Yoshua 21:20-45, Yoshua 22:1-34 NEN

Yoshua 21:20-45

Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu:

21:21 Yos 17:7; 10:33; 20:7; Mwa 33:19; Amu 9:1; 1Fal 12:1Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, 21:22 Yos 10:10; 1Sam 1:1Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

21:23 Yos 19:44Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni, 21:24 Yos 10:12; 19:45Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

21:25 Yos 12:21Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili.

Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.

21:27 Yos 12:5; Hes 35:6; Kum 4:43; 1Nya 6:71-76Koo za Walawi za Wagershoni walipewa:

kutoka nusu ya kabila la Manase,

Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;

21:28 Mwa 30:18; Yos 19:20; 19:12kutoka kabila la Isakari walipewa,

Kishioni, Daberathi, 21:29 Yos 10:3; 15:34Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

21:30 Yos 17:7; 19:26-28kutoka kabila la Asheri walipewa,

Mishali, Abdoni, 21:31 Yos 19:28Helkathi na Rehobu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

21:32 Yos 12:22; Hes 35:6; Yos 12:22Kutoka kabila la Naftali walipewa,

Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano.

Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

21:34 Yos 19:10; 12:22Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa:

kutoka kabila la Zabuloni,

Yokneamu, Karta, 21:35 Yos 19:15Dimna na Nahalali, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

21:36 Yos 20:8; Hes 21:23; Kum 2:32; Amu 11:20kutoka kabila la Reubeni walipewa

Bezeri, Yahasa, 21:37 Yos 13:18Kedemothi na Mefaathi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

21:38 Kum 4:43; Yos 12:2; Mwa 32:2kutoka kabila la Gadi walipewa,

Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu, 21:39 Yos 13:25Heshboni na Yazeri, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na miwili.

21:41 Hes 35:7; Mwa 49:7; Kum 33:10Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho. Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.

21:43 Kum 34:4; 11:31; 17:14Kwa hiyo Bwana akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. 21:44 Kut 33:14; Kum 6:19; Kut 23:31; Kum 21:10; 7:24Bwana akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao. 21:45 Yos 23:14; Neh 9:8; Isa 49:7-8; Mt 24:35; Lk 21:33Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Bwana kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

Read More of Yoshua 21

Yoshua 22:1-34

Makabila Ya Mashariki Yarudi Nyumbani

22:1 Hes 32:25Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, 22:2 Kum 3:18; Hes 32:20naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Mose mtumishi wa Bwana aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Bwana Mungu wenu aliyowapa. 22:4 Kut 33:14; Hes 32:22; Kum 3:22; Hes 32:18; Yos 1:13-15Sasa kwa kuwa Bwana Mungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Mose mtumishi wa Bwana aliwapa ngʼambo ya Yordani. 22:5 Isa 43:22; Mal 3:14; Yos 23:11; Kum 5:29; 6:5-6, 17Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi wa Bwana alizowapa: yaani kumpenda Bwana Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”

22:6 Mwa 24:60; Kut 39:43; Mwa 47:7; Yos 14:13; 2Sam 6:18; Lk 24:50Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao. 22:7 Hes 32:19, 33; Yos 12:5; 17:2; 14:13; Lk 24:50(Kwa nusu ya kabila la Manase Mose alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao). Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki, 22:8 Kum 20:14; Hes 31:22, 27; Mwa 49:27; 1Sam 30:16; 2Sam 1:1; Isa 9:3akisema, “Rudini nyumbani mwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia wingi wa nguo, nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.”

22:9 Yos 18:1; Hes 32:26Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la Bwana kupitia Mose.

22:10 Yos 18:17; Isa 19:19; 56:7Walipofika Gelilothi karibu na Yordani, katika nchi ya Kanaani, Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakajenga madhabahu ya fahari kubwa huko kando ya Yordani. 22:11 Law 17:8; Kum 13:12; Amu 20:12Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli, 22:12 Yos 18:1kusanyiko lote la Israeli wakakusanyika huko Shilo ili wakapigane vita dhidi yao.

