Waamuzi 2:6-23, Waamuzi 3:1-31 NEN

Waamuzi 2:6-23

Kifo Cha Yoshua

Baada ya Yoshua kuwapa watu ruhusa waende zao, Waisraeli wakaenda kwenye urithi wao wenyewe ili kumiliki nchi yao. Watu wakamtumikia Bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, waliokuwa wameona mambo makuu ambayo Bwana alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli.

Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa akiwa na umri wa miaka 110. 2:9 Yos 19:50Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi2:9 Unajulikana pia kama Timnath-Sera, ona Yos 19:50; 24:30. katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima Gaashi.

2:10 1Nya 28:9; Kut 5:2; Gal 4:8Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua Bwana, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli. 2:11 1Fal 15:26; Amu 3:12; 4:1; 6:1; 3:7; 8:33; 1Fal 16:31; 22:53; 2Fal 10:18; 17:16Kwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Bwana na kuwatumikia Mabaali. 2:12 Kum 32:12; Za 106:36; Kum 31:16; Amu 10:6; Hes 11:33; Kum 4:25; Za 78:5, 8; 106:40Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yanayowazunguka. Wakamkasirisha Bwana, 2:13 1Sam 7:3; 1Fal 11:5, 33; 2Fal 23:13; Amu 3:7; 5:8; 6:25; 8:33; 10:6; 1Sam 31:10; Neh 9:26; Za 78:56; Yer 11:10kwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi. 2:14 Kum 31:17; Neh 9:27; Za 106:41; 44; 10; 89:41; Eze 34:8; Kum 32:30; Amu 3:8; Kum 28:25Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. 2:15 Rum 1:13; Ay 19:21; 5:5; 20:22; Za 32:4; Mwa 35:3; 2Sam 22:7; 2Nya 15:4; Za 18:6Popote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.

2:16 Rum 1; 1; 1Sam 4:18; 7:6, 15; 2Sam 7:11; 1Nya 17:10; Mdo 13:20; 1Sam 11:3; Za 106:43Ndipo Bwana akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa katika mikono ya hao watu waliowashambulia. 2:17 Kut 34:15; Hes 15:39; Za 4:2; Neh 9:26; Za 106:36; Kum 9:12Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao, bali walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine na kuiabudu. Waligeuka mara na kuiacha njia ambayo baba zao waliiendea, yaani, njia ya kutii amri za Bwana. 2:18 1Sam 7:3; 2Fal 13:5; Isa 19:20; 43:3, 11; 45:15, 21; 49:20; 60:16; 63:8; Hes 10:9; Kum 32:36; Kut 2:23Kila mara Bwana alipowainulia mwamuzi, Bwana alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa Bwana aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha. 2:19 Mwa 6:11; Kum 4:16; 32:17; Neh 9:2; Za 78:57; Yer 44:9; Amu 4:1; 8:33; Kut 32:9Lakini kila mara mwamuzi alipofariki, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi.

2:20 Kum 31:17; Yos 23:16; 7:11; 1Fal 17:15Kwa hiyo Bwana akawakasirikia sana Israeli na kusema, “Kwa kuwa taifa hili limevunja Agano lile nililofanya na baba zao na hawakunisikiliza, 2:21 Yos 23:5mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki. 2:22 Mwa 22:1; Kut 15:25Nitayatumia ili nipate kuwapima Israeli na kuona kama wataishika njia ya Bwana na kuenenda katika hiyo kama njia baba zao walivyofanya.” 2:23 Amu 1:1Bwana alikuwa ameyaacha hayo mataifa yabaki; hakuyaondoa mara moja kwa kuyatia mikononi mwa Yoshua.

Read More of Waamuzi 2

Waamuzi 3:1-31

Mataifa Yaliyobaki Katika Ile Nchi

3:1 Kut 15:25Haya ndiyo mataifa Bwana aliyoyaacha ili kuwajaribu Waisraeli wote ambao hawakujua vita vyovyote vya Kanaani (alifanya hivi ili tu kuwafundisha wazao wa Waisraeli ambao hawakuwa wamejua vita hapo awali): 3:3 Yos 13:2; Mwa 10:14; 10:17; Kut 3:8; Kum 3:8; Hes 13:21wafalme watano wa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, Wahivi waishio katika milima ya Lebanoni kuanzia Mlima wa Baal-Hermoni hadi Lebo-Hamathi. 3:4 Kut 12:25Waliachwa ili kuwajaribu Waisraeli kuona kama wangetii amri za Bwana, alizokuwa amewapa baba zao kwa mkono wa Mose.

3:5 Za 106:36; Yos 3:10; 11:3; Ezr 9:1Waisraeli wakaishi miongoni mwa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 3:6 Ezr 10:18; Neh 13:23; Mal 2:11; Kut 34:16; Kum 7:3-4, 16Wakawaoa binti zao, nao wakawatoa binti zao waolewe na wana wa hayo mataifa, na kuitumikia miungu yao.

