Yoshua 17:1-18, Yoshua 18:1-28 NEN

Yoshua 17:1-18

Mgawo Wa Nusu Nyingine Ya Manase Upande Wa Magharibi

17:1 Hes 1:34; 1Nya 7:14; Mwa 41:51; 50:23; Yos 12:2, 5Huu ndio mgawo wa kabila la Manase kama mzaliwa wa kwanza wa Yosefu, yaani kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase. Makiri alikuwa baba wa Wagileadi, ambao walipokea Gileadi na Bashani kwa sababu Wamakiri walikuwa askari wakuu. 17:2 Hes 26:30; Amu 6:11, 34; 8:2; 1Nya 7:14-19; Hes 27:1Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yosefu kwa koo zao.

17:3 Hes 27:1; 26:33Basi Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase hakuwa na wana waume ila mabinti tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. 17:4 Hes 27:5-7; Yos 14:1Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “Bwana alimwagiza Mose atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la Bwana. 17:5 Yos 13:30-31Fungu la Manase lilikuwa na sehemu kumi za nchi, licha ya Gileadi na Bashani mashariki mwa Yordani, kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi miongoni mwa wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki.

17:7 Yos 19:24, 31; 21:6, 30; Amu 1:31; 5:17; 6:35; 7:23; Yos 16:6; Mwa 12:6; Yos 21:12; 24:25Eneo la Manase lilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ule ulielekea upande wa kusini kutoka pale kujumuisha watu walioishi En-Tapua. 17:8 Yos 12:17; 15:34(Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) 17:9 Yos 16:8Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde na kuishia kwenye bahari. 17:10 Mwa 30:18; Eze 48:5Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki.

17:11 Amu 1:27; 1Sam 31:10; 2Sam 21:12; 1Fal 4:12; 1Nya 7:29; 2Fal 9:27; Yos 11:2; 1Sam 28:7; Za 83:10; Yos 12:21; 1Fal 9:15; Eze 48:4Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori,17:11 Ndiyo Nafoth-Dori. Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).

17:12 Yos 15:63; Hes 26:29; 32:39, 41Lakini Wamanase hawakuweza kuimiliki miji hii, kwa kuwa Wakanaani walikazana kuishi katika maeneo hayo. 17:13 Amu 1:27-28; Kut 23:29-33; Amu 1:27, 28Hata hivyo, Waisraeli walivyoendelea kupata nguvu waliwatumikisha Wakanaani na kuwatia katika kazi za kulazimishwa, lakini hawakuwafukuza kabisa.

Kabila La Yosefu Lakataa

17:14 Hes 26:28-37; Yos 16:4; Mwa 48:22; 48:19Watu wa Yosefu wakamwambia Yoshua, “Kwa nini umetupa sisi mgawo mmoja tu na sehemu moja tu kuwa urithi? Sisi tu watu wengi sana, na Bwana ametubariki kwa wingi.”

17:15 2Sam 18:6; Yos 3:10; Mwa 14:5; Yos 15:8; 18:16; 2Sam 5:18; 23:13; 1Sam 17:5Yoshua akajibu, “Kama ninyi ni wengi sana, na kama nchi ya vilima ya Efraimu ni ndogo sana kwenu, pandeni msituni mkafyeke eneo kwa ajili yenu wenyewe huko kwenye nchi ya Waperizi na Warefai.”

17:16 Amu 1:19; 4:3, 13; Yos 15:56; 1Sam 29:1; Amu 6:33; 1Fal 4:12; 18:46Watu wa Yosefu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wanayo magari ya vita ya chuma, wote wa Beth-Shani na miji yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.”

