Yoshua 5:13-15, Yoshua 6:1-27, Yoshua 7:1-26 NEN

Yoshua 5:13-15

Jemadari Wa Jeshi La Bwana

5:13 Mwa 18:2; Hes 22:23; Mwa 32:24; Kut 23:23; Mdo 1:10; Zek 1:8Basi wakati Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?”

5:14 Mwa 17:3; 19:1; Dan 10:13; Ufu 2:17; Law 9:24; Hes 16:22Akajibu, “La, siko upande wowote, lakini mimi nimekuja nikiwa jemadari wa jeshi la Bwana.” Yoshua akaanguka kifudifudi hadi chini, akasujudu, akamuuliza, “Je, Bwana, una ujumbe gani kwa mtumishi wako?” 5:15 Mwa 28:17; Kut 3:5; Mdo 7:33; Kut 19:10-13; Za 22:3; 29:2; Isa 6:3; 1Nya 26:25-29; 1Sam 2:2Jemadari wa jeshi la Bwana akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.

Read More of Yoshua 5

Yoshua 6:1-27

Yeriko Yatekwa Na Kuangamizwa

6:1 Yos 24:11Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa ajili ya Waisraeli. Hakuna mtu yeyote aliyetoka au kuingia.

6:2 Kum 7:24; Yos 8:1; Amu 11:21; 2Sam 5:19; Neh 9:24; Dan 5:18-19Kisha Bwana akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. Zunguka mji mara moja pamoja na watu wote wenye silaha. Fanya hivi kwa siku sita. 6:4 Kut 19:13; Law 25:9; Hes 10:8; Amu 7:16Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo dume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 6:5 Kut 19:13; 1Sam 6:15; Ezr 3:11; 10:12; Za 42:4; 95:1; Isa 8:9; 42:13Utakapowasikia wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele.”

Ndipo Yoshua mwana wa Nuni akaita makuhani na kuwaambia, “Chukueni Sanduku la Agano la Bwana na makuhani saba wachukue baragumu za pembe za kondoo dume mbele yake.” 6:7 Kut 14:15; Hes 10:35; 1Sam 4:3; 7:1Naye akawaagiza watu, “Songeni mbele! Mkauzunguke mji, na walinzi wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku la Bwana.”

6:8 Yos 4:13Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele za Bwana, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la Bwana likawafuata. 6:9 Hes 2:31; Isa 52:12, 13; Hes 10:25; Isa 42:11-13Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa. 6:10 1Sam 4:5; Ezr 3:11Bali Yoshua alikuwa amewaagiza watu, “Msipige kelele ya vita, msipaze sauti zenu, wala kusema neno lolote mpaka siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!” Basi akalipeleka Sanduku la Bwana kuzungushwa huo mji, likizungushwa mara moja. Kisha watu wakarudi kambini kulala.

6:12 Kum 31:25Yoshua akaamka mapema asubuhi iliyofuata nao makuhani wakalichukua Sanduku la Bwana. 6:13 1Nya 15:26; Gal 6:9Wale Makuhani saba wakizibeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la Bwana wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la Bwana, huku baragumu hizo zikiendelea kulia. Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja na kurudi kambini. Wakafanya hivi kwa siku sita.

6:15 1Fal 18:44; 2Fal 4:35; 5:14Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba. 6:16 Amu 7:20; 2Nya 14:14Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipopiga baragumu kwa sauti kubwa, Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana Bwana amewapa mji huu! 6:17 Law 27:28; Kum 20:17; Isa 13:5; 24:1; 34:2-5; Mal 4:6; Yos 2:14; Mwa 13:3; 1Sam 15:6; Mt 10:41; 25:40; Ebr 6:10; 11:31; Yak 2:25Mji huu pamoja na vyote vilivyomo ndani yake utawekwa wakfu kwa Bwana. Ila Rahabu tu, yule kahaba na wote ambao wako pamoja naye nyumbani mwake ndio watakaosalimishwa, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma. 6:18 Yos 7:1, 12, 25, 26; 1Nya 2:7; Kum 7:26; 13:17; Isa 52:11; Rum 12:9; 2Kor 6:17; Efe 5:11; 1The 5:2; 1Fal 18:17, 18Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua chochote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu. 6:19 Hes 31:22Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Bwana, lazima viletwe katika hazina yake.”

