Waamuzi 4:1-24, Waamuzi 5:1-31 NEN

Waamuzi 4:1-24

Debora

4:1 Amu 3:15; 2:11; 2:19Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni pa Bwana. 4:2 Kum 32:30; Yos 11:1; 1Sam 12:9; Za 83:9Hivyo Bwana akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu4:2 Haroshethi-Hagoyimu ina maana Haroshethi ya Mataifa. 4:3 Yos 17:16; Amu 10:12; Za 106:42; Amu 1:19Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma yapatayo 900, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli wakamlilia Bwana wakaomba msaada.

4:4 Amu 5:1, 7, 12; Kut 15:20Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye alikuwa anaamua Israeli wakati ule. 4:5 1Sam 14:2; 22; 6; Yos 18:25; 12:5-9; Mwa 35:8Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue. 4:6 Amu 5:12-15; 1Sam 12:11; Ebr 11:32; Yos 12:22; Mwa 30:8; Amu 5:18; 6:35; Yos 19:22Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “Bwana, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume 10,000 toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori. 4:7 Yos 11:1; Amu 5:12; 1Fal 18:40; Za 83:9; Amu 1:2Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ ”

Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitakwenda, lakini usipokwenda pamoja nami, sitakwenda.”

4:9 Yos 12:22; Amu 2:14Debora akamwambia, “Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Bwana atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi, 4:10 2Nya 36:23; Ezr 1:2; Isa 41:2; 42:6; 45:3; 46:11; 48:15mahali ambapo Baraka aliwaita Zabuloni na Naftali. Watu 10,000 wakamfuata Baraka, na Debora pia akaenda pamoja naye.

4:11 Mwa 15:19; Hes 10:29; Yos 24:26; Amu 9:6; Yos 19:33Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni wengine, yaani, wazao wa Hobabu, mkwewe Mose, naye akapiga hema lake karibu na ule mti mkubwa wa mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.

4:12 Yos 19:22Sisera alipoambiwa kuwa Baraka mwana wa Abinoamu alikuwa amepanda Mlima Tabori, 4:13 Yos 17:16; Amu 4:7; 5:19Sisera akakusanya pamoja magari yake yote 600 ya chuma na watu wote waliokuwa pamoja naye, kuanzia Haroshethi-Hagoyimu mpaka Mto wa Kishoni.

4:14 Amu 1:2; Kum 9:3; 1Sam 8:20; 2Sam 5:24; Za 68:7Ndipo Debora akamwambia Baraka, “Nenda! Hii ndiyo siku ambayo Bwana amemtia Sisera mikononi mwako. Je, Bwana hakukutangulia mbele yako?” Hivyo Baraka akashuka kutoka Mlima Tabori, akifuatwa na watu 10,000. 4:15 Kut 14:24; Za 18:14; Kut 14:28; Za 83:9-10Bwana akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, pamoja na jeshi lake lote kwa upanga mbele ya Baraka, naye Sisera akaliacha gari lake na kukimbia kwa miguu. 4:16 Kut 14:28; Za 83:9-10Lakini Baraka akafuata magari pamoja na jeshi mpaka Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia.

4:17 Amu 5:6, 24; Mwa 15:19; Yos 11; 1Sisera, hata hivyo, akakimbia kwa miguu mpaka kwenye hema la Yaeli, mkewe Heberi, Mkeni, kwa sababu palikuwa na uhusiano wa kirafiki kati ya Yabini mfalme wa Hazori na ukoo wa Heberi, Mkeni.

Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema ya Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene.

4:19 Mwa 18:8; Amu 5:25Akamwambia, “Nina kiu, tafadhali nipe maji ya kunywa.” Ndipo akafungua kiriba cha maziwa na kumpa akanywa, kisha akamfunika.

Naye Sisera akamwambia, “Simama mlangoni pa hema na mtu yeyote akija na kukuuliza, ‘Je, kuna mtu yeyote hapa?’ sema, ‘Hapana.’ ”

4:21 Mwa 2:21; 15:12; 1Sam 26:12; Isa 29:10; Yon 1:5; Amu 5:26Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi, akiwa amechoka. Akakigongomea kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa.

4:22 Amu 5:27Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema wakiwa wamefuatana na tazama Sisera alikuwa amelala humo, akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimegongomewa kupitia paji la uso wake.

4:23 Neh 9:24; Za 18:47; 44:2; 47:3; 144:2; Yos 11; 1Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli. 4:24 Za 83:9; 106:43Nao mkono wa Waisraeli ukaendelea kuwa na nguvu zaidi na zaidi dhidi ya Yabini, mfalme wa Kanaani, mpaka wakamwangamiza.

Read More of Waamuzi 4

Waamuzi 5:1-31

Wimbo Wa Debora

5:1 Amu 4:4, 6; Kut 15:1; Za 32:7Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:

5:2 2Nya 17:16; Za 110:3“Wakuu katika Israeli wanapoongoza,

wakati watu wanapojitoa

kwa hiari yao wenyewe:

mhimidini Bwana!

5:3 Kut 15:1; Za 27; 6“Sikieni hili, enyi wafalme!

Sikilizeni, enyi watawala!

Nitamwimbia Bwana, nitaimba;

kwa wimbo nitamhimidi Bwana,

Mungu wa Israeli.

5:4 Kut 13:21; Hes 24:18; Kut 33:2; 2Sam 22:8; Za 18:7; 77:18; 82:5; Isa 2:19-21; 64:3; Yer 10; 10; 50:46; 51:29; Yoe 3:16; Nah 1:5; Hab 3:6; Za 68:8; 77:17“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri,

ulipopita katika mashamba ya Edomu,

nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga,

naam, mawingu yakamwaga maji.