Othnieli

3:7 Kum 4:9; 32:18; Amu 8:34; Za 78:11; 106:7; Yer 23:27; Amu 2:11-13; 1Fal 16:33; 2Nya 34:7; Isa 17:8Waisraeli wakafanya maovu machoni pa Bwana, wakamsahau Bwana Mungu wao na kutumikia Mabaali na Maashera. 3:8 Amu 2:14; Za 44:12; Isa 50:1; 52:3; Mwa 24:10Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli, hivyo akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu-Naharaimu3:8 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. ambaye Israeli walikuwa chini yake wakimtumikia kwa muda wa miaka minane. 3:9 Amu 6:6-7; 10:10; 1Sam 12:10; Za 106:44; 107:13; Kum 28:29; Neh 9:27Waisraeli walipomlilia Bwana, yeye akawainulia mwokozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa. 3:10 Hes 11:25; Amu 6:34; 11:29; 13:25; 14:6; 15:14; 1Sam 11:6; 16:13; 1Fal 18:46; 1Nya 12:18; 2Nya 24:20; Isa 11:2; Mwa 10:22Roho wa Bwana akaja juu yake, hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, akaenda vitani. Bwana akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Aramu mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda. 3:11 Yos 14:15; Amu 5:31; 8:28; Kut 16:35; 15:17Hivyo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arobaini, mpaka Othnieli mwana wa Kenazi alipofariki.

Ehudi

3:12 Amu 2:11; 1Sam 12:9Waisraeli wakafanya maovu mbele za Bwana tena, kwa kuwa walifanya maovu hayo Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu dhidi ya Israeli. 3:13 Mwa 19:38; Amu 10:11; Mwa 14:7; Amu 1:16Egloni akawataka Waamoni na Waamaleki waungane naye, akaja kuishambulia Israeli, nao wakatwaa Mji wa Mitende3:13 Yaani Yeriko. 3:14 Yer 48:1Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na minane.

3:15 Amu 1:4; 20:16; 1Nya 12:2; 2Sam 8:2-6; 1Fal 4:21; 2Fal 17:3; Es 10:1; Za 68:29; 72:10; 89:22; Mhu 2:8; Isa 60:5; Hos 10:6; Za 107:13Waisraeli wakamlilia tena Bwana, naye akawapa mwokozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera, Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja,3:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume. 3:17 Ay 15:27; Za 73:4Akamkabidhi ushuru Egloni mfalme wa Moabu, ambaye alikuwa mtu mnene sana. Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru aliwaruhusu waende zao. Yeye mwenyewe akafuatana nao hadi kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe karibu na Gilgali, ndipo yeye akarudi, akafika kwa Egloni na kusema, “Ee Mfalme, ninao ujumbe wa siri kwa ajili yako.”

Mfalme akasema, “Nyamazeni kimya!” Nao wale waliomhudumia wote wakamwacha, wakatoka nje.

3:20 Amo 3:15; Neh 8:5Ndipo Ehudi akamsogelea alipokuwa ameketi peke yake kwenye chumba cha juu cha jumba lake la kifalme la majira ya kiangazi, na kusema, “Ninao ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yako.” Mfalme alipokuwa anainuka kutoka kwenye kiti chake, 3:21 2Sam 2:16; 3:27; 20:10Ehudi akaunyoosha mkono wake wa kushoto na kuufuta ule upanga aliokuwa ameufunga kwenye paja lake la kulia, akamdunga Mfalme Egloni tumboni mwake. Hata mpini nao ukazama tumboni pamoja na upanga wenyewe, nao upanga ukatokea mgongoni mwake. Ehudi hakuuchomoa huo upanga, nayo mafuta yakashikamana juu ya upanga. Ehudi akatoka nje barazani; akamfungia milango ya chumba cha juu na kuifunga kwa funguo.

3:24 1Sam 24:3Baada ya kuondoka, watumishi wakaja na kukuta milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka amejipumzisha kwenye chumba cha ndani cha nyumba yake ya majira ya kiangazi.” 3:25 2Fal 2:17; 8:11Wakangoja hata wakawa na fadhaa, basi wakati hakufungua milango ya chumba, wakachukua funguo na kuifungua. Tazama wakaona bwana wao amelala sakafuni, amekufa.

Walipokuwa wangali wanangoja, Ehudi akatoroka, akapita hapo kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe na kukimbilia Seira. 3:27 Law 25:9; Amu 6:34; 7:18; 2Sam 2:28; Isa 18:3; Yer 42:14Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.

3:28 Mwa 19:37; Yos 2:24; Amu 1:2; Hes 13:29; Yos 2:9Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa Bwana amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakuacha mtu yeyote kuvuka. Wakati huo wakawaua Wamoabu watu waume wapatao 10,000 ambao wote walikuwa wenye nguvu na mashujaa; hakuna mtu yeyote aliyetoroka. 3:30 Mwa 36:35Siku ile Moabu wakashindwa na Israeli, nayo nchi ikawa na amani kwa miaka themanini.

Shamgari

3:31 Amu 5:6; Yos 23:10; 13:2; Amu 10:11; 13:1; 1Sam 5:1; 31:1; 2Sam 8:1; Yer 25:30; 47:1Baada ya Ehudi akaja Shamgari mwana wa Anathi, aliyewapiga Wafilisti 600 kwa fimbo iliyochongoka ya kuongozea ngʼombe. Naye pia akawaokoa Waisraeli.

Read More of Waamuzi 3