Yoshua 13:1-33, Yoshua 14:1-15 NEN

Yoshua 13:1-33

Sehemu Za Kanaani Ambazo Hazijatwaliwa

13:1 Mwa 24:1; Yos 14:10; 23:1-3; 1Fal 1:1Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, Bwana akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa.

13:2 Mwa 10:14; Amu 3:31; Yos 12:5“Nchi iliyosalia ni hii: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: 13:3 1Nya 13:5; Isa 23:3; Yer 2:18; Yos 15:11; 19:43; Amu 1:18; 1Sam 5:10; 7:14; Amu 3:3; 16:5, 18; 1Sam 6:4, 17; Isa 14:29; Eze 25:15; Yos 11:22; Amo 3:9; Amu 14:19; 2Sam 1:20; Kum 2:23; 13:4; Yos 12:18; Mwa 14:7; 15:16kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani (maeneo yale matano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi); kuanzia kusini, nchi yote ya Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na eneo la Waamori, 13:5 1Fal 5:18; Za 83:7; Eze 27:9; Yos 11:17; Kum 3:8; Hes 13:21; 34:8; Amu 3:3eneo la Wagebali;13:5 Yaani eneo la Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Lebanoni yote kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi.

13:6 Yos 11:8; Za 80:8; Hes 33:54; 34:13; Amu 2:12; Yos 14:1, 2“Na kuhusu wakaaji wote katika maeneo ya milima, kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza watoke mbele ya Waisraeli. Hakikisha umegawa nchi hii kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuagiza, 13:7 Yos 11:23; Za 78:55sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Mwa Yordani

13:8 Yos 12:6; 18:7; Hes 32:33; Kum 3:12; Yos 12:6; 18:7Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa Bwana alivyowagawia.

13:9 Hes 32:34; Kum 2:36; Amu 11:26; 2Sam 24:5; Yer 48:8, 21; Hes 21:30; 32:3; Isa 15:2Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, likijumlisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni, 13:10 Yos 12:2; Hes 21:24nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamoni. 13:11 Yos 12:2-5Vilevile ilijumlisha Gileadi, eneo la Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote ikienea hadi Saleka: 13:12 Kum 1:4; Yos 12:4; Mwa 14:5; Kum 3:5, 11; Hes 21:24yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao. 13:13 Yos 12:5; Kum 3:12-15Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii.

13:14 Kum 18:1-2; Yos 14:2; Hes 18:20; Kum 10:9Lakini kwa kabila la Lawi, Mose hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa Bwana, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.

Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo:

13:16 Yos 12:2; 1Sam 30:28; Hes 21:30; Isa 15:2; Kum 3:12Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba 13:17 Hes 32:3; 22:41; 1Nya 5:8; Yer 48:23; Eze 25:9hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, 13:18 Hes 21:23; Kum 2:26; Yos 21:37; Yer 48:21Yahasa, Kedemothi, Mefaathi, 13:19 Hes 32:37; 32:3Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, 13:20 Kum 3:29Beth-Peori, materemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi: 13:21 Mwa 25:2; Hes 25:15; 31:8; Kum 3:10; Hes 21:24; 31:8miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni. Mose alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile. 13:22 Hes 22:5; Mwa 30:27; Hes 23:23; 2Pet 2:15; Ufu 2:14Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemuua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa mchawi. 13:23 1Nya 5:7Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii na vijiji vyake ndiyo iliyokuwa urithi wa Wareubeni ukoo kwa ukoo.

Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:

13:25 Hes 21:32; Yos 21:39; 12:2; Kum 3:11; Amu 11:13; 2Sam 11:1; 12:26Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni iliyoenea hadi Aroeri, karibu na Raba; 13:26 Hes 21:25; Yer 49:3; Mwa 32:2; Yos 10:3na kuanzia Heshboni mpaka Ramath-Mispa na Betonimu, na kutoka Mahanaimu hadi eneo la Debiri; 13:27 Hes 32:3; Mwa 33:17; Amu 12:1; Za 48:2; Hes 34:11; 1Fal 7:46; Kum 3:17; Yos 11:2; Mt 14:34; Lk 5:1na katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki mwa Mto Yordani, eneo inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi13:27 Yaani Bahari ya Galilaya.). 13:28 Mwa 46:16; Hes 32:3; Eze 48:27Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Gadi ukoo kwa ukoo.

Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo:

13:30 Mwa 32:2; Hes 21:33; Yos 12:4; Hes 32:41Eneo lililoenea kuanzia Mahanaimu, na kujumlisha Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini, 13:31 Hes 21:33; Mwa 50:23; Yos 17:5nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.

13:32 Hes 26:3; 22:1Huu ndio urithi alioupeana Mose wakati alipokuwa katika tambarare za Moabu, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko. 13:33 Hes 26:62; 18:20; Yos 18; 7; Eze 44:28Lakini kwa kabila la Walawi, Mose hakuwapa urithi; Bwana Mungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

Read More of Yoshua 13

Yoshua 14:1-15

Mgawanyo Wa Nchi Magharibi Mwa Yordani

14:1 Yos 11:23; Za 16:6; 136:21; Kut 6:23; Yos 21:1; Hes 26:53; 34:17-18; Yos 19:51Basi haya ndiyo maeneo Waisraeli waliyopokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliwagawia. 14:2 Law 16:8; Hes 34:13; Za 16:5; Mit 16:33; 18:18Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama Bwana alivyoamuru Mose. 14:3 Hes 32:33; 34:14; 35:2; Yos 13:14Mose alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine, 14:4 Mwa 41:54; Amu 1:29; Hes 35:2-3; Yos 21:2kwa kuwa wana wa Yosefu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe wao. 14:5 Hes 34:13; 35:2; Yos 21:2; Eze 45:1-8; 48:8, 22Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vile Bwana alivyomwagiza Mose.

Kalebu Anapewa Mji Wa Hebroni

14:6 Kum 11:30; Hes 13:6; 14:30; Kum 33:1; Hes 14:38; Yos 15:17; Kum 1:19Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Bwana alimwambia Mose mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi. 14:7 Yos 15:6; Hes 13:17; 13:30; 14:6-9Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Mose mtumishi wa Bwana, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni. 14:8 Hes 13:31; 14:24; 32:12; Kum 1:36; Ufu 14:4Lakini ndugu zangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote. 14:9 Kum 11:24; Hes 14:24; Yos 1:3; Hes 13:22Hivyo katika siku ile, Mose akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata Bwana Mungu wangu kwa moyo wote.’

14:10 Hes 11:28; 14:30; Yos 5:6; 13:1; Hes 14:30; Kum 31:2; Za 90:10“Sasa basi, kama vile Bwana alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na mitano tangu wakati alipomwambia Mose jambo hili, wakati Waisraeli wakiwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo, nina umri wa miaka themanini na mitano! 14:11 Kum 34:7; Mwa 15:15Bado ninazo nguvu kama siku ile Mose aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule. 14:12 Hes 14:24-28; 13:33; 1Sam 14:6; 2Nya 14:11, 12; Za 18:32; 44:3; Rum 8:31; Flp 4:13; Yos 15:14; Amu 1:10Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Bwana aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwako huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye maboma, lakini, kwa msaada wa Bwana, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.”

14:13 Yos 22:6-7; 1Sam 30:14; Mwa 23:19; Yos 10:36; Amu 1:26; 1Nya 6:56Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, na akampa Hebroni kama urithi wake. 14:14 Hes 14:24Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama Bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote. 14:15 Mwa 23:2; Yos 15:13; 11:23; Amu 3:11; 1Fal 4:24; 5:4; 1Nya 22:9(Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kutokana na huyo Arba ambaye alikuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.)

Kisha nchi ikawa na amani bila vita.

Read More of Yoshua 14