6:20 Law 25:9; Amu 6:34; 7:22; 1Fal 1:41; Isa 18:3; Yer 4:21; 42:14; Amo 2:2; Ebr 11:30Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, na katika sauti ya baragumu, na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akapanda akiendelea mbele na kuuteka mji. 6:21 Kum 20:16; 1Sam 15:3, 8; 1Fal 20:42; Yer 48:18; Ufu 18:21Wakauweka mji wakfu kwa Bwana, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ngʼombe, kondoo na punda.

6:22 Mwa 42:9; Yos 2:4; Hes 21:32; Yos 2:14; Ebr 11:30-31Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.” 6:23 Yos 2:13Basi wale vijana waliofanya upelelezi wakaenda kumleta Rahabu, baba yake na mama yake, na ndugu zake na watu wote waliokuwa pamoja naye. Wakaleta jamaa yake yote na kuwaweka mahali nje ya kambi ya Israeli.

6:24 Hes 31:10; Kum 13:16Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya Bwana. 6:25 Amu 1:25; Yos 2:1; 2:1, 6; Ebr 11:31Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu yule kahaba, jamaa yake yote na wote waliokuwa wa kwake, kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko, naye anaishi miongoni mwa Waisraeli hata leo.

6:26 1Sam 14:24; Hes 5:21; 1Fal 16:34Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Aliyelaaniwa mbele za Bwana ni mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko:

“Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume

ataiweka misingi yake;

kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho

atayaweka malango yake.”

6:27 Mwa 39:2; Hes 14:43; Yos 9:1; 1Nya 14:17; Amu 1:9; 2Sam 7:9; Rum 8:31; 1Sam 2:30Hivyo Bwana alikuwa pamoja na Yoshua, na sifa zake zikaenea katika nchi yote.

Read More of Yoshua 6

Yoshua 7:1-26

Dhambi Ya Akani

7:1 Yos 6:18; 1Nya 2:7; Yos 22:20; Hes 1:4; Kut 4:14; 32:20; Law 10:6Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyowekwa wakfu; Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli.

7:2 Mwa 12:8; Yos 8:1, 28; 18:12; 1Sam 14:23; Hos 4:15; 5:8; 10:5; Mwa 12:8; Yos 12:16; 16:1; Amu 1:22; 1Sam 30:27; 2Fal 23:15; Yer 48:13; Amo 3:14; 4:4; 5:5-6; 7:10, 13; Hes 21:32Basi Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko waende Ai, karibu na Beth-Aveni mashariki ya Betheli, akawaambia, “Pandeni mkaipeleleze nchi.” Basi wale watu wakapanda wakaipeleleza Ai.

Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Usiwachoshe watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.” 7:4 Law 26:17; Kum 28:25; 32:30; Isa 30:17; 59:2Basi wakapanda kama watu elfu tatu tu, lakini wakashambuliwa na watu wa Ai, 7:5 Yos 22:20; Mwa 42:28; Za 22; 14; Isa 13:7; Eze 21:7; Nah 2:10; Law 26:36ambao waliwaua watu kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawauwa huko kwenye materemko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka ikawa kama maji.

7:6 Mwa 37:29; 17:3; 1Nya 21:16; Eze 9:8; Amu 20:23; Yos 8:10; 9:11; 20:4; 23:2; 1Sam 4:12; 2Sam 13:19; 15:32; Neh 9:1; Ay 2:12; Eze 27:30; Ufu 18:19Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana, na akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo wakatia mavumbi vichwani mwao. 7:7 1Sam 4:3; Kut 5:22; Hes 14:16; 2Fal 3:10Yoshua akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, kwa nini umewavusha watu hawa ngʼambo ya Yordani ili kututia mikononi mwa Waamori watuangamize? Laiti tungeliridhika kukaa ngʼambo ile nyingine ya Yordani! Ee Bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? 7:9 Kut 32:12; Kum 9:28; 28:58; 1Sam 12:22; Za 48:10; 106:8; Yer 14:21Wakanaani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenyewe lililo kuu?”

