Yoshua 3:1-17, Yoshua 4:1-24, Yoshua 5:1-12 NEN

Yoshua 3:1-17

Kuvuka Yordani

3:1 Yos 2:1; Mwa 13:10; Ay 40:23; Hes 25:1; 33:49Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda mpaka Mto Yordani, ambako walipiga kambi kabla ya kuvuka. 3:2 Mwa 40:13; Yos 2:16; Kum 1:16; Yos 1:11Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote, 3:3 Hes 10:33; 4:15; Kum 31:9; 1Fal 8:3; 1Sam 6:15wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata. 3:4 Hes 35:5; Kut 19:12; Kum 28:58; 1Nya 16:30; Za 2:11; 96:9; Ebr 12:28Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa 2,0003:4 Dhiraa 2,000 ni sawa na mita 900. kati yenu na Sanduku.”

3:5 Kut 20:1; Law 11:44; Amu 6:13; 1Nya 16:9, 24; Za 26:7; 75:1; Kut 10:10; Hes 11:18; Yos 7:13; 1Sam 16:5; Yos 2:16Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa kesho Bwana atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”

3:6 Hes 4:15Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao.

3:7 Yos 4:14; 1Nya 29:25; Yos 1:5Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, “Leo nitaanza kukutukuza machoni pa Israeli yote, ili wapate kujua kuwa niko pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Mose. Uwaambie makuhani wanaochukua Sanduku la Agano, ‘Mnapofika kwenye ukingo wa maji ya Yordani, nendeni mkasimame ndani ya mto.’ ”

Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njooni hapa msikilize maneno ya Bwana Mungu wenu. 3:10 Kum 5:26; 1Sam 17:26, 36; 2Fal 19:4, 16; Za 18:46; 42:2; Isa 37:4, 17; Yer 10:10; 23:36; Dan 6:26; Hos 1:10; Mt 16:16; Kum 7:21; Mwa 26:24; Yos 17:15; 24:11; Amu 1:4; 3:5; Kut 3:8; 23:23; Kum 7:1; 9:1; 11:3; Amu 19:11; 1Nya 11:4Hivi ndivyo mtakavyojua ya kuwa Mungu aliye hai yupo katikati yenu, na kwamba kwa hakika atawafukuza mbele yenu hao Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagirgashi, Waamori na Wayebusi. 3:11 Kut 19:5; Kum 14:10; Ay 9:10; 28:24; 41:11; Za 50:12; 97:5; Zek 6:5; Kum 9:3Tazameni, Sanduku la Agano la Bwana wa dunia yote litaingia ndani ya Mto Yordani likiwa limewatangulia. 3:12 Yos 4:2-4Sasa basi, chagueni watu kumi na wawili kutoka makabila ya Israeli, mtu mmoja kutoka kila kabila. 3:13 Yos 4:7; Kut 14:22; Isa 11:15; Za 78:13Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”

3:14 Za 132:8; Mdo 7:44-45; Kut 25:10; 26:30; Hes 10:3; 2Nya 6:41; Ebr 9:4Basi, watu walipovunja kambi ili kuvuka Yordani, makuhani wakiwa wamebeba Sanduku la Agano waliwatangulia. 3:15 2Fal 3:6; Yos 4:18; 1Nya 12:15; Isa 8:7; Mwa 8:22; Yer 12:5; 49:19Wakati huu ulikuwa wakati wa mavuno, nao Mto Yordani ulikuwa umefurika hadi kwenye kingo zake. Ilikuwa kawaida ya Yordani kufurika nyakati zote za mavuno. Mara tu makuhani wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Agano walipofika mtoni na nyayo zao kuzama ndani ya yale maji, 3:16 Za 66:6; 74:15; 114:3; Ay 38:37; Za 33:7; 1Fal 4:12; 7:46; Mwa 14:3; 8:1; Kut 14:22; 2Fal 2:4maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko.

3:17 Yos 4:3-9; Kut 14:22; Yos 2:10Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano la Bwana, wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Mto Yordani, wakati Waisraeli wote wakiwa wanapita hadi taifa lote likaisha kuvuka mahali pakavu.

Read More of Yoshua 3

Yoshua 4:1-24

Ukumbusho Wa Kuvuka Mto Yordani

4:1 Kum 27:2; Yos 2:17Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, Bwana akamwambia Yoshua, 4:2 Yos 3:17; Hes 13:1; 34:18; Yos 1:4-15; 1Fal 18:31“Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja, nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.”

4:4 Yos 3:12Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila, 4:5 Yos 3:17naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Bwana Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli, 4:6 Yos 2:12; Kut 10:2; 12:26; 13:14; Kum 6:20; Za 78:3-6; Isa 38:16kuwa kama ishara katikati yenu. Siku zijazo, wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’ 4:7 Yos 3:13; Kut 28:12; 12:14waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka yalitindika mbele ya Sanduku la Agano la Bwana. Wakati lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.”