22:13 Hes 25:7; 25:7; Yos 24:33; Kum 13:14; Kut 6:25Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase. 22:14 Hes 1:4Wakatuma pamoja naye watu kumi ambao ni viongozi, mmoja kwa kila kabila la Israeli, kila mmoja aliyekuwa kiongozi katika mgawanyiko wa jamaa miongoni mwa koo za Israeli.

Walipofika Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, wakawaambia: 22:16 Kum 7:3; 1Sam 15:11; Kum 12:13-14“Kusanyiko lote la Bwana lasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwacha Bwana na kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi? 22:17 Hes 23:28; 25:1-9Je, dhambi ya Peori haikutosha? Hata ingawa kulikuja tauni juu ya kusanyiko la Bwana, mpaka leo hii hatujatakasika kutokana na dhambi hiyo! 22:18 Law 10:6; Hes 16:22; Mwa 18:23-25; Yos 7:11-12; 2Sam 1:17; 1Nya 21:1, 14Je, sasa ndiyo mnamwacha Bwana?

“ ‘Kama mkimwasi Bwana leo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli. 22:19 Kut 26:1; Law 17:8-9; Yos 18:1Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya Bwana, mahali Maskani ya Bwana ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya Bwana wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, zaidi ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu. 22:20 Yos 7:1; Za 7:11; Law 10:6; Yos 7:5Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ”

Ndipo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walipowajibu viongozi wa koo za Israeli, wakisema: 22:22 Kum 10:17; Za 50:1; 1Sam 2:3; 16:7; 1Fal 8:39; 1Nya 28:9; Za 11:4; 40:9; 44:21; 139:4; Yer 17:10; Ay 10:7“Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwa Bwana, msituache hai siku hii ya leo. 22:23 Yer 41:5; Kum 12:11; 1Sam 20:16; Za 7:3, 5, 10, 13, 14Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha Bwana na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, Bwana mwenyewe na atupatilize leo.

“Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na Bwana, Mungu wa Israeli? Bwana ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa Bwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha Bwana.

“Hii ndiyo sababu tulisema, ‘Tujiweke tayari na tujenge madhabahu, lakini si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa au dhabihu.’ 22:27 Mwa 21:30; Yos 24:27; Isa 19:20; Kum 12:6Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu Bwana katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika Bwana.’

22:28 Mwa 21:30“Nasi tulisema, ‘Ikiwa wakati wowote watatuambia hilo, au kuwaambia uzao wetu, tutawajibu hivi: Angalieni nakala hii ya madhabahu ya Bwana, ambayo baba zetu waliijenga, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu, bali kama ushahidi kati yetu na ninyi.’

22:29 Yos 24:16; Kut 26:1; Kum 12:13-14“Hili jambo la kumwasi Bwana na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.”

Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko na wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika. 22:31 Law 26:11-12; 2Nya 15:2; Kut 25:8; 29:45; Zek 8:23; Ufu 21:3Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia Wareubeni, Wagadi na Manase, “Leo tunajua kwamba Bwana yuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwa Bwana katika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli na mkono wa Bwana.”

Ndipo Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari na viongozi wakarudi Kanaani kutoka kwenye kukutana kwao na Wareubeni na Wagadi huko Gileadi nao wakatoa taarifa kwa Waisraeli. 22:33 Dan 2:19; Lk 2:28; 1Nya 29:20; 29:30; Neh 8:6Walifurahi kusikia taarifa hiyo, na wakamhimidi Mungu. Wala hawakuzungumza tena habari za kupigana vita dhidi yao ili kuharibu nchi ambayo Wareubeni na Wagadi waliishi.

22:34 Mwa 21:30; Yos 24:27Nao Wareubeni na Wagadi wakayaita yale madhabahu Edi, yaani Shahidi: kwa kuwa itakuwa shahidi kati yetu na ninyi kwamba Bwana ndiye Mungu.

Read More of Yoshua 22