huu ndio ule mji ulioitwa

mkamilifu wa uzuri,

furaha ya dunia yote?”

2:16 Za 22:13; 56:2; Ay 16:19; Za 35:25; Eze 36:3; Mao 3:46Adui zako wote wanapanua

vinywa vyao dhidi yako,

wanadhihaki na kusaga meno yao

na kusema, “Tumemmeza.

Hii ndiyo siku tuliyoingojea,

tumeishi na kuiona.”

2:17 Kum 28:15-45; Eze 8:18; Isa 44:26; Mao 1:5; Law 26:16; Za 38:16Bwana amefanya lile alilolipanga;

ametimiza neno lake

aliloliamuru siku za kale.

Amekuangusha bila huruma,

amewaacha adui wakusimange,

ametukuza pembe ya adui yako.

2:18 Za 119:145; Mao 1:16; 3:19; Yer 9:1; 14:7Mioyo ya watu

inamlilia Bwana.

Ee ukuta wa Binti Sayuni,

machozi yako na yatiririke kama mto

usiku na mchana;

usijipe nafuu,

macho yako yasipumzike.

2:19 Mk 13:35; 1Sam 1:15; Za 62:8; Isa 51:20; Neh 3:10; Isa 26:9; Mao 4:1Inuka, lia usiku,

zamu za usiku zianzapo;

mimina moyo wako kama maji

mbele za Bwana.

Mwinulie yeye mikono yako

kwa ajili ya maisha ya watoto wako,

ambao wanazimia kwa njaa

kwenye kila mwanzo wa barabara.

2:20 Kum 28:53; Eze 5:10; Mao 4:10; Yer 23:11-12; 19:9; Za 78:64; Yer 14:15; Kut 32:11; Law 26:29“Tazama, Ee Bwana, ufikirie:

Ni nani ambaye umepata

kumtendea namna hii?

Je, wanawake wakule wazao wao,

watoto waliowalea?

Je, kuhani na nabii auawe

mahali patakatifu pa Bwana?

2:21 Kum 32:25; 2Nya 36:17; Yer 13:14; Zek 11:6“Vijana na wazee hujilaza pamoja

katika mavumbi ya barabarani,

wavulana wangu na wasichana

wameanguka kwa upanga.

Umewaua katika siku ya hasira yako,

umewachinja bila huruma.

2:22 Za 31:13; Yer 6:25; Ay 27:14; Hes 9:13; Yer 20:10“Kama ulivyoita siku ya karamu,

ndivyo ulivyoagiza hofu kuu

dhidi yangu kila upande.

Katika siku ya hasira ya Bwana

hakuna yeyote aliyekwepa au kupona;

wale niliowatunza na kuwalea,

adui yangu amewaangamiza.”

Read More of Maombolezo 2

Maombolezo 3:1-39

3 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 3:1 Ay 19:21; Za 88:7; Yer 15:17-18Mimi ndiye mtu aliyeona mateso

kwa fimbo ya ghadhabu yake.

3:2 Ay 19:8; Za 82:5; Yer 4:23Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee

gizani wala si katika nuru;

3:3 Isa 5:25; Za 38:2hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu

tena na tena, mchana kutwa.

3:4 Za 51:8; Isa 38:13; Yer 50:17; Ay 30:30; Mao 4:8Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa

na ameivunja mifupa yangu.

3:5 Yer 23:15Amenizingira na kunizunguka

kwa uchungu na taabu.

3:6 Isa 59:10; Za 143:3; 88:5-6Amenifanya niishi gizani

kama wale waliokufa.

3:7 Ay 3:23; Yer 40:4Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka,

amenifunga kwa minyororo mizito.

3:8 Kum 1:45; Ay 30:20; Za 22:2; 5:2Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada,

anakataa kupokea maombi yangu.

3:9 Ay 9:24; Hos 2:6; Isa 63:17Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe,

amepotosha njia zangu.

3:10 Ay 10:16; Hos 13:8; Amo 5:18-19Kama dubu aviziaye,

kama simba mafichoni,

ameniburuta kutoka njia,

akanirarua na kuniacha bila msaada.

3:12 Mao 2:4; Ay 16:12; Za 38:2; 34:2Amevuta upinde wake

na kunifanya mimi niwe lengo

kwa ajili ya mishale yake.

Alinichoma moyo wangu kwa mishale

iliyotoka kwenye podo lake.

3:14 Mwa 38:23; Za 22:6-7; Ay 30:9; Neh 4:2-4; Mt 27:29-31; Yer 20:7Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,

wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.

3:15 Yer 9:15Amenijaza kwa majani machungu

na kunishibisha kwa nyongo.

3:16 Mit 20:17Amevunja meno yangu kwa changarawe,

amenikanyagia mavumbini.

Amani yangu imeondolewa,

nimesahau kufanikiwa ni nini.

3:18 Ay 17:15; Za 31:22Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka

na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”

Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,

uchungu na nyongo.

3:20 Za 42:5; 43:5Ninayakumbuka vyema,

nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.

Hata hivyo najikumbusha neno hili

na kwa hiyo ninalo tumaini.

3:22 Za 130:7; Mt 3:6; Neh 9:31; Ay 34:15; Za 130:1; Hos 11:9; Za 78:38; 57:10; Mal 3:6Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

3:23 Kut 34:6; Isa 33:2; Ebr 10:23Ni mpya kila asubuhi,

uaminifu wako ni mkuu.

3:24 Za 16:5Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,

kwa hiyo nitamngojea.”

3:25 Za 33:18; Isa 25:9; 30:18; Za 130:6Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,

kwa yule ambaye humtafuta;

3:26 Za 37:7ni vyema kungojea kwa utulivu

kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

3:27 Za 90:12Ni vyema mtu kuchukua nira

bado angali kijana.

3:28 Yer 15:17Na akae peke yake awe kimya,

kwa maana Bwana ameiweka juu yake.

3:29 Yer 31:17; Ay 2:8; 42:6Na azike uso wake mavumbini

bado panawezekana kuwa na matumaini.

3:30 Ay 16:10; Isa 50:6; Mik 5:1; Mt 5:39Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,

na ajazwe na aibu.

3:31 Za 94:14; Isa 54:7Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali

na Bwana milele.

3:32 Za 106:43-45; Nah 1:12; Hos 11:8Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma,

kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.

3:33 Ay 37:23; Ebr 12:10; Yer 31:20; Eze 18:23Kwa maana hapendi kuwaletea mateso

au huzuni watoto wa wanadamu.

Kuwaponda chini ya nyayo

wafungwa wote katika nchi,

3:35 Mwa 14:18-22Kumnyima mtu haki zake

mbele za Aliye Juu Sana,

3:36 Za 140:12; Mit 17:15; Hab 1:13; Yer 22:3kumnyima mtu haki:

Je, Bwana asione mambo kama haya?

3:37 Mit 19:21; Za 33:9-11; Mit 21:30Nani awezaye kusema nalo likatendeka

kama Bwana hajaamuru?

3:38 Ay 2:10; Isa 45:7; Yer 32:42Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana

ndiko yatokako maafa na mambo mema?

3:39 Yer 30:15; Mik 7:9Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika

wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?

Read More of Maombolezo 3