Yoshua 19:1-51, Yoshua 20:1-9, Yoshua 21:1-19 NEN

Yoshua 19:1-51

Mgawo Kwa Simeoni

19:1 Mwa 49:7Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, ukoo kwa ukoo. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. 19:2 Mwa 21:14; 1Fal 19:3; Yos 15:26; 1Nya 4:28; Neh 11:26Ulijumuisha:

Beer-Sheba (au Sheba), Molada, 19:3 Yos 15:28-29Hasar-Shuali, Bala, Esemu, Eltoladi, Bethuli, Horma, Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.

Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii mpaka Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).

Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni ukoo kwa ukoo. 19:9 Mwa 47:9; Eze 48:24Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.

Mgawo Kwa Zabuloni

19:10 Yos 21:7, 34Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo:

Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. 19:11 Yos 12:22Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea mpaka kwenye bonde karibu na Yokneamu. 19:12 Yos 22; 21:28; 1Nya 6:72Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea. 19:14 Mwa 49:13; Hes 34:6-7; Kut 23:31; 1Fal 4:12Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli. 19:15 Yos 21:35; 11:1; Mwa 35:19; Amu 1:30Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

19:16 Eze 48:26; Yos 21:7; Mdo 17:26Miji hii na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa Zabuloni, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Isakari

19:17 Mwa 30:18Kura ya nne ikamwangukia Isakari, ukoo kwa ukoo. 19:18 Yos 15:56; Isa 28:4; 1Fal 1:3; 2Fal 4:8Eneo lao lilijumuisha:

Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, 19:20 Yos 21:28Rabithi, Kishioni, Ebesi, 19:21 Yos 15:34Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi. 19:22 Amu 4:6, 12; 8:18; Za 89:12; Yer 46:18; Yos 15:10Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani. Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

19:23 Yos 17:10; Mwa 49:15; Eze 48:25Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Asheri

19:24 Yos 17:7Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo. 19:25 Yos 11:1; 1Sam 2:16Eneo lao lilijumuisha:

Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu, 19:26 Yos 21:30; 12:22; 1Fal 18:19; 2Fal 2:25Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. 19:27 Yos 15:41Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. 19:28 Yos 21:30; 1Nya 6:74; Hes 13:21; Amu 1:31; 1Nya 6:76; Yos 16:8; Mwa 10:16-19; Yos 11:8Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. 19:29 Yos 18:25; 2Sam 5:11; 24:7; Ezr 3:7; Za 45:12; Isa 23:1; Yer 25:22; Eze 26:2; Amu 5:17; Yos 15:44; Amu 1:31Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, 19:30 Yos 12:18Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

19:31 Mwa 30:13; Yos 17:7; Eze 48:2Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Naftali

Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo:

19:33 Amu 4:11; Yos 15:11Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mti mkubwa ulio katika Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. 19:34 1Nya 6:75; Kum 33:23Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki. 19:35 1Nya 2:55; Yos 11:2; Hes 13:21; 1Fal 14:25; Yer 39:5; Mk 6:53Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, 19:36 Yos 18:25; 11:1Adama, Rama, Hazori, 19:37 Yos 12:22; Hes 21:33Kedeshi, Edrei, na En-Hasori, 19:38 Amu 1:33; Yos 15:10Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.

19:39 Kum 33:23; Eze 48:3Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Naftali, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Dani

Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, ukoo kwa ukoo. 19:41 Yos 15:33; Amu 13:2Eneo la urithi wao lilijumuisha:

Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, 19:42 Amu 1:35; Yos 10:12; 1Fal 4:9Shaalabini, Aiyaloni, Ithla, 19:43 Mwa 38:12; Yos 13:3Eloni, Timna, Ekroni, 19:44 Yos 21:23; 1Fal 15:27; 16:15; 9:18; 2Nya 8:6Elteke, Gibethoni, Baalathi, 19:45 Yos 21:24; 1Nya 6:69Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, 19:46 2Nya 2:16; Ezr 3:7; Yon 1:3; Mdo 9:36Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.

19:47 Amu 18:1, 7, 14; Kum 3:14; Amu 18:27-29; Mwa 49:17(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)

19:48 Mwa 30:6; Hes 26:54; Mdo 17:26Miji hii na vijiji vyake ndio iliyokuwa urithi wa kabila la Dani, ukoo kwa ukoo.

Mgawo Kwa Yoshua

Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao, 19:50 Yos 24:30; Amu 2:9kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera19:50 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi, ona Yos 24:30; Amu 2:9. ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.

19:51 Yos 23:4; 14:1; 18:10; Mdo 13:19; Hes 34:17; Amu 21:19; Za 78:58Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

Read More of Yoshua 19

Yoshua 20:1-9

Miji Ya Makimbilio

(Hesabu 35:9-34)

Ndipo Bwana akamwambia Yoshua, 20:2 Kut 21:13; Hes 35:6-14; Kum 4:41-43; Ebr 6:18-19“Waambie Waisraeli, watenge miji mikubwa ya kukimbilia, kama nilivyokuagiza kupitia Mose, 20:3 Law 4:2; Hes 35:12ili mtu yeyote atakayemuua mtu kwa bahati mbaya na pasipo kukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi wa damu.

20:4 Mwa 23:10; Rut 4:1; Yer 35:7; Yos 7:6“Anapokimbilia mojawapo ya hii miji mikubwa atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao. 20:5 2Nya 10:1; Lk 1:39Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru. 20:6 Hes 35:12Huyu aliyeua atakaa kwenye mji mkubwa huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”

20:7 Yos 12:22; Mwa 12:6; 35:27; Yos 10:36; Lk 1:36; Yos 21:11, 32; 1Nya 6:76Basi wakatenga Kedeshi katika Galilaya kwenye nchi ya vilima ya Naftali, Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-Arba (yaani Hebroni) kwenye nchi ya vilima ya Yuda. 20:8 Yos 21:36; 1Nya 6:78-80; Yos 12:2-5; 1Nya 6:71Katika upande wa mashariki mwa Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase. 20:9 Law 4:2; Kut 21:13; Hes 35:13Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji mikubwa hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.

Read More of Yoshua 20

Yoshua 21:1-19

Miji Kwa Walawi

21:1 Yos 14:1; Hes 34:17; Yos 17:4; 24:33Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli 21:2 Yos 18:1; Hes 35:2-3; Law 25:2; Yos 14:4huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwana aliamuru kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.” Hivyo kama vile Bwana alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe.

Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini. Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

21:6 Hes 3:17; Mwa 30:18; Yos 17:7Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

21:7 Kut 6:16; Yos 19:10Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

21:8 Mwa 49:7; Hes 35:2-3; Yos 18:6; Mit 16:33Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose.

Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

21:11 Yos 15:48-50Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) 21:12 Yos 15:13Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji mkubwa walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

21:13 Hes 35:6; 33:20; 1Nya 6:57Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna, 21:14 Yos 15:48-50; Kum 4:43; 1Fal 22:3Yatiri, Eshtemoa, Holoni, Debiri, 21:16 Hes 34:11; Yos 15:55; 15:10Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili.

21:17 Yos 9:3; Neh 11:31; 1Nya 6:55; Mwa 23:2; Yos 14:15; 2Sam 2:1-3; Lk 1:39Kutoka kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba, 21:18 2Sam 23:27; 1Fal 2:26; Ezr 2:23; Neh 7:27; 11:32; Isa 10:30; Yer 1:1; 11:21; 32:7; Yos 14:14Anathothi na Almoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

21:19 2Nya 31:15; Yos 20:7-9; 15:54; Isa 37:8Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

Read More of Yoshua 21