5:5 Kut 19:18; Za 29:6; 46:3; 77:18; 114:4; Isa 64:3Milima ilitetemeka mbele za Bwana,

hata ule wa Sinai,

mbele za Bwana,

Mungu wa Israeli.

5:6 Amu 3:31; 4:17; Law 26:22; Isa 33:8; Za 125:5; Isa 59:8“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi,

katika siku za Yaeli,

barabara kuu hazikuwa na watu;

wasafiri walipita njia za kando.

5:7 Amu 4:4Mashujaa walikoma katika Israeli,

walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka,

nilipoinuka kama mama katika Israeli.

5:8 Kum 32:17; Amu 2:13; Yos 2:5; Hes 25:7Walipochagua miungu migeni,

vita vilikuja katika malango ya mji,

hapakuonekana ngao wala mkuki

miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.

Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli,

pamoja na wale wanaojitoa wenyewe

kwa hiari yao miongoni mwa watu.

Mhimidini Bwana!

5:10 Mwa 49:11; Amu 12:14; 10:4“Nanyi mpandao punda weupe,

mkiketi juu ya matandiko ya thamani,

nanyi mtembeao barabarani,

fikirini 5:11 1Sam 12:7; Dan 9:16; Mik 6:5juu ya sauti za waimbaji

mahali pa kunyweshea maji.

Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana,

matendo ya haki ya mashujaa wake

katika Israeli.

“Ndipo watu wa Bwana

walipoteremka malangoni pa mji.

5:12 Za 44:23; 57:8; Isa 51:9, 17; Amu 4:4-6; Za 68:18; Efe 4:8‘Amka, amka! Debora!

Amka, amka, uimbe!

Ee Baraka! Inuka,

chukua mateka wako uliowateka,

ee mwana wa Abinoamu.’

“Ndipo mabaki ya watu

wakashuka dhidi ya wenye nguvu,

watu wa Bwana,

wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.

5:14 Mwa 41:52; Amu 1:29; 3:13; Hes 34:21; Mwa 50:23Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;

Benyamini akiwa miongoni

mwa watu waliokufuata.

Kutoka Makiri wakashuka viongozi,

na kutoka Zabuloni wale washikao

fimbo ya jemadari.

5:15 Mwa 50:18; Amu 4:4-6Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;

naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,

wakija nyuma yake kwa mbio

wakielekea bondeni.

Katika jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

5:16 Mwa 49:11; Hes 32; 1Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo

kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi?

Kwa jamaa za Reubeni,

palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.

5:17 Yos 12:2; 17:7; 19:29Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani.

Naye Dani, kwa nini alikaa

kwenye merikebu siku nyingi?

Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari,

akikaa kwenye ghuba zake ndogo.

5:18 Mwa 30:20; 30:8; Za 68:27; Amu 9:6Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao,

vilevile nao watu wa Naftali.

5:19 Yos 11:5; Amu 4; 13; Ufu 16:16; Yos 12:21; Amu 1:27“Wafalme walikuja na kufanya vita;

wafalme wa Kanaani walipigana

huko Taanaki karibu na maji ya Megido,

lakini hawakuchukua fedha wala nyara.

5:20 Yos 10:11Kutoka mbinguni nyota zilipigana,

nyota kutoka njia zake

zilipigana na Sisera.

5:21 Amu 4:7; Yos 1:6Mto wa Kishoni uliwasomba,

ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.

Songa mbele, ee nafsi yangu,

kwa ujasiri!

5:22 Yer 8:16Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo:

farasi wake wenye nguvu

huenda mbio kwa kurukaruka.

Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe.

Walaaniwe watu wake kwa uchungu,

kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana,

kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’

5:24 Lk 1:42; Amu 4:17; Mwa 15:19“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote,

mkewe Heberi, Mkeni,

abarikiwe kuliko wanawake wote

waishio kwenye mahema.

5:25 Mwa 18:8; Amu 4:19Aliomba maji, naye akampa maziwa;

kwenye bakuli la heshima

akamletea maziwa mgando.

Akanyoosha mkono wake

akashika kigingi cha hema,

mkono wake wa kuume

ukashika nyundo ya fundi.

Akampiga Sisera kwa nyundo,

akamponda kichwa chake,

akamvunjavunja na kumtoboa

paji lake la uso.

Aliinama miguuni pa Yaeli,

akaanguka; akalala hapo.

Pale alipoinama miguuni pake,

alianguka;

pale alipoinamia, ndipo alipoanguka,

akiwa amekufa.

5:28 Yos 2:15; Mit 7:6“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia;

nyuma ya dirisha alilia, akasema,

‘Mbona gari lake linachelewa kufika?

Mbona vishindo vya magari yake

vimechelewa?’

Wanawake wenye busara

kuliko wengine wote wakamjibu;

naam, husema moyoni mwake,

5:30 Kut 15:9; 1Sam 30:24; Za 68:12; 45:14; Eze 16:10; 2Sam 1:24‘Je, hawapati na kugawanya nyara:

msichana mmoja au wawili kwa kila mtu,

mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara,

mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa,

mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu:

yote haya yakiwa nyara?’

5:31 Hes 10:35; 2Sam 23:4; Ay 37:21; Za 19:4; 89:36; Isa 18:4; 2Sam 18:32; Amu 3:11“Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana!

Bali wote wakupendao na wawe kama jua

lichomozavyo kwa nguvu zake.”

Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.

Read More of Waamuzi 5