4:8 Kut 28:21; Yos 3:17Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kama Bwana alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini. 4:9 Mwa 28:18; Yos 24:26; 1Sam 7:12; Mwa 35:20Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo.

Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu Bwana alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka, na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku la Bwana na makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama. 4:12 Mwa 29:32; 30:11; 41:51; Hes 32:27-29Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamevaa silaha, kama Mose alivyowaamuru. 4:13 Kut 13:18; Hes 32:17Kiasi cha watu 40,000 waliojiandaa kwa vita walivuka mbele za Bwana hadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita.

4:14 Yos 3:7; 1Sam 2:30; 2Nya 32:23; 1Nya 29:12Siku ile Bwana akamtukuza Yoshua mbele ya Israeli yote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Mose.

Basi Bwana akamwambia Yoshua, 4:16 Kut 25:22; Ufu 11:19; Yos 3:15“Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda, wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.”

Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.”

4:18 Kut 14:27; Yos 3:15Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la Bwana. Mara tu walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla.

4:19 Kum 11:30; Yos 5:9; 15:17; 1Sam 11:14-15; Amo 4:4; 5:5; Mik 6:5Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki ya Yeriko. Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’ 4:22 Kut 14:22; Yos 3:17Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’ 4:23 Kut 14:19-22; Neh 9:11; Za 77:16-19; Isa 43:16; 63:12Kwa maana Bwana Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Bwana Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. 4:24 1Fal 8:60; 18:36; 2Fal 5:15; Za 67:2; 83:18; 106:8; Isa 37:20; 52:10; Kut 15:16; 1Nya 29:12; Za 44:3; 89:13; 98:1; 118:15-16; Kut 14:31Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha Bwana Mungu wenu.”

Read More of Yoshua 4

Yoshua 5:1-12

5:1 Kut 4:25; Hes 13:29; Mwa 42:28; Yos 2:9-11; Kut 15:14; Za 48:6; Eze 21:7; 1Fal 10:5Basi wafalme wote wa Waamori magharibi ya Yordani na wafalme wote wa Kanaani waliokuwa kwenye pwani waliposikia jinsi Bwana alivyoukausha Mto Yordani mbele ya Waisraeli hata tulipokwisha kuvuka, mioyo yao ikayeyuka kwa hofu, wala hawakuwa na ujasiri kuwakabili Waisraeli.

Tohara Huko Gilgali

5:2 Kut 4:25; Mwa 17:10-14Wakati huo Bwana akamwambia Yoshua, “Tengeneza visu vya mawe magumu sana na uwatahiri Waisraeli tena.” Kwa hiyo Yoshua akatengeneza visu vya mawe magumu sana na kutahiri Waisraeli huko Gibeath-Haaralothi.5:3 Gibeath-Haaralothi maana yake ni Kilima cha Magovi.

5:4 Hes 1:3; Kum 2:14, 16; Hes 14:29; 26:64Hii ndiyo sababu ya Yoshua kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani baada ya kuondoka Misri. Watu wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, lakini watu wote waliozaliwa jangwani wakiwa safarini toka Misri walikuwa hawajatahiriwa. 5:6 Hes 32:13; Yos 14:10; Za 107:4; Kut 16:35; Hes 14:23-35; Kum 2:14; Kut 3:8Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini mpaka wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati waliondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtii Bwana. Kwa maana Bwana alikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao katika kuapa kutupatia, nchi inayotiririka maziwa na asali. 5:7 Hes 14:31Kwa hiyo akawainua wana wao baada yao na hawa ndio hao ambao Yoshua aliwatahiri. Walikuwa hawajatahiriwa bado kwa sababu walikuwa safarini. 5:8 Mwa 34:25Baada ya taifa lote kutahiriwa, waliendelea kukaa kambini mpaka walipokuwa wamepona.

5:9 Kum 11:30; 1Sam 14:6; Law 18:3; Yos 24:14; Eze 20:7Bwana akamwambia Yoshua, “Leo nimeiondoa aibu ya Wamisri kutoka kwenu.” Basi mahali pale pakaitwa Gilgali hadi leo.

5:10 Kut 12:6; 12:11Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi, wakiwa kambini huko Gilgali katika tambarare za Yeriko, Waisraeli wakaadhimisha Pasaka. 5:11 Hes 15:19; Kut 12:15; Law 23:14; Hes 9:5Siku iliyofuata Pasaka, katika siku ile ile, wakala mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka za kukaanga. 5:12 Kut 16:35Mana ilikoma siku iliyofuata baada ya Waisraeli kula chakula kilichotoka katika nchi; hapakuwa na mana tena kwa ajili ya Waisraeli, ila mwaka huo walikula mazao ya nchi ya Kanaani.

Read More of Yoshua 5