Bwana akamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini hapo chini kifudifudi? 7:11 Kut 9:27; Kum 29:27; Yos 24:16-27; 2Fal 17:7; Hos 10:9; Yos 6:17-19; 23:16; Amu 2:20; 1Sam 15:24; Za 78:10; Mdo 5:1-2Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao. 7:12 Law 26:37; Za 18:40; 21:12; Law 26:17; Yos 6:18; Za 44:9; 60:10Ndiyo sababu Waisraeli hawawezi kusimama dhidi ya adui zao. Wanawapa visogo na kukimbia kwa kuwa wanastahili maangamizi. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka mwangamize kila kitu miongoni mwenu kilichotengwa kwa maangamizi.

7:13 Law 11:44; Yos 3:5; Kut 19:10“Nenda, ukawatakase watu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.

7:14 1Sam 10:19; Mit 16:33; 1Sam 14:41-42; Yn 1:7; Mdo 1:24-26“ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa Bwana litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaoutwaa Bwana utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakuja mbele mtu kwa mtu. 7:15 Yos 6:18; Kum 7:25; 2Fal 25:9; 1Nya 14:12; Isa 37:19; Yer 43:12; Eze 30:16; 1Sam 14:39; Mwa 34:7Yule atakayekutwa na vitu vilivyowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, pamoja na vitu vyote alivyo navyo. Kwa kuwa amelivunja agano la Bwana na kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ”

Kesho yake asubuhi na mapema Yoshua akawaamuru Israeli kuja mbele kabila kwa kabila; na Yuda akatwaliwa. 7:17 Hes 26:20Koo za Yuda zikaja mbele, naye akawatwaa Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ya Zabdi ikatwaliwa. 7:18 Yos 7:1; Law 24:11; Yn 1:7; Mdo 5:1-10; Yer 2:26; Mit 13:21; Hes 32:23; Mwa 4:7Yoshua akaamuru watu wa jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu kwa mtu, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akatwaliwa.

7:19 Kut 14:17; 1Sam 6:5; Za 96:8; Isa 42:12; Yer 13:16; Yn 9:24; Law 5:5; 1Sam 14:43Ndipo Yoshua akamwambia Akani, “Mwanangu, mtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, nawe ukiri kwake. Niambie ni nini ulichotenda; usinifiche.”

Akani akamjibu Yoshua, “Ni kweli! Nimetenda dhambi dhidi ya Bwana, Mungu wa Israeli. Hili ndilo nililofanya: 7:21 Mwa 34:29; 49:27; Kum 7:25; Efe 5:5; 1Tim 6:10; Kut 20:17; 1Fal 21:1; 2Fal 5:20-27; Mit 15:27; Hab 2:9; Lk 12:15; Rum 7:7, 8Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili7:21 Shekeli 200 za fedha ni sawa na kilo 2.3. za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini,7:21 Shekeli 50 ni sawa na gramu 600. nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”

Kwa hiyo Yoshua akatuma wajumbe, nao wakapiga mbio mpaka hemani, tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, pamoja na ile fedha chini yake. Wakavichukua vile vitu toka mle hemani, wakamletea Yoshua pamoja na Waisraeli wote, na wakavitandaza mbele za Bwana.

7:24 Hes 16:27; Yos 7:26; 15:7; Isa 65:10; Hos 2:15Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ngʼombe, punda na kondoo wake, hema yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori. 7:25 Yos 6:18; Law 20:2; Kum 17:5; 1Fal 12:18; 2Nya 10:18; 24:21; Neh 9:26; Mwa 38:24; 1Nya 2:7; Gal 5:12Yoshua akasema, “Kwa nini umeleta taabu hii juu yetu? Bwana ataleta taabu juu yako leo hii.”

Ndipo Israeli yote ikampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto. 7:26 2Sam 18:17; Mwa 35:20; Hes 25:4; Kum 13:17; Isa 65:10; Hos 2:15; Yos 8:29; 2Sam 18:17; Mao 3:53; Kum 13:17; 2Sam 21:14Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo mpaka leo. Naye Bwana akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori7:26 Akori yamaanisha taabu. tangu siku hiyo.

Read More of Yoshua 7