Waamuzi 14:1-20, Waamuzi 15:1-20 NEN

Waamuzi 14:1-20

Ndoa Ya Samsoni

14:1 Amu 13:24; Mwa 38:12Samsoni akateremkia Timna, akamwona mwanamke wa Kifilisti. 14:2 Mwa 21:21; 34:4Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipe ili awe mke wangu.”

14:3 Mwa 24:4; 34:14; 1Sam 14:6; Kut 34:16; Kum 7:3Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda kujitwalia mwanamke kutoka kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?”

Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza.” 14:4 Kum 2:30; Yos 11:20; Amu 13:1; 15:11(Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Bwana, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.) Samsoni akateremkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. 14:6 Amu 3:10; 1Sam 17:35; Amu 13:25Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono yake bila silaha yoyote kama vile mtu ampasuavyo mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake aliyoyafanya. Basi akateremka na kuongea na yule mwanamke, naye akampendeza Samsoni.

Baada ya muda aliporudi ili akamwoe, akatazama kando ili kuutazama mzoga wa yule simba, na tazama, kulikuwa na kundi la nyuki ndani ya ule mzoga wa simba na kulikuwa na asali; akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.

14:10 Mwa 29:2Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye.

14:12 Hes 12:8; Eze 17:2; 20:49; 24:3; Hos 12:10; Mwa 29:27; 45:22Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.”

Wakamwambia, “Tuambie hicho kitendawili, hebu na tukisikie.”

Akawaambia,

“Ndani ya mlaji,

kulitoka kitu cha kuliwa,

ndani ya mwenye nguvu,

kulitoka kitu kitamu.”

Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.

14:15 Amu 16:5; Mhu 7:26; Law 20:14-16; Amu 15:6Siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atueleze hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyangʼanya kile tulicho nacho?”

14:16 Amu 16:15Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.”

Samsoni akamwambia, “Wala sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?” 14:17 Es 1:5Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ile ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye akawaeleza watu wake kile kitendawili.

Siku ya saba kabla ya jua kutua, watu wa mji wakamwambia Samsoni,

“Ni nini kitamu kama asali?

Ni nini chenye nguvu kama simba?”

Samsoni akawaambia,

“Kama hamkulima na mtamba wangu,

hamngeweza kufumbua

kitendawili changu.”

14:19 Amu 3:10; 2Nya 24:20; Yos 13:3; Isa 11:2; 1Sam 11:6Ndipo Roho wa Bwana akamjia Samsoni kwa nguvu. Akateremka mpaka Ashkeloni, akawaua watu waume thelathini miongoni mwa watu wa mji, akatwaa mali zao na nguo zao, akawapa watu wale waliofumbua kile kitendawili. Akiwa na hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake. 14:20 Amu 15:2, 6; Yn 3:29Lakini huyo mke wa Samsoni akakabidhiwa kwa rafiki yake Samsoni ambaye alikuwa rafiki yake msaidizi siku ya arusi.

Read More of Waamuzi 14

Waamuzi 15:1-20

Kisasi Cha Samsoni Kwa Wafilisti

15:1 Mwa 30:14; Amu 13:24; Mwa 38:17; 29:21Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia.

15:2 Amu 14:20Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa kike si mzuri zaidi kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.”

Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” 15:4 Wim 2:15; Mwa 15:17Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga, 15:5 Mwa 15:17; Kut 22:6; 2Sam 14:30-31akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka zilizosimama, pamoja na mashamba ya mizabibu na viunga vya mizeituni.

15:6 Amu 14:20; Mwa 38:24; Amu 14:15Ndipo Wafilisti wakauliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, yule mkwewe Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe akampa mwenzake.”

Hivyo Wafilisti wakapanda wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake. Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia mpaka niwe nimelipiza kisasi juu yenu.” 15:8 Isa 2:21Akawashambulia kwa ukali kwa mapigo makuu na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa katika ufa kwenye mwamba wa Etamu.

Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”

Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.”

15:11 Amu 13:1; 14:4; Za 106:40-42Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”

Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.”

15:12 Mwa 47:31Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.”

Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”

15:13 Amu 16:11-12Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya. Wakamchukua toka huko kwenye ufa katika mwamba. 15:14 Amu 3:10; Yos 2:6; Amu 14:19; 1Sam 11:6Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15:15 Law 26:8; Yos 23:10Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao 1,000.

15:16 Yer 22:19Ndipo Samsoni akasema,

“Kwa taya la punda

malundo juu ya malundo.

Kwa taya la punda

nimeua watu 1,000.”

Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi.15:17 Ramath-Lehi maana yake Kilima cha Taya.

15:18 Amu 16:28; Kum 20:4Kwa kuwa alikuwa amesikia kiu sana, akamlilia Bwana akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?” 15:19 Mwa 45:27; 1Sam 30:12; Isa 40:29; Kut 17:6Bwana akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore,15:19 En-Hakore maana yake ni Chemchemi ya Aliyeita. nayo iko mpaka leo huko Lehi.

15:20 Amu 13:1; 16:31; Ebr 11:32Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.

Read More of Waamuzi 15