17:17 Eze 48:5Lakini Yoshua akanena na nyumba ya Yosefu, yaani Efraimu na Manase: “Ninyi ni wengi sana na wenye nguvu sana. Hamtakuwa na mgawo mmoja tu, 17:18 1Sam 1:1; Kum 20:1; Yos 11:4-6; 13:6; Rum 8:31; Ebr 13:6bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”

Read More of Yoshua 17

Yoshua 18:1-28

Mgawanyo Wa Nchi Iliyobaki

18:1 Yos 19:51; 21:2; Amu 18:31; 21:12; 1Sam 1:3; 3:21; 4:3; 1Fal 14:2; Za 78:60; Yer 7:12; 26:6; 41:5; Kut 27:21; 40:2; Mdo 7:45Kusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.

18:3 Amu 18:9; Sef 3:16; Mt 20:6; Yn 6:27; Flp 3:13-14Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? 18:4 Mik 2:5Chagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia. 18:5 Yos 15:1; 16:1-4Mtaigawanya hiyo nchi katika sehemu saba. Yuda atabaki katika eneo lake upande wa kusini na nyumba ya Yosefu katika nchi yake upande wa kaskazini. 18:6 Law 16:8; Yos 14:2Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura kwa kura mbele za Bwana Mungu wetu. 18:7 Yos 13:33; 13:8Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Bwana ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Mose mtumishi wa Bwana aliwapa.”

Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuandika vizuri kuhusu hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo kuihusu. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Bwana.” Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo. 18:10 Hes 34:13; Yer 7:12; Hes 33:54; Yos 19:51; Mit 16:33Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za Bwana, na hapo akagawanya ile nchi kwa Waisraeli kufuatana na mgawanyo wa kabila zao.

Mgawo Kwa Benyamini

Kura iliangukia kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yosefu.

18:12 Yos 8:15; 7:2Upande wa kaskazini mpaka wao ulianzia pale Yordani, kupitia kaskazini ya mteremko wa Yeriko na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni. 18:13 Mwa 28:19; Yos 12:9; Hes 32:3; Yos 16:5; Amu 1:23; Hes 18:20; Kum 10:9; Eze 44:28Kutoka hapo ulikatiza kwenye mteremko wa kusini mwa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya Chini.

18:14 Yos 10:10; 9:17; 1Nya 13:6Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi.

18:15 Yos 15:9Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa. 18:16 Yos 17:15; 15:7-8; 2Fal 23:10; 2Nya 28:3; 33:6; Isa 30:33; Yer 19:2; Yos 15:8Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Refaimu. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli. 18:17 Yos 22:10; 15:6-7Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea mpaka Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 18:18 Yos 15:6; 11:2; 16:1Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba. 18:19 Yos 15:6; Mwa 14:3Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini.

18:20 1Sam 9:1; Yos 21:4, 17Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki.

Hii ilikuwa ndiyo mipaka iliyoonyesha urithi wa koo za Benyamini pande zote.

18:21 Yos 6:26; 1Fal 16:34; Lk 10:30Kabila ya Benyamini, ukoo kwa ukoo, ilikuwa na miji mikubwa ifuatayo:

Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi, 18:22 Yos 15:6; 2Nya 13:4; Yos 16:1Beth-Araba, Semaraimu, Betheli, 18:23 Kum 2:23; Amu 6:11, 24; 8:27, 32; 9:6; 1Sam 13:17Avimu, Para na Ofra, 18:24 Yos 21:17; 1Sam 13:3, 16; 14:5; 1Fal 15:22; 2Fal 23:8; Isa 10:29; Amu 19:12-16; Ezr 2:26Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

18:25 Yos 10:40; Amu 4:5; 19:13; 1Sam 2:11; 7:17; 25:1; Neh 11:33; 1Fal 15:17, 21; Neh 7:29Gibeoni, Rama na Beerothi, 18:26 Yer 11:3; Yos 9:17; Ezr 2:25; Neh 7:29Mispa, Kefira, Moza, Rekemu, Irpeeli, Tarala, 18:28 2Sam 21:14; Yos 15:8; 10:1; 15:57; 9:17; Eze 48:23; Mwa 46:21; Mdo 17:26Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake.

Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.

Read More of Yoshua 18